Nimewahi kusema huko nyuma kwamba watanzania wanakila kitu isipokuwa Viongozi.
Nakubaliana na wewe kwa hoja ya pili kwamba kuna madhira yanatusibu kwa vile tu viongozi wanapenda kufikiri kwa niaba yetu badala ya kutushirikisha. Yapo matatizo ktk jamii tunamoishi yanahitaji ushirikishwaji wa watu tu. Kwa mfano:
- Usafi wa mtaa
- kuziba/kufukia mazalia ya mbu
- ukarabati mdogo wa barabara za mtaa (za vumbi)
- Usafi kwenye maeneo ya wazi ili watoto wacheze mahali safi n.k
Tunahitaji kusikilizwa na kutoa maoni juu ya maendeleo yetu wenyewe.
Kama CDM watafanya hivi, ntakuwa wa kwanza kuomba kadi ya uanachama na itakuwa mara yangu ya kwanza kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
hivi haswa ndio vitu vya msingi vya kuanzia itasaidia sana kuwaweka viongozi wetu sawa, na kujua majukumu yao kwa jamii maana wanachokifanya sas hivi hakieleweki kabisaaaaaaaaa(e.g unakuta mwenyekiti wa kitongoji hajui hata taka za home kwake zinatupwa wapi anachojua ni kudai posho za vikao)