CHADEMA Jibuni Hoja hii...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Jibuni Hoja hii...!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Jul 6, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Jana waziri wa Utumishi Management ya Umma Hawa Ghasia, jana kaituhumu Chadema mbele ya Bunge.
  Kadai bajeti yenu ni tril 9, kwa mujibu wa Waziri Ghasia, mkilipa
  mishahara ya wafanyakazi kima cha chini laki tatu kumi na tano(Tsh 315000) mtabakiwa na tril 1, Je serikali
  gani inaweza kuongozwa kwa tril `1??{Bajeti kivuli ya wizara ya utumishi wa umma ilisomwa na Suzan Lyimo}

  Na yy Waziri kasema wazi kwamba Chadema acheni kudanganya wafanyakazi(wananchi).

  Magazeti ya leo sijaona sehemu yoyote kuhusu Chadema kukanusha haya maelezo ya Waziri. Je ni kweli bajeti yenu
  iliongopa?? Mkiifumbia mamcho hii hoja bila majibu yenye mashiko tuwaeleweje Chadema??
  Naomba Dk Slaa, Mh Zitto Kabwe au kiongozi yoyote atoe jibu hapa.

  Angalizo: Hapa nisingependa majibu kwamba eti madini tunayo, sijui rasilimali, mara posho zitafutwa,hapana!! Majibu yaendane na hoja ya bajeti yenu mbadala mliyowasilisha bungeni na kutaka kima cha chini kiwe kiasi hicho mlichokitaja.
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Watu Makini huwa hawakurupuki, wanakokotoa na kupitia vielelezo vyao ili wakijibu wasitoe siasa bali watoe vitu venye ushahidi wa kutosha
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sijaelewa kitu hapo.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huyu hawa gasia ni kilaza kama bosi wake,hiyo bajeti ya mshahara ni ya ccm.
  walisema wanalipa t.3 wakasema kwa vile ukilipa laki tatu ni asilimia mia mbili ya laki na tano wanayolipa kwa hiyo wakazidisha hiyo laki 3*asilimia 200=9000000000.akili ya kimagamba.cdm walisema unaongeza kima cha chini tu. wao wakaongeza mpaka mtu anayelipwa milioni 3 akawa na milioni 9.akili ya kuambiwa changanya na zako.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Thread yenyewe makosa kibao.....hao kina Zitto wtajibuje?til ndio nini?

  Jana waziri wa Utumishi Management ya Umma Hawa Ghasia, jana kaituhumu Chadema mbele ya Bunge.
  Kadai bajeti yenu ni til 9(ingawa kama nakumbuka ilikuwa ni til 13), kwa mujibu wa Waziri Ghasia, mkilipa
  mishahara ya wafanyakazi kima cha chini laki tatu kumi na tano(Tsh 3,015,000) mtabakiwa na til 1, Je serikali
  gani inaweza kuongozwa kwa til `1??{Bajeti kizuli ya wizara ya utumishi wa umma ilisomwa na Suzan Lyimo}

  Na yy Waziri kasema wazi kwamba Chadema acheni kudanganya wafanyakazi(wananchi).

  Magazeti ya leo sijaona sehemu yoyote kuhusu Chadema kukanusha haya maelezo ya Waziri. Je ni kweli bajeti yenu
  iliongopa?? Mkiifumbia mamcho hii hoja bila majibu yenye mashiko tuwaeleweje Chadema??
  Naomba Dk Slaa, Mh Zitto Kabwe au kiongozi yoyote atoe jibu hapa.

  Angalizo: Hapa nisingependa majibu kwamba eti madini tunayo, sijui rasilimali, mara posho zitafutwa,hapana!! Majibu yaendane na hoja ya bajeti yenu mbadala mliyowasilisha bungeni na kutaka kima cha chini kiwe kiasi hicho mlichokitaja.
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  You are right! Majibu ya hoja za Chadema si za kukurupuka!
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Naunga hoja Mkuu!
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ndugu huwezi kumuomba mh.Zitto au hata dr akajibu mada za kukurupuka,mfano hapo juu umesema laki tatu kumi na tano elfu lakini tarakimu zinaonesha unamaanisha milioni tatu na kumi na tano elfu yan 3,015,000/= nani hakuelewe? Hata figure zenyewe si sahihi. Pia nakushauri uisake mwanahalisi iliyotolewa baada ya rais kutoa hotuba wakati akiongea na wazee wa dar baada ya mgomo wa walimu,alipotaja kuwa hata kwa mabomu na bunduki mtafanya kazi,walichanganua hesabu vizuri.
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ni kweli unayoyasema, lakini mbona naona kama kuna hoja ya msingi hapo??au hesabu zao wamekokotoaje??
  Kilichonisikitisha zaidi, Ghasia kawakebehi kwam kujigamba kwamba hata yy kasomea mambo ya uchumi na
  anawashangaa wachumi wa Chadema na kudai wamechukua namba na kuzipachika tu. Hiko kitu hakiwezekani.

  CAMARADERIE ahsante kwa kunirekebisha!! til means tillion!! Hapa wCDM waje na Majibu sahihi plz
   
 10. m

  mndeme JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ghasia kapiga siasa sana, kama utafikiria vizur baada ya kusoma bajeti ya upinzani na vyanzo vya mapato utagundua yeye ndo kapotosha umma. Yule mama ni kilaza sana, na hajibu hoja kwa hoja anajib kwa hisia.
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ghasia...mmhhh sijui walimtoa wapi yule mama
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mbona mtoa mada kasepa au salio limeisha..
   
 13. MsakaGamba

  MsakaGamba JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 392
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hebu wekeni sawa hapa wakuu. Na nyie msikurupuke lazima tutoe majibu makini kabla ya kina Zitto kujibu.
  Hivi ukiongeza kima cha chini tu ambacho kwa sasa ni 135,000/= hadi laki 315,000/= hugusi wengine unawaacha kwenye viwango vyao vya awali? Anae pata 315,000/= kwa sasa kikipanda atalipwa shilingi ngapi?

  Wekeni sawa hapa kabla hatuja mparamia Ghasia.
   
 14. Chaser

  Chaser Member

  #14
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majibu rahisi kwa swali gumu, umewashika pabaya mkuu, ha ha ha ha ha ha
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mkuu hiyo ni typing errors, nimesharekebisha!! Hoja imeeleweka!!

  Hapo(red) ndipo nisipopataka mimi...hesabu sawa walichanganua vizuri, tatizo ni kwamba bajeti kwa utumishi wa Umma ni Tillion 9 ( ukilipa wafanyakazi 315000 itabakia til 1, je hii ipoje??zile hesabu za kipindi kile na mchanganuo wake zilitolewa wakati bajeti haijapangwa!! Sasa bajeti tayari iko mezani fixed!! Wakokotoe hapo!!
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Bado tillion ni nini?......mimi najua trillion(kiingereza) na trilioni(kiswahili).....Sizinga tulia kwanza kabla ya kuandika

  ''THINK BEFORE YOU INK''
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mkuu nipo nafuatilia sredi...!! Nilifanya typing error, lakini nisha-update!!
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mkuu ile ndio bajeti mbadala kwa mwaka nzima wa fedha, sasa vyanzo vipi tena vya mapato unavyozungumzia??
  Hii t 9 ndio mpango nzima kujumuisha hiyo figure...!!
   
 19. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #19
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba huyu mama hajasoma uchumi. Kama anataka tumwage historia yake sawa, sio kazi kubwa. Na niseme tu hata Masters yake aliyofanya SUA, ilikuwa 'kazi nzuri' ya mama Salma (wakati huo akiwa mke wa waziri wa mambo ya nje) kutia maji ndipo akaachiwa.

  Pili niseme sio kweli wala sahihi kuwa mishahara kima cha chini ikiwa laki 3.15, fungu la mishahara ni Tsh 9 Trillions (Sio tillion ndugu Sizinga)...
   
 20. m

  mndeme JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa mwaka itakuwa ni trilioni 1.3 na haizidi trilioni 2 hata ukiwalipa laki 5 kwa mwezi kima cha chini. Hata hivyo CDM haiwez kuwa na mawazir 52 kama serikali ya JK, mashangingi yanapigwa bei, Posho zote zisizo na tija kwnye re-current bajet zinafutwa, hatukopi zaid ya deni la taifa lililopo na mishahara ikipanda mpaka hapo wengi zaid watalipa kodi ya PAYE pamoja na kuwa inapungua mpaka 19%. Sasa huyo mchumi ghasia anasema bajet mbadala ni manamba tu ana hoja ipi? Alipotosha, mwnye kuelewa atafanya hivyo.
   
Loading...