CHADEMA Kidedea kwa Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye na Waziri Mary Nagu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Kidedea kwa Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye na Waziri Mary Nagu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambugani, Oct 3, 2011.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Chadema washinda kwa Sumaye, Nagu


  Bendera ya Chama cha Maendeleo (Chadema)
  Waandishi Wetu
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda kiti cha udiwani katika Kata ya Endasak, ambako ni nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu ambaye pia ndiye Mbunge wa Jimbo la Hanang ilipo kata hiyo.

  Ushindi huo wa Chadema sasa unakifanya chama hicho, kuwa na idadi sawa ya madiwani na CCM katika Halmashauri ya Hanang kwa kufikisha madiwani 12. Pia kila chama kina mbunge mmoja, Nagu na Rose Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema).

  Kwa mujibu wa matokeo kutoka vituo 13 vya kura, mgombea wa Chadema, Hashim Muna alipata kura 1,244 wakati mgombea wa CCM, Lazaro Shauri alipata kura 1,183. Kura 62 ziliharibika.

  Awali, Muna alikuwa Diwani wa CCM wa Kata hiyo, lakini alijiuzuru na kujiunga na Chadema baada ya jina lake kuenguliwa na chama hicho tawala alipokuwa akigombea nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri ya Hanang.

  Baada ya matokeo hayo, kuwekwa kwenye mbao za matangazo, wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Mkurugenzi wake wa Uchaguzi, Jimbo la Hanang, Mustapha Akoonay ambaye pia ni Mbunge wa Mbulu waliibuka na shangwe.

  Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Endasaki, Herman Jerojika alitangaza matokeo hayo saa 1:43 usiku baada ya kuyapokea katika vituo 13 kuwa mgombea wa Chadema ameshinda kwa tofauti ya kura 62 na wapiga kura walikuwa 2,489.

  Katika uchaguzi mwingine wa udiwani, mgombea wa CCM Kata ya Engutoto, wilayani Monduli, Gideon Kimongishu ameibuka mshindi kwa kura 1,020 dhidi ya mgombea wa Chadema, Gilbert Mganga aliyepata kura 207. Waliojiandikisha walikuwa 3,569.

  Uchaguzi huo ulifanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Magdaline Shoo kufariki dunia Aprili, mwaka huu.

  Huko Serengeti, Mara, Ryoba Marwa wa Chadema ameshinda udiwani wa Kata ya Stendi Kuu kwa kupata kura 650 wakati Tugoro Mboto wa CCM amepata kura 270 na Joseph Rhobi CUF 35. Msimamizi wa uchaguzi, Bhoke Ruhinda alisema kura zilizopigwa ni 964 , kura halali 955.

  Manispa ya Shinyanga: Mshindi wa udiwani Kata ya Masekelo ni Zacharia Mfuko wa Chadema ambaye amembwaga mwenzake wa CCM, Rashida Mahenga. Akitangaza matokeo hayo, Mtendaji wa Kata ya Masekelo, Steven Masabo, alisema Mfuko alipata kura 1,080 dhidi ya 603 za mgombea wa CCM.

  Habari hii imeandikwa na Mussa Juma, Hanang, Suzy Butondo, Shinyanga, Anthony Mayunga, Serengeti na Peter Saramba, Monduli.

  Source: MWANANCHI
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Indicator nzuri sana katika mageuzi.
   
 3. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri CHADEMA hivi kule Serengeti ndiko Nape alisema mkutano wake ulifunika wa Mbowe? sijui yuko wapi ajitetee jana kajiajiri NEC ghafla na kutangaza matokeo,Kijana kaivamia siasa kichwa kichwa,soon atabaki Historia
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  chadema hoyeee vueni magamba yote tupeni mtaroni huko!
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hongereni CHADEMA kwa ushindi huu!! Itabidi kuanza kujipanga vyema katika uchaguzi wa serikali za mitaa!! Awareness to people should be the first thing on this!!
   
 6. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Matokeo haya ni kati ya matokeo mazuri sana kuwahi kupatikana kwa chadema. Inavyoonekana chama kina nguvu sana kuliko mwanachama mmoja mmoja. Na hii ni dalili njema.
   
 7. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa jimbo la igunga raia wameonyesha siasa za udini azipo upande wao ila serikali na bakwata ndio wanaozipandkiza.viva cdm mmekubalika na 2014 tuanze na serkal za mitaa.
   
Loading...