CHADEMA ipo hatarini

Haya mabandiko mawili ya DR Slaa yananipa wasi wasi sana juu ya huu uwezo uliotumika kufikiri na kujiu posts za Logo.

Kiongozi hapaswi kuhamaki kwa vile tunaamini kwamba hekima na busara ni miongoni mwa vigezo vikuu vya kuwa kiongozi.
 
Mh dr. Slaa mimi naungana na wenzangu kwamba makao makuu hamjagawa madaraka/jimbo kikanda kama katiba ya chama inavyosisitiza. Sisi wamananchi tunategemea viongozi wa kata /jimbo wawe karibu na wananchi ktk huu muda tunaojiandaa kwenda kwenye chaguzi za serikali ya mitaa/vitongoji na uchaguzi mkuu wa 2015.

Kwa mawazo yangu mepesi sijafanya utafiti, naona viongozi wa kata na jimbo ninaloishi wako kimaslahi zaidi kuliko kuitisha vikao au kutembelea matawi na misingi kutuhamasisha kuhusu chaguzi zijazo za kiserikali. Huu ni wakati mwafaka wa kuhamasisha wale wananchi wenye uwezo na wanaokubalika kujitambulisha kwa wanachi wa mitaa na vitongoji ili wakati wa uchaguzi ukifika wajue wanataka kumchagua fulani wa chama fulani kwani anaweza kutuletea mabadiliko ktk sehemu husika.

Kwa upande wangu naona huu umuhimu ni wa msingi na msemo wa "the earlier the better" hapa ndio pake.
 
I know chadema is party that will liberate Tanganyikans from these black colonialists, ccm.No one should be worried about this.Let's give it a chance for sometime.
 
Logo ni mchungaji na anakemea mapepo.... Hii sentensi ni ya kukemea kwani jukwaa hili si la wachungaji peke yao wala chadema si ya wachungaji peke yao.
 
Pamoja na majibu makali ya dr slaa lakini ukweli utabaki pale pale kuwa hali ya mambo ndani ya chadema sio nzuri na hairidhishi.
 
Logo ni mchungaji na anakemea mapepo.... Hii sentensi ni ya kukemea kwani jukwaa hili si la wachungaji peke yao wala chadema si ya wachungaji peke yao.

Kidogo namimi nikutukane, soma vizuri hiyo post mkuu!
 
Dk Slaa kajibu vizuri tu nashangaa watu wanatoka povu hapa

Mlitaka awe kama Mr Dhaifu kucheka cheka tu?

Nchi hii inataka kiongozi mwenye msimamo na kauli kali za kukemea

Ni kweli kama kuna mtu anafikiria ki 47 huu si muda wake hatuitaji hayo mawazo ya zamani enzi za chama kimoja.

Dk Slaa ndo aina ya viongoz wanaotakiwa kuongoza taifa kama Tanzania
 
kwa mawazo hayo kweli kabisa itakuchua mda sana kukua kiakili ndugu ya embu jaribu kufikiri zaidi ya hapo kwa kweli.
 
Mbali na maelezo toka kwa Dr Salaa na Kamanda Makene, ndugu yangu Logo ninakuomba uzingatie nukuu ifuatayo " MWANADAMU ANAPO ACHA KUTAFAKARI MAMBO MUHIMU ANAKUWA ANAJIWEKA KWENYE KUNDI LA WANYAMA WENGINE. ANAWEZA KUISHI NA KUTENDA KAMA WANYAMA WENGINE .MUNGU ALITUPATIA AKILI NA UTASHI ILI TUISHI NA KUTENDA KWA KUTAFAKARI . NDIYO MAANA TUNAFIKIA HATUA YA KUWA NA MAADILI ,MIIKO ,UTAMADUNI ,MIONGOZO ,MIFUMO NA FALSAFA YA KUTUONGOZA KATIKA MAISHA ." By Padre Privatus Karugendo ,January 2, 2013 kwenye makala yake Gazeti Raia Mwema
 
Dah....
Wewe mtu si vizuri kujifanya Dr Slaa...
Najua Dr Slaa hajakomaa Kisiasa..lakini si kiasi hichi ulichoandika wewe..

Too low....

Kwanza Kiswahili kibovu...
Pili mipasho kama ya kizaramu...
Tatu umeandika kama umelewa...

Mkuu Bengo: jf walifanya vema kuruhusu kutumia majina yasiyo halisi. Heshima kitu cha bure kaka, wewe njoo na hoja hapa si mipasho, unashusha credibility yako mkuu.
 
Dr Slaa kamaliza, i too much dought Logo, upeo wangu unanituma kuamini sio mtu mzuri hata kidogo, he can be a TISS agent, for sure, ameingiza propaganda kwa umakini sana.
Amechomekea kuwa CHADEMA kinapendwa na wavuta bangi na wasio na kazi.
Amechomeka propaganda ya udini, yeye kajiita ni mchungaji na kampa uchungaji na Tumaini Makene.
Logo wherever you are, umeshtukiwa, be cursed.
 

Hii Thread imeletwa na Shushushu Logo Kwaa ajli ya Makanda wa CHADEMA Ingawa na yeye Tumestukia.
Ma CCM mnataka nini, mbona mko kama Ma bint wanaovunja Ungo Jaman
 

Umefika mbali sana huko! Pole sana!
 
Du ! Kama kweli hilo ni jibu la Dr Slaa , kamwe sitamwamini mwanasiasa yoyote :scared:
Ngoja nipiganie tu familia yangu
Ni kweli unachosema, kila mtu kajaaliwa kipawa chake, wewe unauwezo tu wa kupigania familia yako, mwache Slaa mwenye kipawa cha kuwapigania watanzania wote awapiganie.
 

Hayo ni mawazo yako, sijasema CHADEMA kinapendwa na wavuta bangi au na watu wasio na kazi, nimesema maandamano yaliyokuwa yafanyike yangekuwa na watu wengi kama hao. Kiswahili kigumu? Hivi siku hizi hata kusema mchungaji ni udini? Mmepoteza hata maana ya udini. Hata kama wewe ni mwanaCHADEMA tuweni na pointi tunapochangia siyo kubishana tu kipuuzi.
 
Hii Thread imeletwa na Shushushu Logo Kwaa ajli ya Makanda wa CHADEMA Ingawa na yeye Tumestukia.
Ma CCM mnataka nini, mbona mko kama Ma bint wanaovunja Ungo Jaman

Ni upeo wako tu wa ubongo mbandiko unaokusumbua. Huna hoja nyamaza siyo kutukana!
 
Haya mabandiko mawili ya DR Slaa yananipa wasi wasi sana juu ya huu uwezo uliotumika kufikiri na kujiu posts za Logo.

Kiongozi hapaswi kuhamaki kwa vile tunaamini kwamba hekima na busara ni miongoni mwa vigezo vikuu vya kuwa kiongozi.

Umesahau Kikwete. Alivyohamaki na kusema hataki kura za wafanyakazi? Au alipoanguka mbele za watu?
 
Upeo wako wa kujenga hoja sio mdogo, hadi Dr amestuka, kama una nia njema na CDM, carry on, kama uko against also carry on.
 
Mpaka sasa sijajua kinachojadiliwa ila nadhani nakiona kinachobishaniwa! Pole pole ndiyo mwendo TUTAFIKA TU!!
 
Upeo wako wa kujenga hoja sio mdogo, hadi Dr amestuka, kama una nia njema na CDM, carry on, kama uko against also carry on.

Hehehehehe heeeeee, usitake niimbe taarabu.
Mimi nisisherehekeee, pasaka ya kistaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…