CHADEMA, Jipangeni na mpango huu wa serikali na vyombo vyake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Jipangeni na mpango huu wa serikali na vyombo vyake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki sawa, Mar 15, 2013.

 1. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mtakumbuka kuwa mnamo siku ya jumatatu tarehe 11.03.2013 Mwenyekiti Mbowe akiwa Musoma alitangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa maandamano makubwa ya kuisimamisha nchi kwa siku nzima yaani tarehe 25.03.2013 ambayo yatahusisha Majiji ya Dsm, Arusha, Mbeya na Mwanza , ambayo yatakuwa na lengo lla kumshinikiza waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa na Naibu wake wajiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao walifeli zaidi ya asilimia 95.

  Aidha baada ya tahere hiyo kutangazwa na kutokana na umuhimu wa siku hiyo kwa taifa kuwa ni siku ambayo Rais wa China atakuja nchini mwetu ikiwa ni ziara yake ya pili tangu aapishwe kwenda nje ya nchi na ni ziara ambayoatakuja kusaini mikataba kumi na moja , pia anategemewa kutoa hotuba kwa ulimwengu kuhusu mwelekeo wa sera za China kwa Afrika siku hiyo na hotuba hiyo itakuwa ikirushwa moja kwa moja na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni kama ,BBC, CCTV,CNN na Aljazeera NA vinginevyo , kikao kizito cha idara kilichofanyika siku ya jumanne kiliazimia kuwa video ya Lwakatare iwekwe kwenye mtandao kwa lengo la kuhamisha mjadala na maandalizi ya Maandamano ya CDM ili wanadiplomasia na mashushushu kutoka China ambao wapo nchini kwa ajili ya maandalizi kuwepo tangu tarehe 03.02.2013 ambao wapo wasione kuwa kuna tishio la maandamano , ili wasije wakaahirisha ziara ya rais huyo ambayoni ya umuhimu mkubwa kwa china na msimamo wake kuhusu Afrika .

  Mkakati huo ulipangwa licha ya kuwa utengenezaji wa video hiyo ulikuwepo na kujulikana tangu mweziJanuary 2013 na Denis MSacky alifungua jalada polisi kuhusiana na mkanda huo na pia alipewa ulinzi na waziri wa mambo ya ndani , mpaka leo amepewa askari kanzu ambaye anafanya naye shughuli kama dereva wake tangu mwezi Januari , mliokuwa mnafahamu maisha yake kabla ya hapo mtakuwa mmejua jambo, na hata juzi wakiwa Beach Comber hoteli kwenye inhouse training hilo alilisema mbele ya waandishi wenzake na mabosi wao waliokuwepo.

  Chadema jipangeni kwani mkakatiwa idara ndio huo juu yenu,

  Kwa kuwa nimewaeleza nyie Chadema mambo haya ya ndani, na juzi niliwaeleza kuhusu maelekezo ya Zoka kwa Kova kuhusu Lwakatare na hamkuonekana kuchukua tahadhari mapema , ni vyema mkajua maandamano mliyokuwa mmetangaza yalijadiliwa sana na kama mkijipanga Kawambwz na Mulugo wanaondoka ili kunusura Taifa na aibu iliyoko mbele , hasa ukizingatia mikataba itakayotiwa saini ipo tayari........wenye kumbukumbu kumbukeni tuhuma zilizozagaa za mtoto wa Kigogo kukamatwa China........
   
 2. UNDENIABLE

  UNDENIABLE JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 26, 2013
  Messages: 2,312
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Tupo sawa mkuu, usihofu kitu, tuko kamili gado!!!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,285
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haki sawa:high5::yo::yo::yo::yo:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,015
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Huyu Dennis Msacky ndiye nani?
   
 5. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,832
  Likes Received: 1,577
  Trophy Points: 280
  ....si hiyo tu...hata hii ya juzi ya waziri wa ulinzi kuwaadhibu polisi waliobambika kesi watu imefanyika strategically......inajulikana sana polisi wanabambika watu kesi tz...lakini imekuja juzi tu kwa waizri kuwatangazia Watanzania adhabu hii kwa polisi kipindi hiki...ambapo kuna kelele nyingi za watu kudhuriwa na vyombo vya dola.....Mbaya zaidi ni paradox iliyopo sasa kwa hivi vyombo vya ulinzi tz....kwamba wanajifanya wanashughulikia matatizo...wakati huo huo wanaongeza matatizo....Unawaadhibu polisi kubambika kesi...wakati huo huo hao hao polisi wanabambika wengine kesi(refer the Lwakatare saga (though unconfirmed)).......​Inauma...
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Kuna kipindi alikuwa mwandishi wa Gazeti la mwananchi,sijajua kwa sasa yupo wapi!!!
   
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,015
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
 8. Magwangala

  Magwangala JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 2,011
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Ni mhariri mtendaji wa Mwananchi
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,470
  Likes Received: 3,364
  Trophy Points: 280
  Hata mie nilipata mashaka na eti police wameanza kujisafisha,kuna kitu hapo ..kwanini wasianze na Iringa,Arusha na Moro?
   
 10. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Haya ni maneno ya Membe, kama yeye hana genge, hana kundi hilo na hana fedha , ni nani mwenye genge na fedha za kuwatesa watu hapa Tanzania ? Anaonekana kumfahamu mtu mwenye genge .......aitwe kusaidia Polisi , niliandika juzi kuhusu ziara yake Morocco na Zoka aseme walienda kupanga nini

  Kama hajagombana na Kibanda amegombana na nani na huyo waliyegombana naye ameshammaliza ama bado , tutarajiemtu mwingine kuumia kwa sababu ana ugomvi naye ?ina maana kila anayegombananaye huwa anaumizwa ...,,,,,,,,,,chambueni kauli hizi .......

  “Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo. Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye (Kibanda) na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi sina uhasama na Kibanda.”
   
 11. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna mkakati wa kumjenga Nchimbi kuwa anaweza kuchukua hatua ,,.......mkakati huu ni wa kumpanga kwani inavyoonekana ni kuwa Lowassa amejengwa kuwa ndio kiongozi pekee ndani ya CCM ambaye anauwezo wa kuchukua hatua .......hapa anajengewa taswira ....ila wapo waliofungua kesi na watamshinda hizo kesi mahakamani ......ataumbuka ......time tuu........
   
 12. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mahariri mtendaji wa gazeti la mwananchi ..ambaye inasemekana kuwa yeye ndio alikuwa adhuriwe kulingana na hiyo video iliyowekwa baada ya kutengenezwa ..........mambo ni makubwa kuliko mnavyoweza kufikiria .......
   
 13. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,296
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ndipo utapojua watanzania wenye kupenda nchi yao ,hakuna kubakisha kitu ,ndipo watajiju maandamano pale pale kulinusuru taifa
   
 14. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,296
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ni mhariri mtendaji wa mwananchi rafiki yake sana Zitto Kabwe aliyeaapa kumlinda maisha yake sasa muangalie trend hiyo connect na masalia nchi hii bwana tunazunguka pale pale
   
 15. s

  schlumberger JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2013
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 642
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  DR. SLAA. Ndugu Waandishi,CHADEMA haiko tayari kuruhusu watu wenye maslahi binafsi kutuchafua mbele ya jamii. Katika hilo, tutapambana na yoyote bila kujali cheo chake, madaraka yake serikalini, fedha alizonazo au madaraka mengine.

  MY STANCE:
  KAMA HUNA VYOMBO VYA DOLA, JESHI, MAHAKAMA, POLISI, MAGEREZA N.K UNAPAMBANA KWA NJIA GANI KAMA SI KUNYAMAZISHA WATU KWA KUWATESA NA KUWAUA??

  KWA KAULI HIYO YA DR. SLAA HIVI WATANZANIA HATUONI KAMA DR. SLAA YUPO NYUMA YA LWAKATARE?? KWA NINI VYOMBO VYA DOLA HAVIMKAMATI KWA KUANDAA MAUAJI???

  NAAMINI ILE VIDEO CLIP YA LWAKATARE NI YA KWELI. NDIO MAANA WAKATI ANAPANGA MIKAKATI MACHOZI YANAMTOKA. KAPEWA MAAGIZO AMBAYO LAZIMA AYATEKELEZE LAKINI NAFSI INAMSUTA KWA KUHUJUMU HAKI YA MTU.
   
 16. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,296
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Inaelekea Membe ndio Usalama wa taifa maassasin ni wa kumwogopa kama ukoma mtu bila aibu aende kwenye public television na kuapiza atakapo kuwa Raisi wabaya wake 11 watamkoma au atawamaliza halafu mtu kama huyo anaendelea kukalia ofisi nyeti kama anayoongoza,
  ndugu zangu watanzania tusiposimamisha hiki kikundi cha mamafia waliojimilikisha pande la ardhi la Tanzania na watu wake wote wakiwafanya watakavyo basi tujue tumekwisha moja kwa moja
  gendge hili linapaswa kutokomezwa kabla kiza cha masaibu kwenye nchi yetu kuendelea kuingia
   
 17. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,296
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jibu ni kwamba silaha kubwa ya kutumia ni kupeleka kesi kwenye mahakama za umma basi na wao ndio waamuzi wawafanye nini viongozi wa serikali mumiani wa haki za watu ,dhuluma ya mali za wananchi na wakiukaji wa haki za wananchi na huku wakifanya kila waliwezalo kuziba sauti za wanyonge
   
 18. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,015
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Motive ya kumdhuru ni nini? Nani ambaye atafaidika katika kudhuriwa kwake? Na kwa vipi? Hayo ni maswali ya msingi ya kujiuliza!
   
 19. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,225
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na vipi mh. Membe?
   
 20. M

  Magesi JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2013
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi Ile Picha Ya Zitto Kwenye Mwananchi Inamaanisha nini
   
Loading...