Chadema kuelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuelekea 2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkono, Mar 31, 2011.

 1. M

  Mkono JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kutokana na chadema kukubalika kwa sehemu kubwa ya nchi hii hasa upande wa bara kwa mikoa ya kaskazini ,kanda ya ziwa ,Magharibi(Kigoma) na kwa kiasi flani nyanda za juu ni vizuri zaidi kwa sasa nguvu kubwa ikaelekezwa maeneo ya mikoa ya kati kama Singinda,Dodoma na Tabora huku mikakati na mbinu za hali ya juu zikihitajika kwa upande Tanzania visiwani kupata watu sahihi wa kuimarisha chama maeneo hayo.
  Moja ya njia za kuanza kutekeleza mkakati huo ni kutumia uchaguzi wa BAVICHA unaotarajiwa kufanyika mwaka huu,kwa mara ya kwanza ningefarijika kuona mwenyekiti wa BAVICHA akitokea ZANZIBAR na kama siyo hivyo basi na iwe DODOMA.
  NI MTAZAMO TU!
   
 2. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Heading yako ni nzuri sana inatakiwa kuwe na mjadala wa CHADEMA kuelekea 2015 jambo ambalo huwezi kutenganisha na uchaguzi wa BAVICHA. Ila kuzungumzia uchaguzi wa BAVICHA na kusema mwenyekiti ataoke kutoka mikoa miwili tu napata wasiwasi kuwa wewe au rafiki zako wanaogombea wanatoka mikoa hiyo miwili. Wakau ungetaja kanda na si mkoa. Hata hivyo, kuna wakati tunaangalia uwezo wa mtu bila kuangaliza kanda anayotoka. Katika haionyeshi kuwa uongozi wa BAVICHA utaangalia kanda fulani.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA KIANDAE MAZINGIRA NA KUTOA MFANO NCHINI JUU YA NAMNA YA KUENDESHA
  SIASA KISASA KWA MISINGI YA UWAZI NA USHINDANI ZAIDI


  Nimeafiki mapendekezo yako kwa kuwa yanania njema sana hivyo yanafikirika lakini chini ya alama zote za COMPETITIVE POLITICS ambayo ndio kiini cha mfumo wa vyama Vingi nchini.

  Nakubaliana na wewe kwamba vijana wenzetu wa Tanzania Visiwani wapate nafasi na uhalali wa kuzungumza ndani ya chama chao CHADEMA tena kwa kinywa kipana sana tu baada ya wao kuwekwa kifungoni kwa miaka mingi na wajanja wanaoeneza siasa za udini nchini.

  Hadi leo hii vijana kote nchini wamethihirisha wazi kwamba tu kitu kimoja sana kama taifa na vile vile kama wazulumiwa na kwamba wa utawala wa KIFISADI kote nchini bila ajira wala kutendewa haki kila kona. Nasema uenyekiti BAVICHA itumike kutuunganisha zaidi Ki-Muungano na Vijana wenzetu kule Zanzibar (Dodoma hapana) ukizingatia kwamba kazi ilioko mbele yetu si lelemama. Ila tu kiongozi huyo asiteuliwe bali ni kwamba apatikane kwa njia ya ushindani mkali na kinyanganyiro cha wazi sana toka huko Zanzibar.

  Binafsi kama mtu angeniuliza basi ningesema kiongozi (Mwenyekiti toka Zanzibar), kama ambavyo pia nafikiria viongozi wengine wa ngazi mbalimbali katika chama kote nchini, huyo awe na sifa zifuatazo: (1) mwanamama, (2) kahitimu japo ka-digri ya kwanza, (3) mewahi kutumikia wananchi wa ngazi zozote kama kiongozi, (4) awe anaamini katika falsafa ya CHADEMA ya siasa za 'Nguvu na Mamlaka ya Umma' katika kujiletea maendeleo nchini, (5) awe ni mtu mwenye rekodi njema katika ujumla wa mienendo yake, (6) mtu mwenye msimamo thabiti (ipimwe kwa rekodi yake) na mawazo huru, (7) muumini katika ukweli kwamba akina mama wanaweza hata bila kutumikia ufisadi.

  Ndio, nasema kwamba ili BAVICHA iwe ni chombo tofauti kabisa chenye kutegemewa kuwa na (i) NGUVU, (ii) TASWIRA YA CHOMBO CHA VIJANA WA ULIMWENGU WA UTANDAWAZI KULETA MABADILIKO MAKUBWA like no other na bado wakaonyesha NIDHAMU YA HALI YA JUU KWA CHAMA NA WANANCHI KWA UJUMLA ni kwamba napendekeza kiongozi wa BAVICHA (8) awe ni mtu mbaye anachukia ufisadi, mizengwe, fitina na siasa tupu katika maswala ya maendeleo ya umma, (9) mtu asiye na dalili zozote za kibaguzi kidini, jinsia, kikanda wala kabila, (10) awe tayari ku-sign Perfomance Contract na Katibu Mkuu wa CHADEMA akiwa ndiye mtendaji mkuu wa chama (11) awe ni muumini katika kuletwa kwa mabadiliko ya Kikatiba ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (12) mbunifu, mwenye mpangilio mzuri wa kazi na mwenye kujituma katika shughuli zake bila kulaza kaziwala kusukumwa ... na kadhalika.

  Njia sahihi ya kuwapata viongozi hawa natamani iwe mchakato mgumu sana, ya kidemokrasia ambayo kwanza usaili wake wa awali (Screening Interview) ipewe an independent and dependable non-partisan professional body kama vile PriceWatersCoopers ifanye na kwamba kila anayetamani kuwa kiongozi aruhusiwe bila kikwazo kisha aingie kwenye kinyang'anyiro cha wazi bila zengwe.

  Nawambia tukifanya hivi wala hatutopata bora vingozi bali ni viongozi bora tupu, wkomavu na wanaojua kitu gani wanatakiwa kukifanyia CHADEMA na taifa hili. Pili, itazuia ushawishi wa mwanasisa kupenyeza watu wake na matokeo yake CHADEMA kufanikiwa kujenga a formidable institution na wala si a collection of political factions under the same roof. Nafurahi kwamba vingozi wa ngazi za CHADEMA kama vile Wazee Edwin Mtei, Bob Makani, Dr Slaa, Mzee Ndesamburo, Prof Baregu, Dr Mkumbo, Mhe Tundu Lissu na Halima Mdee wanaelewa fika point yangu hapa.

  Mwisho wa siku BAVICHA inaandaliwa mafunzo makali sana juu ya skills zinazohitajika kwa kiongozi bora, namna ya kufanya kazi kwa tija, kuhudumia umma wa wapiga kura kwa uso wa bashasha kiukweli wakati wote, mbinu za kutatua changamoto mbali mbali katika ngazi za nafsi, familia, chama na jamii kwa ujumla, mbinu za kujenga akili ya kijasiriamali jamii ili kuwa chachu wa maendeleo hata pale ambapo wengine ndio hivo hawaoni mlango wa matumaini tena, mbinu za kutayarisha michanganuo wa miradi, taratibu za kuitisha na kuendesha mkutano wenye tija, taratibu za kutoa taarifa mbaya kwa jamii, mbinu za kuandika hutuba za kila aina na namna ya kuhutubia katika jamii yenye sura mbali mbali ... na kadhalika.

  Endapo yote haya yatafanyika kwa CHADEMA kuwekeza vya kutosha katika kutafuta taasisi bora zenye kuwapa huduma bora basi nasema CHADEMA kitakua ni moto wa kuotea mbali zaidi nchini.

   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mbona unanipa mashaka. Huo ukanda unaosemwasemwa huko CHADEMA unataka kuupaka mafuta na kuubariki? Yangu macho
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Chadema inatakiwa iangalie sana.Kwanza CHADEMA iweke mikakati na si kuwa chama cha kubeba makapi yaliyotemwa CCM tu
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  nakuaminia mkuu! Kwel uwezo 2nao!
   
Loading...