na Francis Godwin, Iringa
ZIKIWA zimepita siku chache tangu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Said, kuifuta mahakamani kesi ya Diwani wa Kata ya Itunundu-Pawaga, Philipo Mkumbata, aliyekuwa akituhumiwa kuhujumu miundombinu, kwa madai kuwa kumfikisha mahakamani diwani huyo ni kuwapa nguvu wapinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Iringa, kimeonyesha kulipinga agizo hilo kwa kumtaka kulifuta.
Haya hapo juu yalikuwa matamshi au kulikuwa na barua? Hapa JF.....?
Kapwani alisema wanaamini kuwa katika kushughulikia suala hilo Waziri Mkuu amedanganywa na baadhi ya watendaji waliokuwa na malengo ya kisiasa zaidi lakini pia agizo hilo limemdhalilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Said, kwa kumfanya aonekane kiongozi asiye na mamlaka baada ya kuruhusu diwani huyo afikishwe mbele ya sheria
.
Halafu hapa upinzani na una sua sua, wanaamini Waziri Mkuu mwenyewe hawezi kutoa maamuzi hayo bila kudanganywa
😱
Sio jambo baya lakini linadhalilisha?
Hata hivyo alisema kuwa bado Pinda ana nafasi kubwa ya kubatilisha uamuzi wake, kwa sababu suala lolote lililopo mahakamani halipaswi kuongelewa au kutolewa uamuzi nje ya mahakama.
CHADEMA tunataka kesi hiyo namba 335/2008 iendelee kama ilivyoanzwa kusikilizwa na kwa sababu mali iliyoharibiwa ni ya Watanzania wote na si mali ya CCM, alisema Kapwani.
Siasa hizo hapo juu!
Naye Katibu Pascal Bella, alisema wana tuhuma nyingi za diwani huyo na wapo tayari kuzitoa na hapaswi kupewa msamaha na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama inavyofanyika hivi sasa.
Nafikiri ingekuwa hivyo "kapewa msamaha" basi lazima awe amehukumiwa? au?
Kali nyingine hapo chini...mie mbavu sina...
Bella alisema wapo tayari kuwasiliana na uongozi wa taifa wa CHADEMA ili kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa misingi ya sheria na kuondokana na mizengwe iliyoanzwa kufanywa hivi sasa kwa lengo la kupindisha sheria ili kulifanya liwe la kisiasa.😀
Alisema ni vema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akawa makini zaidi na matamshi yake anapofanya ziara mikoani ili kauli zake zisije zikamsababishia matatizo mbele ya jamii ambayo ina imani na utendaji wa kiongozi huyo.