Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Kipindi cha utawala wa Rais Kikwete,CADEMA walisema yafuatayo kuhusu ziara za nje ya nchi; Safari za Rais zimeifilisi nchi. Rais anaenda nchi za nje kutalii, Rais anapaswa kubaki nchini ashughulikie kero za wananchi badala ya kusafiri, Ziara za Rais Kikwete ni za kuombaomba hazina mkakati wowote nk.
Katika kipindi hiki cha utawala wa Rais Magufuli vinywa vya CHADEMA vinanena haya: Rais Magufuli ni mshamba hataki kujichanganya na Marais wenzie. Rais Magufuli asafiri nje ya nchi majukumu ya ndani awaachie wasaidizi wake. Kutosafiri nje ya nchi kunaikosesha nchi misaada. Rais Magufuli aende nje kujifunza kutoka mataifa mengine nk.
Kabla ya kuhitimisha niwakumbushe kuwa pamoja na Kenyatta kwenda China kwa mbwembwe lakini hao China wamemnyima mkopo ujenzi wa reli.
Kuna mengi mnaweza kuongezea kwenye hoja hii nawatakia siku njema.