chadema ishukuru kupata wabunge 23! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chadema ishukuru kupata wabunge 23!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 14, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WANANCHI wametakiwa kutobabaishwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na chama hicho kutokuwa na nguvu ya umma, na badala yake wajikite zaidi katika kuijenga nchi kwa mshikamano bila kubagua itikadi za vyama.

  Aidha, viongozi wakuu wa Chadema wametakiwa kushukuru angalau kwa kuambulia ushindi katika majimbo 23 kati ya 239 ya uchaguzi nchini wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana.

  Hayo yalisemwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Stevin Kazidi, wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Kia wilayani Hai mkoani hapa, katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi na wanachama wa chama hicho kwa kuichagua CCM kuongoza nchi.

  Kazidi alisema wananchi wanahitaji kutambua kuwa Chadema haina nguvu yoyote ya Umma, na kwamba chama chenye nguvu ya umma ni CCM kutokana na kuongoza nchi na kuwa na idadi kubwa ya wabunge.

  “Watanzania hawajazoea vurugu kama za Chadema wanaotafuta madaraka kwa nguvu zote…uchaguzi umemalizika na kila chama kilipewa muda wa kufanya kampeni zake, wananchi walikata mzizi wa fitina nani anafaa na nani hafai ndo maana CCM ikashika
  madaraka, kinachotakiwa ni kutekeleza mahitaji ya wananchi na si kuwaingiza katika malumbano ya siasa,” alisema Kazidi.

  Alikitaka Chadema kushukuru kwa nafasi walioipata ya kuwa na wabunge 23 kutokana na wananchi kupiga kura za hasira kutokana na CCM kusimamisha wagombea wasiokubalika na kuondoa chaguo la wananchi, na kudai kuwa wananchi hao hawakukichukia chama bali mgombea aliyesimamishwa kugombea.

  “Mbowe na chama chake wana majimbo 23 kati ya majimbo 239 wakati usiku na mchana wanazunguka wakisema wana nguvu ya umma, je hapo kuna nguvu ya umma kweli…

  “Wananchi mnatakiwa kutambua muda mwingi viongozi wa Chadema wanatumia
  kuzunguka kwa maandamano bila kutekeleza ahadi zao, lakini serikali inayoongozwa na CCM inaendelea kuwahudumia wananchi wake bila kubagua ni wa chama kipi,”
  alisema Kazidi Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga, alisema wananchi wanahitaji kujipanga
  upya kwa kufanya maamuzi ya kutowachagua viongozi wanaosusia vikao vya Bunge ambavyo vinasikiliza kero zao, hatua inayowafanya kutotatuliwa matatizo yao kwa vile viongozi hao hawawasilishi malalamiko yao.

  “Kazi ya viongozi wa Chadema ni kupinga maendeleo ya serikali yanayoletwa kwa wananchi pamoja na kususia vikao vya Bunge ambavyo hutoa fursa ya kusikiliza matatizo ya wananchi na kuzitatua.

  “Tabia ya viongozi hawa inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi, ikizingatiwa sasa chama hicho kipo katika maandamano badala ya kuwahudumia wananchi,” alisema Mtenga.

  source: habari leo
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  yahe vipi,umeshapata ghahawa asubuhi hii?
  naona aliyepika alikuwa uchi ndio maana ghahawa inakulevya.

  By the way nakupa ofa ya kashata tatu ili upunguze mauzanduzandu.
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maumivu ya kichwa huanza polepole!!!!!!!
  ukiona kinazidi kuuma meza PANADOL (CHADEMA) Peoples power.
  Thanks in advance Mr Kashaga with your gabbages
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is a good way to start a monday. Chadema again! At least a minute doesnt pass without a word about the party that is causing CCM sleepless nights and restless days.

  Habari ya Katibu wa Wilaya imeandikwa kuliko habari ya Waziri Mkuu kuhusu mfumuko wa bei.

  It tells a good tale about where we have been, where we are and where we are going.
   
 5. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  People power forever...
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli CHADEMA kiboko wabunge 23, wanamfanya mkuu wa nchi na majeshi, mawaziri wake wote mbendembende. kweli uwingi si hoja. Hoja ni hao wabunge wananini cha kuwambia umma. kwani simba mmoja si anatosha kusambaratisha na kujilia nyama kiulaini toka miongoni mwa Nyumbu 100. Wabunge 200 CCM wanini kama wote wanounga mkono au wanoungozwa na mawazo ya mtu mmoja ( Mwenyekiti wao)
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  huyo nae ni mbumbumbu bado.. nahisi hajui hata kwa nini ni mwenyekiti wa chama chake

  kuelimisha umma kuhusu upuuzi unaofanywa na chama chake ye anaona sio kitu au inawauma sana wananchi wanapopata uelewa?
   
 8. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Pyuuuuuuuuuuuu!!!"Kashaga" again!! bojo notugora.
   
 9. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nidokeze Kero za wananchi amazo wabunge wa CCM wamezitatu au nitajie Maendeleo amabayo wamwwaletea wananchi, wewe unayasema hayo kwa sababu ni miongoni mwa watu wanaokula mara 3 au zaidi kwa siku, kunawatu hawawezi huko vijijini na unafahamu ila unafanya moyo wako kuwa mgumu kwa ubinafsi ulionao.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na tume ingekuwa huru mbona chadema ingezoa yote na urais mwaka huu!

  Na hao washukuru kuww wao ndio wanaounda tume vinginevyo wangekuwa wamesahaulika huko...
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Tell me your friends i'll tell you who you are!
   
 12. l

  lyimoc Senior Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona mwenyekiti kalewa
   
 13. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thank you for a nice joke on early Monday morning!!!!!
   
 14. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Yaani uchaguzi umeisha miezi mitatu iliyopita CCM wako hoi,mpaka leo hii CHADEMA utafikiri ndo chama kilichopo madarakani,wabunge 23 wa CHADEMA wanawatoa jasho CCM yote kweli wingi sio hoja,hawajui kuwa jinsi wanavyozidi kuiongelea CHADEMA ndo wanazidi kuipa umaarufu.CCM wameingia choo cha kike.
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda sielewi kiswahili, kuna chama chochote kilichosusia VIKAO VYA BUNGE vilivyokuwa vinajadili KERO za Watanzania???? Ni vikao vya lini hivyo na walikuwa wanajadili kero gani siku hiyo????
   
 16. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwani hujui chama kinachoongoza nchi hii wakati huu? CDM ndicho chama kinachoongoza kwa remote control. Kikisema CCM na serikali yao lazima wafanye kazi ama kwa kujibu hovyo na hivyo kuiimalisha zaidi CDM ama kwa kuyafanyia kazi. CCM na serikali yake hawawezi kuwa strategic. All the strategic thinking comes from CDM.
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  Kashoga Kashoga Kashoga Kashoga Kashoga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Uharo mtupu, unakera, hiyo tigo yako haichoki?
   
 18. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli sioni kama 2015 chadema atafanikiwa hata viti vitano nchini hasa kwa mwendo huu.
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Hivi Chadema ni viti 23 tu!, duhh wanakelele hao, mie nilifikiri wana japo robo ya viti vya Ubunge!

  Halafu wenyewe wanaamini kabisa kuwa Silaa kashinda uchaguzi! wanashangaza kweli, bado mnakazi kubwa sana ya kufanya mpaka wananchi wawakubali.
   
 20. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UMEONA EEEH? KURA ZENYEWE WALIPATA ZA HURUMA TUU HIVI WANAHISI WATU WAKICHAGUA CHADEMA AU WALICHAGUA MTU? KWAMFANO WALE WATU WALIOSHINDA KUPITIA CHADEMA WANGEWEZA KUSHINDA KUPITIA CHAMA CHOCHOTE KILE mfano,MTU KAMA ZITO,HALIMA,NDESAPESA,SUGU,ARFI, etc hawa wanaeza gombea chama chochote wakashinda
   
Loading...