CHADEMA jifanyieni tathmini

Leo hii wanaituhumu na kuitukana selikali kwamba inahusika.,lkn utashangaa siku Lisu akipona wanaomba ulinzi toka selikalini.

......
Serikali haiendeshwi na hela za CCM mkuu.....Kodi ni Watanzania wote wanachanga,usifikiri ni hela za ccm
 
Kazi ya polisi ni KULINDA KILA RAIA bila kujali itikadi yake.

Polisi hawatakiwi kuwa na chama, ila hapa kwetu wana vyama.

Ni sawa na referee. Hatakiwi kuwa na timu, japo nao wana timu zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa hiyo ulitaka polisi wawemo kwenye gari la lissu wakimlinda? hebu elewa kinachosemwa na mleta maada.

Ngw'ana Kabula
 
hawa hawakupewa jukumu la kumlinda mh. lissu, kazi yao nini sasa?
si wangekabiliana na moto wa kalashinikov ama wenyewe ni special force.




Ngw'ana Kabula
 
Shame on you too kwa sababu hata Rais Kennedy wa Marekani au PM Yitzak Rabin wa Israeli waliuawa licha ya kuwa na ulinzi wa hali ya juu. Ulinzi kwa kiongozi ni deterrence tu, lakini sio absolutely 100% foolproof against assassination

Unapoilaumu Chadema kwa kutompatia ulinzi Lissu unaonyesha kuwa huna uelewa japo kidogo kuhusu ulinzi wa viongozi nchini Tanzania. Kuna tofauti kubwa kati ya mlinzi wa Diamond na specialist wa personal protection. Why don't you blame the government ambayo ndo pekee inayoweza kumpatia Lissu ulinzi stahili (na sio wa kufikirika unaoongelea hapa)? Next time, jielimishe kwanza kabla ya kukurupuka kulaumu.

Halafu hata kama taratibu zingekuwa rahisi, je ungechangia gharama za ulinzi wa masaa 24 ya kiongozi huyo?



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kweli ujamaa umelemaza watu wengi mno na athari zake zitachukua muda mrefu sana kupotea.

Yaani kabisa wewe unaamini kuwa serikali ndiyo pekee inayoweza kumpa Lissu ulinzi stahilifu?

Duh!

Haya bana. Wewe na wenzako endeleeni kuitegemea serikali basi.
 
Kumbe Polisi ni mali ya CCM! Au mimi ndio sijakuelewa unapowataka chadema wasiitegemee Serikali ya CCM kwa Ulinzi?
 

Hili chini ni bandiko lako kipindi kile ungosha haujakuathiri:

Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?
Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini kuna mengine yenye ukakasi sana hadi kunifanya nianze kuhoji hekima na busara za huyo bwana!

---
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa rais wetu huyu, mheshimiwa mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli si kiongozi mzuri hata kidogo, hususan katika ngazi ya urais.

Hilo nimekuwa nikilisema kwa muda mrefu sasa. Nakumbuka hata ile siku alipoteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM nilisema hivyo humu humu JF.

Kwa kiasi fulani namkubali kwenye usimamizi lakini si kwenye uongozi. Hana kabisa haiba ya kiuongozi. Pia hana sifa za kuweza kuwa kiongozi mzuri.

Ni mtu mwenye jazba. Ana jeuri. Mwenye kuongea bila kufikiria athari za maneno yake[nyakati zingine]. Wengine wanasema eti kuwa hashauriki. Kwa ufupi ni mengi sana yanasemwa juu yake kiasi kwamba mengine ni vigumu kwa watu wa mbali kama sisi kujua kama ni ya kweli au la. Hivyo kwa sisi wa mbali tunaenda na yale tuyaonayo na tuyasikiayo toka kwake yeye mwenyewe.

Sasa kwa jinsi vile mambo yanavyoenda sasa hivi kuna kila dalili huenda nchi imeshamshinda kuiongoza. Hivyo ndivyo niuonavyo mwelekeo.

Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.

Naamini asipojiangalia na kujifanyia tathmini basi hiyo kazi itamshinda kabla hata hajafikia nusu ya muhula wa hii miaka mitano.

Niliwahi kuandika kuhusu 'a police state'. Jikumbushe....
 
Chadema azimeni hata walinzi kwa rafiki yenu Gwajima..

JPM hadi 2025, hutaki hama nchi.
!
 

Hakuna nilichobadilika.

Msimamo wangu upo palepale.

Tatizo ni nyie. Ni nyie mnaodhani na kuchukulia mambo katika rangi mbili tu.

Hamuwezi ku process nuance.

Ushabiki wenu umeghubika kabisa hata hizo akili zenu chache mlonazo.

Hizo akili zenu zinawatuma muamini kuwa huwezi kukubaliana na mtu kwa kiasi fulani na ukatofautiana naye kwa kiasi fulani.

Kwenu kama unatofautiana na mtu basi ni lazima iwe kwa asilimia 100 na kama unakubaliana naye basi ni lazima iwe kwa asilimia 100.

Baada ya hayo machache, nina mashaka sana hata kama umeelewa nilichokiandika.

Natanguliza pole zangu.....
 
Inawezekana sijaelewa lakini angalao mimi nafikiria nje ya ukabila! Wewe unachosupport ni ungosha lakini unajua kabisa jamaa nchi ilimshinda siku ya kwanza alipoingia ofisini!
 

Nyani, ni wazo langu tu. Kwa mtazamo wangu kwa hayo unayoyasema hapo juu yanalenga kuwa adui anatoka nje. Na kama ni kinyume cha hapo (Insiders)hatuna sababu ya kumpa ulinzi ili tupate simple target. Kwakuwa hatujui adui anatoka wapi kila linalofanywa na lisilofanywa lina sababu yake. Mwenye kuelewa ameelewa.
 
Inawezekana sijaelewa lakini angalao mimi nafikiria nje ya ukabila! Wewe unachosupport ni ungosha lakini unajua kabisa jamaa nchi ilimshinda siku ya kwanza alipoingia ofisini!

Wewe unasadiki tu. Hujui kitu.

Huna ushahidi wowote ule unaoonyesha kuwa mimi kwa yale mambo ninayomuunga mkono Magufuli nafanya hivyo kwa ukabila.

Ningekuwa nafanya kwa ukabila basi ningemuunga mkono kwa asilimia 100.

Ila siwezi kukulaumu maana uwezo wako wa uelewa ni mdogo..uko chini ya wastani!
 
Pp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…