CHADEMA jengeni chama kote kote. Wakati unawajenga

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,752
Hivi sasa kinachoendelea ni kwamba hofu kubwa sana ya CCM Taifa ni uwepo wa CHADEMA kama chama cha siasa hususani kinachojijenga kuwa chama mbadala kwa malengo chanya ya Taifa.

Kabla sijaendelea nataka nikufahamishe mwanajamvi kuwa mimi ni mwanachama hai wa CCM. Nimelipia kadi yangu mpaka 2025 pia nashiriki vikao vyote halali vya chama kwa nafasi yangu. Nimeshawahi kuwa mwanakampeni wa Team JPM 2015 na mwanamkakati ngazi niliyopangiwa 2020. Naandika nikiwa najitambua.

Katika siasa za nchi hii, sijawahi kuona kipindi ambacho watawala wanaingia hofu kubwa dhidi ya chama kimoja cha siasa nchini. Neno UKAWA ndiyo Code inayotumika ndani ya CCM kumbrand mtu anayehisiwa ni mfuasi ama anayeunga mkono CHADEMA.

Hali tete inayoikabili CCM sasa inasababisha iwaite makada wake iliowatuma vyama vya upinzani warudi kuimarisha mikakati ya chama kuendelea kushinda kwa mbinu mbinu kutokana na hali tete ya kugeukana na kusababisha mpasuko wa ndani unaotishia maslahi yake ya kukwapua kura wakati wa uchaguzi. Bado makada wa CCM waliobakia ndani ya upinzani wamefikia mpaka nafasi za juu za uongozi kwenye vyama hivyo. Hivyo wengine ni watumishi waaminifu kwenye intelejensia ya CCM na inarahisisha sana kupatikana kww taarifa muhimu na mikakati inayosaidia Chama Cha Mapinduzi kushinda.

Inawezekana hii makala yangu fupi ikanigharimu lakini ni muhimu sana kusema ukweli baada ya kuona Watanzania wanashawishiwa kuamini taabu na matatizo yaliyozalishwa na viongozi wa CCM yanaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia Ilani inayoshindishwa kinguvu na dola.

USHAURI
CHADEMA kwa sasa kimeweza kujidhihirisha kama chama cha siasa kikichokomaa, hivyo kijipange kuongoza dola ili kuwaletea maendeleo Watanzania hususani maendeleo ya kweli. WanaCCM wanaenda kukikana chama chao kwenye uchaguzi mkuu ujao na hilo limewezeshwa na matukio yanayojiri sasa.

Chadema iimarishe timu zake za mikakati, iimarishe uhusiano wake na wananchi kuanzia mitandaoni, mijini na na vijijini. Chama kiandae viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa. Chama kijenge mfumo wa kusimamia viongozi wake wanaoiwakilisha kwenye dola tofauti na sasa ambapo viongozi wa kuchaguliwa kwenye dola wamekuwa na sauti kuliko viongozi wa ndani ya chama.

CHADEMA kijenge kuhamasisha maendeleo, mshikamano, ulinzi na usalama hata kama vyombo vya dola vinatumika dhidi yao. Chama kihubiri amani na upatanisho badala ya kujenga visasi na kuumizana.

CHADEMA kijipamabue kwenye siasa za kimataifa kama chama kinachoweza kushika dola.

CHADEMA kisiwekeze sana kwenye harakati bali uwezo wa kujenga jamii inayoendana na falsafa yake.

CHADEMA kisisitize utii wa sheria kwani hapo ndipo kimetegwa kwani watu wa dola wanavunja sheria makusudi ili kuwashughulikia CHADEMA.

CHADEMA kichukue hatua dhidi ya wanachama au viongozi wake wanaoonekana ni wasaliti na kukiumiza chama.

CCM ina hazina kubwa ya viongozi kwa sababu wameweka mfumo wa kuwasimamia viongozi hao na pia wakongwe ndani ya chama wanatumika vyema kuwajengea uwezo. Lakini asilimia 80 ya michakato yote ya uongozi ndani ya CCM imejaa rushwa, ukatili na visasi.

QUIZ KWA WANAHARAKATI
Ninatoa challenge kwa wanaharakati kama kweli ni makini, wafungue kesi ya kikatiba dhidi ya CCM kwa kutumia rushwa ya madaraka kwa tasnia ya ulinzi na usalama kutumikia siasa. Katiba imekataza na haitekelezwi. Mifano ipo wazi lakini maneno yanaishia mitandaoni pekee.

Tuishi kwa legacy.

JamiiForums-1685294223.jpg
 
Chadema ilikuwa ile ya Dr Slaa!

Hii iliyomfanya Gwajima kuwa mshenga wao wa kumleta EL chamani na baadae kumfanya Amsterdam kuwa ndio mwana mikakati ya kumpeleka Lisu ikulu ni takataka kabisa.
 
Chadema ilikuwa ile ya Dr Slaa!

Hii iliyomfanya Gwajima kuwa mshenga wao wa kumleta EL chamani na baadae kumfanya Amsterdam kuwa ndio mwana mikakati ya kumpeleka Lisu ikulu ni takataka kabisa.
Iwapo unakubali CHADEMA ilishawahi kuwa makini hapa juzi kati, basi hata sasa wanaweza kujipanga na kumakinika.

CCM ilikuwa makini sana hapo awali lakini kadiri siku zinavyoenda inazama kwenye shimo la makundi maovu ya kisiasa na dampo la viongozi wasio na uchungu na nchi zaidi ya matumbo yao.
 
Back
Top Bottom