February
Member
- Nov 15, 2011
- 90
- 21
Juzi rais JK amekula moto na upinzani hususan chadema kwamba wanataka kuyumbisha nchi katika mchakato wa katiba mpya. Kama umesoma katikati ya mistari kitu kilichomtisha sana jk ni hoja ya kuwa na mchakato sambamba wa kupata katiba mpya kwani alianza kujiuliza na kujijibu mwenyewe. Anauliza hao wakienda kwa watu wataenda kama nani na kwa sheria ipi? Watatoa wapi uhalali? Ukiona adui anapinga mkakati wako jua huo mkakati ndio wenyewe. Wengi tuliomsikia kijana kafulila akichambua BBC namna ya kuendesha huo mchakato tulivutika sana. Najua nccr chama bado pengine ndio maana kafulila alikuwa akisisitiza iunganishwe nguvu kwa vyama kama chadema na wanaharakati nje ya siasa. Kwa mtazamo wangu chadema tuchukue wazo hili. Ni agenda ya kudumu. Ndo kampeni ya urais 2015. Ni mpambano wa katiba mpaka kinaeleweka. Naamini slaa akibeba agenda hii kuanzia sasa uchaguzi ujao hakuna namna ya kumzuia ikulu. Lazma cdm ibane hapo. Ikiachia tu jk anateleza.