CHADEMA itabaki kuwa CHADEMA tu

Unaweza kutoa sababu za msingi kwa nini unapenda kuona uongozi wa juu ukibadilika mawazo yanayofanana na wafuasi wa CCM wanaotaka kuona Mbowe akiondoka.

Sababu ya kukaa muda mrefu itoe siyo sababu ya msingi.
 

If possible nitumie ulichotaka kiwe wazi PM nikianzishie uzi. Cheers.
 
 


Ni kweli kabisa, nilichogundua, wanachama hawaangalii mtu toka ccm.... wanachofanya ni kusupport maamuzi ya chama, hivyo lazima viongozi wake wajue kwamba wanachama hawajali umaarufu wa mtu, wanachoangalia ni kiongozi anayehitajika toka chadema............ kwa hiyo ni wakati sasa viongozi wa chadema kuacha kutegemea umaarufu wa watu toka ccm....... kuna vijana wengi na nina uhakika watapewa support na wanachma wengi wa chadema...... na hapo ndio ccm itatoka madarakani...... watu wote wenye element za kiccm/ walikuwa ccm.... hawapendwi, na hakuna mtu anakubaliana na maamuzi ya kuwaleta.... ila sema wanachama wanasupport tu maamuzi ya viongozi wao.
 
Unaweza kutoa sababu za msingi kwa nini unapenda kuona uongozi wa juu ukibadilika mawazo yanayofanana na wafuasi wa CCM wanaotaka kuona Mbowe akiondoka.

Sababu ya kukaa muda mrefu itoe siyo sababu ya msingi.

Post yangu namba 31 ina sababu hizo za msingi. Huenda hujaisoma. Anaweza kukaa madarakani hata miaka 40, ila usitegemee mafanikio yake kuvuka aliyofikia hadi 2015. Ninafahamu vizuri matakwa ya wanaccm kuhusu cheo cha Mbowe na nina uwezo wa kutofautisha propaganda na uhalisia. Ninajua propaganda za wanaccm na nimeweza na nitaendelea kuweza kukabaliana nazo. Ila nadhani umeitaja cdm kama taasisi lakini ww binafsi huamini katika utendaji wa kitaasisi bali mtu.

Samahani pia nahisi ww ndio Mbowe mwenyewe maana sio mara moja au 2 tumekuwa mimi na ww kutokukubaliana kwenye hiki cheo cha Mbowe, na mara zote utetezi wa hiki cheo imekuwa muda hauruhusu. Kama ww ndiye basi fahamu hujenga taasisi bali umejijenga ww na unapaswa kujilaumu ndani ya 15yrs kushindwa kuweka mazingira ya kupokezana vijiti.
 

Haya ni mawazo mujarabu kabisa. Nadhani viongozi wa cdm inapaswa watambue hili kwamba wanapowapokea watu toka ccm na kuwapa nafasi haraka haraka wanawavunja moyo sana wanachama waaminifu. Kama sehemu haina mgombea wa cdm hapo sawa, lakini sio sehemu yenye mgombea anatolewa dakika za lala salama na kupewa muhuni toka ccm.
 
Mkuu mimi hata mlango wa Chadema siujui ila ni mtetezi wa haki za mtanzania na mnyonge,

Chadema ni watu ni wanachama, Mbowe kawekwa na wana Chadema ataondolewa na wana Chadema, endapo wataona bado wanamhitaji kwa mujibu wa katiba yao watamchagua tena na binafsi nitamuunga mkono.

Nikuambie tu Mbowe hawezi kuondolewa kwa propaganda za CCM na ukiona mpinzani wako analialia kuhusu jambo fulani kuwa linamkera endelea kupigilia hapo hapo.
 

Mkuu uko sahihi kwamba Mbowe kawekwa na wanacdm na wao ndio wenye haki ya kumtoa. Kila siku naona propaganda za wanaccm pamoja na kwamba kwa mtazamo wangu ni muda sahihi Mbowe kupisha sina popote nilipo wahi kuwasupport na huwa nawaambia kiwazi wazi kwamba Mbowe atatoka kwa matakwa ya wanacdm sio kwa propaganda zao. Lakini hilo halipunguzi ukweli niliokuambia kwamba wakati ukuta.
 
Nimesoma sijaona sababu yeyote ya msingi kwa nini Mbowe apumzike, porojo ni zile zile kakaa muda mrefu.

Mafanikio hupimwa kutokana na uzalishaji, mapato, Chadema imeanza haina diwani hata mmoja haina mbunge hata mmoja haina halmashauri hata moja leo imekuwa threat kwa chama tawala still huoni mafanikio?

Unaposema huoni matawi mpya nafikiri huijui Chadema, Chadema sasa inaendesha programme ya Sera Mbadala, kufungwa kwa mbunge na kufutwa kwa Nasari ubunge nazo unamlaumu Mbowe ambaye naye juzi akatoka mahabusu? Nafikiri hata kupigwa risasi kwa Lissu utamlaumu Mbowe.

Ndiyo maana sisi tunaoziangalia siasa za Tanzania tukiwa huru tunawaona mnaoilaumu Chadema na Mbowe hamna tofauti na watu wasiojulikana.
 
kidumu chama cha demokrasia chadema
 

Mkuu nilitarajia ungenipa majibu kwenye paragraph ya pili ili kunionyesha uimara wa Mbowe. Ila naona umechomoka kwa hoja zile zile za mahaba niue. Sitaki kukukwaza sana maana kipendacho roho. Chukua tu ujumbe wangu kwamba wakati ukuta.
 
Mkuu nilitarajia ungenipa majibu kwenye paragraph ya pili ili kunionyesha uimara wa Mbowe. Ila naona umechomoka kwa hoja zile zile za mahaba niue. Sitaki kukukwaza sana maana kipendacho roho. Chukua tu ujumbe wangu kwamba wakati ukuta.
Mkuu kama unachukulia kuhama kwa madiwani na wabunge kwenda CCM ni kushindwa kwa Mkiti basi huzijui siasa za Tanzania, hujui nguvu inayotumika, polisi, msajili, hazina, mahakama, bunge, pole sana, halafu kujenga ofisi siyo siasa ndugu unaweza kufanya siasa bila kujenga hata chumba, Nyerere alifanya siasa chini ya miembe.

Jisomee kidogo mafanikio ya Chadema isiyo na ofisi. COPY & PASTE from somewhere. Hoja kwa hoja.

TREND YA USHINDI YA CHADEMA

CHADEMA kimepta usajili wa kudumu 21.01.1993 baada ya hapo kilianza kushiriki uchaguzi wa SM na Madiwani mwaka 1994. Toka hapo hadi sasa ushindi wetu kwa Madiwani, Halmashauri, Wabunge na kura za Uraisi umekuwa hivi;

*Mwaka 1994*
1. Madiwani 13 Tanzania nzima
2. Hatukupata Halmashauri hata moja.

*Mwaka 1995*
1. Wabunge tulipata wanne (4). Kati ya hao watatu wa Majimbo na mmoja wa Viti Maalum ambao ni;
- Karatu (Dr Slaa)
- Rombo (Masumbuko Lamwai)
- Kigoma Mjini (Dr Wared Kaburu)
- Viti Maalum alikuwa Mary Kabigi wa Mbeya.
2. Uraisi
- Tuliwaunga Mkono NCCR Mageuzi (Mrema)

*Mwaka 2000*
1. Madiwani tulipata 45 nchi nzima
2. Halmashauri mbili (Karatu na Hai)
3. Wabunge watano. Majimbo manne na viti maalum mmoja.
- Karatu (Dr Slaa)
- Hai (Freeman Mbowe)
- Moshi Mjini (Marehemu Ndesamburo)
- Kigoma Mjini (Dr Wared Kaburu)
- Viti Maalum alikuwa Grace Kihwelu ambaye yuko hadi leo.

*Mwaka 2005*
1. Madiwani 102 nchi nzima.
2. Halmashauri mbili (Karatu na Moshi Manispaa)
3. Wabunge tulipata 11. Watano wa Majimbo na sita viti Maalum. Ambao walikuwa;
- Karatu (Dr Slaa)
- Moshi Mjini (Marehemu Ndesamburo)
- Kigoma Kaskazini (Zitto)
- Mpanda Kati (Said A. Arfi)
- Tarime (Chacha Wangwe)
- Viti maalum walikuwa 6 pamoja na Halima Mdee, Grace Kihwelu na wengine.
4. Uraisi Freeman Mbowe
- Tulipata kura 670,000/=

*Mwaka 2010*
1. Madiwani 589 Nchi nzima
2. Halmashauri 7
- Karatu
- Moshi Manispaa
- Hai
- Musoma Mjini
- Ukerewe
- Ilemela
- Kigoma Ujiji (50/50)
3. Wabunge 49
- Majimbo 24 (Ni pamoja na kina Msigwa, Wenje, Mnyika, Halima, etc)
- Viti Maalum 25 (pamoja na Kiwanga, Lyimo, Conchester, etc)
4. Uraisi (Dr Slaa)
- Kura 2,300,000

*Mwaka 2015*
1. Madiwani 1108. Nchi nzima
2. Halmashauri 25 nchi nzima.
- 22 tunaziongoza
- 3 wametupora CCM (Kilombero DC, Sumbawanga MC, Kyerwa DC)
3. Wabunge tumepata 74
- Majimbo 35 pamoja na Ndanda
- Viti Maalum 37
- Africa Mashariki 2
Kati ya hao wanaume 29 na wanawake 45.
4. Uraisi (Edward Lowassa)
- Tulipata kura 6,080,000

*Tukutane kwenye Msingi, Tuongeze ushindi. CHADEMA haijawahi kudumaa wala kushuka katika ushindi.
 
Mnukuu mwenyekiti alivyosema, chama cha siasa ni jalala. Kwahiyo hatuwezi kuchagua wanachama, kila mwanachama ana umuhimu wake na wakati wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu nilitarajia unakuja na hoja za msingi kumbe unanibebea hoja nyepesi hivyo? Hiyo kwamba Nyerere alifanya siasa chini ya miembe mimi ndio nimekuwa nikiwajibu wanaccm hapa jukwaani toka 2013 walipokuwa wanaibeza cdm kutokuwa na ofisi. Hivi unaweza kukabidhiwa watoto uwaongoze kisha leo kapotea mmoja, kesho mwingine, na mtondogoo hivyo hivyo kisha useme bado una uwezo wa kuwaongoza? Hayo mafanikio ndio hayo ninayokuambia kilele cha Mbowe kwenye mafanikio ilikuwa 2015, kwa mtu asiyejijali bali kuamini taasisi angepisha mwingine. Haidhuru basi angesema uchaguzi ujao hatagombea ili kutoa nafasi kwa mwanachama mwingine. Narudia tena, wakati ukuta.
 
Mosi, kitu kimoja kikubwa CHADEMA haina, ambacho nadhani ni muhimu kwa siasa za Afrika ni kuwa na wanachama watiifu ambao ni watu kutoka vyombo vya dola kama TISS, JWTZ, POLISI na Mahakama.

Sina hakika kama nimekuelewa sa vizuri ulichokiandika hapa. CHADEMA watakuwaje na wanachama wa aina hiyo? Hata kama ndani ya vyombo hivyo kutakuwa na wanaowaunga CHADEMA mkono, sidhani kuwa wewe na mimi tunaweza kuwa na uhakika wa kuwafahamu bayana. Hawa watu ni waTanzania kama tulivyo sote, lakini matakwa ya kazi zao ya kupokea na kutii amri ni kikwazo.

Hali ikibadilika na kuruhusu amri kutofanya kazi utawaona wengi wakiwa upande huo.
 
Unataka Mbowe aingie msituni?, talk the alternatives ili tuzijadili tuzichambue kama ni relevant lkn kusema tu uwezo wake umeisha haina uzito wowote mtu yeyote anaweza kusema hivyo including his enemies.
 
Marcos Albanie anafaa sana kuwa katibu Mkuu wa CDM ni msomi mzuri na mwanaharakati anayejua kujenga hoja vizuri halafu Heche apewe kitengo cha itikadi na uenezi Mwalimu aendelee kuwa Naibu katibu Mkuu he is also brilliant sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku tutakayokubaliana kwamba Mbowe anapaswa kuwajibika kama kiongozi mkuu wa chama kwa upuuzi alioufanya 2015, chama kitapiga hatua kubwa sana.

Tuendelee tu kumtetea na kumkingia kifua kwa kusababisha chama kimpoteze Katibu mkuu mwenye ushawishi DR Slaa mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…