CHADEMA, jino kwa jino haiwezi kuwa Haramu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,900
Kulitolewa wito kuwataka vyama kufanya siasa za kistaarabu.

Kama vile wametumwa yamezuka magenge ya chawa yenye rabsha na uzushi wa kila aina mitandaoni, kupalilia fitna zozote ndani ya vyama vingine.

Kwamba wenye chawa hawakemei hali hizi yawezekana ndiyo sera zao.

Torati ya Mussa inafundisha "jicho kwa jicho."

Walileta na wanaleta mapandikizi vyamani wakiwemo vipenyo. Hii haiwezi kuwa haki yao peke yao kutoka kwa mola.

Ushauri wa kunyooka nao hauwezi kuwa kwao dhidi ya wengine tu.

Upotoshaji, uchochezi na kupika migogoro haiwezi kuwa wao kwa wengine tu.

Espionage, destabilization nk haiwezi kuwa wao dhidi wengine tu.

"Eye for an eye" kama ibada haijaacha kuleta adabu.

-----------
https://www.jamiiforums.com/threads/chawa-wapandisha-site-fake-kwa-niaba-ya-chadema.2060655/

https://www.jamiiforums.com/threads/mgogoro-wa-lissu-na-mbowe-mzee-edwin-mtei-aingilia-kati.2062234/
 
Jino kwa jino au jicho kwa jicho zije pale ambapo itathibitika mbinu nyingine zote zimefeli.

Tumeona maridhiano yakirudisha mikutano ya siasa, tumewaona viongozi wakuu wa yale maridhiano wakionesha dhamira ya kuileta Katiba Mpya, wapewe muda.
 
Kunyooka nao, kuwekeana vipenyo, espionage, destabilization, upotoshaji nk hakuwezi na hati miliki yao peke yao.

Kama hayo ni halali kwao hayawezi kuwa haramu kwa wengine.

"Eye for an eye."

Kwa hakika ingewafanya Kila mtu akawadhibiti chawa wake.
 
Naona chawa umekuja kuhamasisha fujo na kuchochea ukosefu wa amani kwa faida ya aliekutuma.

Mwisho wa siku aliekutuma atakutelekeza kama vile mtu anaetelekeza condom baada ya kumwaga kojo. Achana na siasa za chuki, hazitakusaidia kitu zaidi ya kumfaidisha tu aliekutuma na genge lake.

Migogoro ndani ya vyama vyenu ipo na haiepukiki kwa sababu ya uchu wa madaraka na kugombania kujaza matumbo. Afrika nzima hakuna mwanasiasa au chama cha siasa chenye lengo la kumkomboa masikini.

Kila chama cha siasa au mwanasiasa anajipambania mwenyewe na familia yake, akiwa na huruma kidogo basi atawapambania na ndugu zake. Kwa aina hii ya wanasiasa hawa unafikiri migogoro itaisha vyamani hasa kundi moja linapohisi kuwa kundi lingine linafaidi memo ya chama?

Pesa ni mbaya na huwa haimuachi mtu salama.

Kama ndugu wa baba mmoja na mama mmoja huwa wanagombana na sometimes hadi kuuwana kwa kila mmoja akipigania usimamizi au uongozi wa kampuni alioacha baba yao, vipi kwa watu waliokutana tu vyamani, tena katika kipindi ambacho mmoja inasekana amelamba asali na kusahau wengine?

Kwenye moto lazima kufuke moshi na kwenye moshi lazima kutafuka moto.
 
Chawa wako kwenu tu. Kwingine uchawa ni machukizo!

Wapi unasoma hamasa ya fujo? Au nyie mnadhani kufanya fujo ni haki yenu?

Kwa nini mnaona kujibiwa fujo kwa fujo ni tatizo? Kwanini msichague kutokuwa waanzilishi wa fujo Ili msijibiwe kwa fujo?

Mnataka kunyooka na wengine ila mwingine asinyooke nanyi kama mlivyoitishwa?

Kwani mmiliki wenu aliwaambiaje? Mmekwisha sahau?

Kwanini msiyoyataka mngependa kuwatendea wengine?

Bure kabisa.
 
Hebu twende taratibu na haya mambo, hivi kiuhalisia, jino kwa jino itawezekana vipi kati ya wale wenye polisi na virungu, na wengine wasio na chochote?

Ieleweke vizuri, sitetei ukondoo hapa, lakini pia, kulazimisha matumizi ya nguvu usiyokuwa na uwezo nayo sioni kama ni maamuzi timamu.
 
Post #7 inajieleza vyema.

Kuweka mapandikizi kwao kama tunavyowekewa sisi inahitaji matumizi ya nguvu?

Kuweka vipenyo kama tunavyowekewa sisi, inahusika vipi na virungu na polisi?

Kunyooka nao kama alivyowashauri wao Tulia kunatuletea vipi virungu sisi kama haviwapelekei wao virungu?

Kujipanga kuwafanyia wao wanayopanga kutufanyia sisi, haiwezi kuwa ni kuitisha fujo labda kama una maana wanayo nia ya kutufanyia fujo.

Kujibu sawia na tunavyofanyiwa, huko ndiko kwenda "jino kwa jino" Kwa maana yake halisi na si vinginevyo.

Zingatia Raila alijiunga KANU kama mamluki. Ubaya gani Mbowe au Lissu au Mimi au wewe kujiunga kwao kama mamluki?

Kwani wale vipenyo walikuwa Chadema kama nani?
 
Chawa wako kwenu tu. Kwingine uchawa ni machukizo!

Wapi unasoma hamasa ya fujo? Au nyie mnadhani kufanya fujo ni haki yenu?

Kwa nini mnaona kujibiwa fujo kwa fujo ni tatizo? Kwanini msichague kutokuwa waanzilishi wa fujo Ili msijibiwe kwa fujo?

Mnataka kunyooka na wengine ila mwingine asinyooke nanyi kama mlivyoitishwa?

Kwani mmiliki wenu aliwaambiaje? Mmekwisha sahau?

Kwanini msiyoyataka mngependa kuwatendea wengine?

Bure kabisa.
Toka raisi aliporuhusu mikutano ya vyama vya upinzani, ni wapinzani gani ambao wameshafanyiwa fujo aidha kwa kupigwa na polisi au wana CCM.
Ninachokiona hapa ni wewe kujaribu kuficha migogoro ambayo iko ndani ya vyama vyenu. Kwa kuihusisha CCM au serikali na migogoro yenu mlioanzisha wenyewe kutokana na tamaa ya madarakana pamoja na kutofautiana misimamo ambapo kiongozi mkubwa wa juu ana siasa za kistaraab huku makamu wake akitaka waendelee na siasa za fujo akifikiri kuwa ndio zitamsaidia na yeye kuitwa ikulu akalambe asali kama mwenzake.
 
Zingatia siasa zenu za maji taka haziwezi kuwa halali dhidi yetu tu, ila haramu dhidi yenu:

Screenshot_20230203-140057.jpg

Huo ni mfano mmoja tu yako mengi.

Wala usiende mbali mnayoyafanya tunayaweza. Na huo ndiyo ulio msingi wa jino Kwa jino.

Kulikoni kuchachawa hivi ndugu chawa? Kwani mna mpango gani mwingine zaidi karibuni?
 
Back
Top Bottom