:drum:Tanzania kuna vijana wa aina mbili. Kuna wale vijana wa system ambao wazazi au ndugu zao wapo kwenye system na wale walio nje ya SYSTEM. Walio kwenye system ni kama akina January marope, hussein Mwinyi, Nape na wengine. Vijana hawa hakika wanataka system ya CCM iendelee ili wawaandalie jamii zao nafasi. Vijana wengine ni wale ambao wanategemea misuli zaidi wapo bright ila hawapati nafasi.
CCM ikiendelea kukaa madarakani, vijana wasio wa system wataendelea kutengwa. Ila CCM ikianguka na Chadema wakiingia vijana walio nje watapata nafasi kwa kutegemea competence zao. Kwanini? Wataingia watu wapya tena wachache ambao hawana historia hivyo hata wakipendelea hawawezi kuchukua nafasi nyingi.
Nilikuwa nazungumza na kijana alisomea diplomasia ila hana kazi. Akaniambia kuwa ukienda balozi za nje wamejaa vijana wa wakubwa pamoja na kwamba hawajasomea diplomasia. Chadema ikishinda itawarudisha wote na kupeleka waliosomea hivyo kuivunja kabisa system iliyopo. Kijana ambaye si wa system anaye support CCM hafikirii vizuri. Huwa mtu ambaye hana kitu yakitokea mabadiliko yana nafasi kubwa zaidi ya kumnufaisha kuliko yule ambaye ana kitu. After all, wewe kijana wa mkulima huna cha kupoteza yakitokea mabadiliko ila kuna nafasi ya ku gain. Vijana tuungane tubadilishe system, tuivuruge tuijenge upya. Mwisho kwa vile sisi vijana ndio tutakuwa tumeiweka chadema madarakani, watatuheshimu, watatusikiliza maana wanajua tutawaondoa wasipofikisha malengo. Ndio maana SA ANC inawaheshimu sana wafanyakazi maana wanajua wao ni muhimu sana kwa ANC kubakia madarakani. :drum: