Chadema kinafuata siasa gani?

mpingauonevu

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
623
430
Ukiacha muhemuko wa kuitoa CCM madarakani naanza kupata wasiwasi wa nini zitakuwa ni policy za kiuchumi za CHADEMA. Nikifuatilia mikutano yao CDM wanajipambanua kama CENTRE-RIGHT PARTY. Mpaka sasa sielewi hizo ni policy gani. Mimi naelewa mbili tu UJAMAA na UBEPARI. Sasa leo CDM wanamtaja nyerere kwani wao ni wajamaa? wakiikosoa CCM kwani ubepari si ndio CCM wanafanya na CDM si ndio watafuata? WASOMI WA HIZI SIASA HEBU NIELEWESHENI NDIO ZIKOJE? angalizo:kama huna cha kuchangia tafadhali pita tu matusi yasijeanza hapa maana kuna watu hawaangalii kesho wao wanaona leo tu!
 
kama sijakosea ni sera za mlengo wa kati au za kiribelali yaani sio kibepari wala kijamaa, so ni mchanganyiko i.e sera zinatoa fursa kwa watu binafsi na serikali kumiliki njia kuu za uchumi eg viwanda
 
hebu katafute Ilani ya Uchaguzi ya 2010 ya Chadema na Katiba yao usome uelewe.
mkuu hivyo vitu nimetafuta mbeya na iringa nimeambiwa vimekisha nimekuja hadi dsm kinondoni makao makuu ya cdm nimeambiwa vitu ivyo vimekwisha so kama utakuwa na ufafanuzi ntashukulu zaidi !
 
Ni swali zuri bora wenye kujua sera za CHADEMA wakaja kulieleza hili. CCM wanajipambua kama Chama cha mlengo wa kushoto, huku sera zao kizikiwa zimebadilika kwenda exteme right bado wanajitambulisha kama chama chenye mlengo wa kushoto. Kama CHADEMA kweli ni cetral-right, kipi chama cha kuwatetea watu wenye mlengo wa kushoto. Kuna haja kumbe kuunda chama cha siasa chenye kutetea watu wa mlengo wa kushoto ambao wamejosa mtetezo mpaka sasa
 
Back
Top Bottom