Pata darsa dogo:
Mathayo 15.21-28
Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina. Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa." Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi: "Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Mathayo 7.6
Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu. Kama asemavyo Isaac Asimov katika kitabu chake Guide to the Bible (Uwongozi kwa Biblia):
"Suala liliopo ni nani hao mbwa na nguruwe wnaokusudiwa katika mstari huu? Yaweza kuwa maana ya mstari huu ni kuwa haifai kufunza ukweli wa dini kwa wale wasiotubu katika kejeli zao, au wale waliozama katika madhambi, lakini hayo hayaelekei kabisa. Basi mtu amfundishe nani? Wale waliokwisha amini? Yesu mwenyewe anakanya hayo, kwani aliposhutumiwa kuwa anachanganyika na wenye dhambi ananukuliwa kusema:Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.
Nakushangaa wewe unayeijua biblia hayo huyaoni.