CHADEMA kina wanachama wangapi?

Wapiga kura ni zaidi ya uanachama.
 
Wacha kupayuka hapa tunakwenda kwa fact, Dr Lwaitama ni miongoni mwa Wanachama millioni 5 wa CCM wewe hujui uliongealo hapa, hao Maprofesa wako waliwahi kuvumbuwa hata Sindano?
 
na kuna watu wana kadi zote
za ccm na chadema

Mimi ni mwana CCM lakini mwaka 2000 sikuichagua ccm kwenye uchaguzi wowote, 2005 na 2010 ndo kabisaaaaa, na kadi nailipia ila sitawapigia kura hadi naondoka ulimwenguni
 

Usifanye mchezo na Lowassa mkuu. Huoni mawazo ya Pasco na Mzee Mwanakijijiyanavyofanana siku hizi?
 
Last edited by a moderator:

ukiniita mjinga kwa mtazamo wako inaweza kuwa uko sawa,inategemea kwako mjinga ni mtu wa aina gani...ni kama mie nikisema leo nimegundua Matola ni MNAFIKI..anataka uku na uku..kwako wewe sijui utachukuliaje MNAFIKI maana kuwa vyama viwili kwa wakati mmoja kwako inaweza kuwa ndio ujanja.
 
Hivi nikikuuliza swali dogo tu unaweza kunijibu?

Ni kwa nini Chadema wakati inapigania kuchukuwa dola mwaka 2010 wewe ulikuwa bize kuhamasisha watu wajiunge na CCJ?

Mkuu CCJ inahusikaje hapa?
 
Ndio maana nikasema wewe huna akili, ni nani aliyekwambia mimi ni Mwanachama wa Chadema? au siku hizi kuipinga CCM tafsiri yake wewe ni Mwanachama wa Chadema? hebu format upya ubongo wako naona mishipa yako ya utambuzi ilishakufa.
 
Mkuu CCJ inahusikaje hapa?
Wewe ni Member hapa tangu 2009 unashangaa CCJ inahusikaje hapo? ni nai alikuwa mpiga debe mkuu wa CCJ? ni kwa nini hakuipigia debe Chadema ambayo ilikuwa tayari imekubaliwa na Watanzania? je hakuwawaamini Chadema au alitumwa na nani?
 
Tuache ushabiki hoja hii ni nzito sana na ina ukweli ndani yake.vyama vya upinzani vinatakiwa kuweka wazi vina wanachama wangapi na mtandao ukoje kuanzia mashina,matawi,kata,jimbo,wilaya,mkoa na Taifa.Chadema haina mtandao wa kutosha Vijijini je itachukuaje dola?ni nani atalinda kura zisiibiwe ?
 
Siasa ni sayansi na siasa ni sanaa.
Hili neno MM. nafkiri kuwa sayansi mojawapo ni kujua mfano kama uchaguzi ungekuwa leo CDM ingepata kura ngapi dhidi ya zile za CCM na vyama vingine. Kisha tutafute maana ya hizo kura na jinsi tunavoweza kujipanga kuongeza kura zaidi, sanaa maana yake ni zile njia za kukifanya chama kionekane chafaa mbele ya wtz walio wengi. hiyo itafanyika katika kampeni na propaganda. katika sanaa ni vema kuepuka kuonekana cdm ni chama cha vurugu na kuwahakikishia watz kuwa ndo chenyewe kitakachowakomboa. hapo twaweza sema siasa ni sayansi na sanaa. kama nimekosea nakubali kusahihishwa
 

Labda sasa ninaweza kuona wapi Mzee Mwanakijiji is coming from, kweli muelekeo wa CHADEMA kisiasa labda mbinu na mikakati yao itafafanuliwa na idadi ya wanachama na jinsi walivyosambaa strategically
 
Kifupi Cdm kijue kinatoka wapi, kiko wapi na kinaeleekea wapi. kuelekea wapi kunatokana zaidi na ulipo na si lazima ulikokusudia kwenda pekee. maana yake, mfano, kama unataka shs milioni moja baada ya muda fulani na sasa una shs 500 tu na huna njia za uhakika kupata hizo zilizobaki lengo litakuwa ni zuri lakini hapo ulipo ni tatizo vema ungekuwa na shs 500,000. CDM hapa tulipo ni aje? tunaweza kujadili hoja ya MM kwa namna hii.
 
Kimsingi idadi ya wanachama wa CDM haijulikani au ni siri.

Wanachama wa Chadema hawaeleweki inategemea na maandamano na mikutano ndio utawaona baada ya mikutano na maandamano wanapotea...kimsingi hawajajiandikisha kupiga kura mfano daraja mbili ngome ya Chadema lakini watu 10,000 wamegoma kupiga kura.
 
Kimsingi idadi ya wanachama wa CDM haijulikani au ni siri.
kwa estimation, kupata exact number katika uhalisia wake kama walivosema wengine si rahisi sana. hili litajuliana kwa kuitisha vikao katika matawi yote na kuona hasa wanachama kwa maana ya uactive wao na sio tu wanaofika katika mikutano ya hadhara. pia tusitafute idadi kwa mising ya kadi zilizotolewa
 
Kimsingi idadi ya wanachama wa CDM haijulikani au ni siri.
Jipange upya mkuu, hata kama ulikuwa na nia njema na kutaka tujadili kitu fulani faida za kuwa na mtaji wa Wanachama lakini hapa umekurupuka, na thread yote imekuwa useless.

Swali la idadi ya Wanachama wa Chadema unaweza kujibiwa na uongozi wa Chadema tu na siyo JF.
 
Cha msingi ninachokiona ni kwa CDM kuendelea na kampeni yake ya M4C baada ya tishio la pale Nyololo. Kazi iliyo mbele bado ni kubwa. Wanaopiga kura ni mashabiki na ndio wanaokipa chama ushindi na si lazima wawe wanachama wenye kadi. Ushawishi (influence) ni wa muhimu sana. Ushawishi wa M4C ulikuwa unatisha na ndo ikabidi usimamishwe na watawala kwa gharama yoyote. CHADEMA inukeni tena!
 
Reactions: Ame
Wanachama wa Chadema hawaeleweki inategemea na maandamano na mikutano ndio utawaona baada ya mikutano na maandamano wanapotea...kimsingi hawajajiandikisha kupiga kura mfano daraja mbili ngome ya Chadema lakini watu 10,000 wamegoma kupiga kura.
I see!!.... The end of ur brain thinking Capacity, Jk kutoka kura miliion 8 plus mwaka 2005 mpaka kura milllioni 6 mwaka 2010 hapa ni kwamba wanaCCM wamegoma!! na wale wapiga kura karibu millioni 10 ni Chadema? who is the winner uchaguzi wa daraja mbili? kakojowe ukalale kesho shule huna point ya kuchangia hapa.
 

CDM haijawahi onyesha ni chama cha vurugu japo CCM imejitahidi sana kuipaka CDM kuwa hivyo mwisho wa siku CCM inaonekana ni hatari zaidi kuliko CDM na hiki kinajionyesha wazi hasa kwa matukio ya hivi karibuni ya nguvu nyingi iliyotumika dhidi ya demokrasia....Kama nawe unafanya spinning ili ku amplify hii dhana pengine nitakuelewa otherwise mtu yeyote hata awe mtoto hawezi amini ni vipi CDM wafanyiwe hayo yote na bado wakae kimya then uwaite eti ni chama chenye vurugu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…