Kuna watu wanaifananisha Chadema na NCCR Mageuzi, wanaifananisha Chadema na CUF wengine wamefikia kuifananisha Chadema na ACT Wazalendo, hawako sahihi hawajui historia yake.
Chadema haikufika pale ilipo kwa kubebwa na vyombo vya dola imepambana kwa jasho la damu, haijafika hapo kwa kupata wanachama wa mkupuo wanachama wa mafuriko kama ilivyopata NCCR 1995 wakati Mrema alipohama CCM au kama ACT Wazalendo inavyopata wanachama wengi (Zanzibar) baada ya Maalimu Seif kuhama CUF. Chadema imewajenga wanachama na viongozi wake kutoka mashinani, wengi wa viongozi wake imewa groom yenyewe, Mnyika, Zitto, Mbowe, Mdee, Heche, Kafulila, Katambi nk.
Waliosahau historia ya Chadema naomba niwakumbushe kidogo. Mwaka 1994 Chadema ilikuwa na Madiwani 13 tu Tanzania nzima haikuwa na Halmashauri hata moja. Mwaka 1995 ilikuwa na Wabunge wanne (4). Mwaka 2000 ilipata Madiwani 45 tu nchi nzima. Kwa hiyo safari ya Chadema siyo ya kuangalia leo, yanayo wakuta ndugu zake ACT Wazalendo wao yaliwakuta zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Chadema ina wanachama wenye imani na damu ya demokrasia, wanaharakati, wanachama wake wengi siyo wanaofuata mtu, ina wanachama na wapenzi waliojitoa.
Kuwa mwanachama wa Chadema lazima u-risk kazi yako ref. Prof. Baregu, u-risk maisha yako ref. Tundu Lissu, u-risk biashara zako ref. Mbowe. Kama huna moyo wa kiuana mapinduzi, una tamaa ya utajiri, tamaa ya kazi serikalini, tamaa ya tenda Chadema siyo sehemu yako. Alikuwepo Dr. Slaa kaondoka mwenyewe, alikuja Lowassa na watu wake kaondoka na watu wake kaiacha Chadema na watu wake wasioyumba.
Chadema inajengwa na mfumo ambao unafika hadi vijijini kwenye mashina si rahisi kuuvunja, Chadema ya leo haina tofauti na Chama cha Mapinduzi CCM, imejengeka ki taasisi zaidi, CCM hata aondoke Magufuli itabaki kuwa CCM, vivyo hivyo Chadema hata aondoke Mbowe itabaki kuwa Chadema, si rahisi kuilinganisha na vyama vingine, vitakuja vitapata umaarufu na kama havitasimamia misingi vitaondoka na kuiacha Chadema.
Mchambuzi huru mwana JF Quinine.