CHADEMA jipangeni upya Watanzania wamechoshwa na siasa za kibabe na vurugu

kwa iyo mimi na wenzangu hapa ni WANYARWANDA.

Tatizo la CCM ni shule! Hata reasoning capacity ndogo hawana! wewe tafakari - CCM ili kuwa inatetea viti 28 and CDM viti 2 tu lakini katika uchaguzi CDM ikapata viti 5 and CCM kupoteza 6 na kupata 22 tu. sasa katika ya CDM and CCM nani alipoteza?????? CCM tatizo hawana shule na ndiyo maana wanamwona hata Lowasa anafaa kwa vile ana ka-dree kamoja nako kakupepea! Ni nani CCM anayetaka kugombea urais mwenye shule? Tafakari
 
Barubaru,
Hawa jamaa zetu tunawafahamisha lakini hawataki kukubali mwaka 2015 panapo uzima sio mbali. Majibu watayapata kwenye box la kura.


Shukran kwani siku zote kwenye ukweli uongo unajitenga na njia ya mwongo ni fupi kwani sasa ukweli umedhihiri.

Kumbuka kuwa wakti CCM wanaanza mkutano wao huko Dodoma walitengeneza vijikaratasi vya kumpinga Kikwete na kueneza propaganda kibao ili asipate kura za kutosha kuwa Mwenyekiti. Lakin ukweli umedhihiri amepata kura zote za NDIO na Mbili tu za hapana katika kura zaidi ya 2900.

Ni vizuri muzidi kuwaombea tu siku moja nao waone UKWELI na sio Propaganda chafu ili kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi. Ikumbukwe kuwa Nchi haiongozi kwa Kusema Uwongo au siasa chafu za maji taka.

Wamekuwa watu wa kuomba mabaya tu.

 
Shukran kwani siku zote kwenye ukweli uongo unajitenga na njia ya mwongo ni fupi kwani sasa ukweli umedhihiri.

Kumbuka kuwa wakti CCM wanaanza mkutano wao huko Dodoma walitengeneza vijikaratasi vya kumpinga Kikwete na kueneza propaganda kibao ili asipate kura za kutosha kuwa Mwenyekiti. Lakin ukweli umedhihiri amepata kura zote za NDIO na Mbili tu za hapana katika kura zaidi ya 2900.

Ni vizuri muzidi kuwaombea tu siku moja nao waone UKWELI na sio Propaganda chafu ili kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi. Ikumbukwe kuwa Nchi haiongozi kwa Kusema Uwongo au siasa chafu za maji taka.

Wamekuwa watu wa kuomba mabaya tu.


Tatizo hawataki kujifunza siku zote wao wanajiona wabora na wana mamlaka ya kuwasemea watanzania wakati si kweli.

Jana mwenyekiti wao Mbowe anamuamlisha rais Kikwete aivunje Takukuru imeshindwa kudhibiti rushwa ndani ya chaguzi za CCM.

Cha kushangaza Mbowe mwenyewe alikuwa kimya wakati rushwa za wazi kwenye uchaguzi wa Bavicha Taifa, pamoja na wengine kukamatwa lakini alikuwa kimya.
 
Nyumba NDOG a.k.a KIDUMU mara zote huwa hamna maamuzi mugumu ni propaganda tu.vaa GAMBA lako vizuri ukifa japo lilete jembe ufukiwe.
 
mtoa maada huna thamani kwa watanzania wazalendo kakae na mafisadi mtafute exile kwani dawa yenu inachemka
 
wewe nae ni magamba tu, siasa za fujo anafanya nani kama sio ccm na jeshi lake, unapokandamiza haki ya mtu unategemea nn? Mikutano halali inpingwa kwa maslahi ya ccm jeshi la polisi badala ya kulinda amani linaua watu waliopo katika shughli za chama. Sikubaliani na wewe kwa kauli zako.
 
Hawa vijana waleo hawayajui hayo. Waambie watetezi wa Nyerere waje kusema vilikuwa vyanini vile, nakuhakikishia hawawezi.
Nakwambia tuliogopa hata kuvigusa. Hata sikusoma kilichoandikwa. Vilikusanywa harakaharaka na mwalimu kisha kuna watu walikuja kuvichukua wakaondoka navyo. Baada ya hapo hakuna hata aliyezungumzia vipeperushi hivyo, Infact nilishasahau kabisa habari ile, nimekumbushwa na hii thread.
 
Ritza kweli Fikra zako na umri na mwili wako ni wazi huo ubongo wako, ni kama engine ya beetle kufungwa bulldozer.

Jana tuu Kikwete alikuwa akisema chama chao ni Dume.
 
Wanabodi.

Ukianza kwa kuangalia matokeo ya udiwani jinsi walivyopata ushindi inakatisha tamaa kwa Chadema kama chama cha siasa, pamoja na mikutano mingi ya M4C, na kupambwa sana na TV na Radio hatimaye wakapata viti vitano ambavyo wao wanaona ni ushindi mkubwa wa kujivunia. Kwa mtu makini akitafakari kushindwa vibaya huko kwa Chadema atabaini jambo jingine la pili katika mioyo na akili za Watanzania....
Ritz wa JF.

Ritz bila shaka una taharuki ya M4C.

Bila shaka inakuuma wabunge wa CHADEMA wanapotoa hoja nzito bungeni kukosoa watendaji wa serikali, wakilenga kutetea maslahi ya wananchi.

Isingetosha tu kusema wana siasa za ubabe, zinazovunja sheria ya nchi, ungepaswa kutoa mifano hai ili katika kujibiwa uweze kujibiwa vizuri. Hata hivyo, mwenyekiti wa CCM amesaidia sana kutoa elimu ya uraia kwa wana CCM kama wewe. Shughuli ya M4C si uvunjaji wa sheria kama Tendwa alivyotaka kuwaaminisha. Ndivyo vyama vya siasa vinavyopaswa kufanya, na JK amewaomba CCM wafanye hivyo.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete amewataka wajumbe wapya wa NEC wa CCM kutokulala bali kuzunguka kila kona ya nchi kufanya mikutano ya hadhara,kuingiza wanachama wapya na kueneza sera za chama hicho.

Source: ITV/Chanel Ten.

Lakini pia JK amesema wazi kuwa CCM inabebwa na Polisi, na hivyo waanze kufanya siasa za kwenda kujieleza kwa watu na si kutegemea Polisi.

KITAIFA
Na Julius Magodi na Habel Chidawali, Dodoma

Posted Jumatano,Novemba14 2012 saa 21:33 PM

KWA UFUPI

"Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,"alisema Kikwete na kuongeza:


RAIS Jakaya Kikwete juzi aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliofanyika kwa siku tatu mfululizo katika Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kitendo cha wanaCCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la Polisi hakipaswi kukubaliwa kwani kimepitwa na wakati.

"Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,"alisema Kikwete na kuongeza:

"Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wakawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine."

Licha ya kwamba hakuwataja moja kwa moja, kauli za Rais Kikwete zilikuwa zikielekezwa kwa uogozi wa Chadema ambao kimsingi kinaonekana kuwaumiza vichwa CCM.

Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, "Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli."

Kikwete aliwatuhumu viongozi wa upinzani kwamba ni waongo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakizusha mambo ambayo hayapo, huku wakijifanya kuwa na ushahidi wa kimaandishi.

Alimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwamba kuna wakati aliwahi kuzusha kwamba yeye (Kikwete), na makada kadhaa wa chama hicho wakiwamo Rostam Aziz walikuwa jijini Mwanza usiku, wakati si kweli kwani siku waliyodai alikuwa Nachingwea mkoani Lindi kwenye mikutano ya kampeni za urais.

Katika mazingira hayo, aliwataka wanaCCM kila mahali kujibu hoja za wapinzani kwa kauli na vitendo na wasikubali kuburutwa kwani uongo ukiachwa kwa muda mrefu unageuka kuwa ni ukweli.

Aliwaeleza kuwa ukimya wao katika kujibu hoja za wapinzani ni sumu kwao na kwamba wenzao wameanza kuaminika zaidi yao licha ya kuwa CCM ndio wenye majibu yote.

"Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani," alisisitiza Kikwete.

Mbali na hilo aliwaonya kuacha malumbano ya mara kwa mara akieleza kuwa hali hiyo inakibomoa chama.

Alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakitumia muda mwingi kukosoana wao kwa wao, huku wakitoa nafasi kwa adui zao.

Mwenyekiti huyo alisema hakuna mtu kutoka nje ya chama anayeweza kukidhoofisha CCM kwa hoja isipokuwa chama hicho kinaumizwa na wanachama wake ambao wamekuwa wakilumbana bila sababu.

Akizungumzia suala la wagombea urais aliwataka wanachama wenye nia kufuata taratibu zote za chama pamoja na kuvumiliana ili ifikapo Mei 2015, mkutano utafanya uamuzi wa nani anasimama kupeperusha bendera ya chama hicho.

"Kwa wale mnaotaka kugombea, andikeni hiyo tarehe tutakuja hapa kuteua, lakini msituvuruge lazima mfuate utaratibu. Utaratibu huo utatangazwa, maana mkianza kupita huko na huko ndiko tunakopata matatizo," alisema Kikwete.

Kikwete juzi alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata asilimia 99.92 ya kura zilizopigwa, huku kura mbili zikimkataa. Kadhalika mkutano huo uliwachagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania – Zanzibar) na Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara).


Sasa hapa mkuu Ritz nani anayetumia ubabe? Anayetumia jukwaa, au anayetumia Polisi?
 
CCM ISHAKUFA. Buriani
<BR><BR>

Jaribu kupima haya maandishi yako kwa kina kama unadhani yako sahihi!!!!!!!!!!!sikuungi mkono hata kidogo kwa sababu CCM hii hii ndio inayoongoza serikali uliyonayo hivi sasa,unakula,unakunywa,unakojoa na kunya,na unapata hata muda wa Kuchat ndani ya JF,sasa kuniambia kwamba imeshakufa sikubaliani na wewe,ila nakubaliana na wewe kwamba CCM imeyumba,imetoka katika baadhi ya misingi yake hasa ile ya kuwatetea na kuwajali wanyonge,lakini si kweli kwamba imekufa.NONONONONONONONONONONONONONO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!<BR><BR>
 
Lazima upost kuponda chadema na upinzani ili jina lako liendelee kudumu kwenye payroll ya Nape, bila hivi vi thread mbuzi vyako utalipwaje??
 
Hii CD ya chadema ya ufisadi imeshaanza kupata scratch kwa sasa inakwamakwama. :becky::becky:
 
Katika lugha yetu ya asilia kule kijijini ukisema "CHADEMA" umaanisha kina "dema dema" yaani kinayumba yumba kwa maana nyingine kinapepesuka pepesuka! Sasa ukisimama jukwaani ukasema hiki chama chetu Chadema kichagueni :becky::becky::becky:
 
Back
Top Bottom