Source: Mimi mwenyewe mwana CHADEMA
Source nyingine ni
Home
Inasomeka hivi:
Mnyika ataka Israel ibanwe
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka serikali kutoa tamko dhidi ya kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Ehud Barak, kwamba Tanzania si ya muhimu wala ya maana kwa nchi hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Barak alipofanya mahojiano na Radio Israel na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo wiki iliyopita.
Alitaja nchi muhimu na zenye maslahi kwa Israel kuwa ni Ujerumani, Uingereza na Ufaransa na siyo baadhi ya nchi maskini, ikiwamo Tanzania.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema kupitia kauli ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel, inaiona Tanzania sio nchi ya muhimu wala ya maana hata kufikia hatua ya kuilinganisha na eneo tu ndani ya Libya linaloitwa Tripolitania.
Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Benard Membe kuitaka serikali ya Israel kuomba radhi kufuatia kauli hiyo au kueleza wazi iwapo mazungumzo hayo ya Waziri Barak ni msimamo wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa yetu, alisema Mnyika.
Mnyika alisema barua pekee ya balozi wa heshima wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Lieberman ya kulaani matamshi hayo ya Waziri Barak na kumkaribisha mwakilishi wa Israel kutembelea Tanzania haitoshi kuifanya serikali ya nchi hiyo kutambua athari za kidiplomasia za kauli iliyotolewa.
GAZETI: NIPASHE