CHADEMA ipo hatarini

Logo

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
588
Reaction score
49
Nawaomba viongozi wa CHADEMA amkeni, ITISHENI mkutano mkuu mkae mpange mikakati thabiti ya kukinusuru chama chenu kwani hali ya sasa inaiweka CHADEMA hatarini sana.

Suala la Lwakatare, Polisi kuiminya CHADEMA, mara Kigoma, mara wapi. Msikubali kunyanyasika kiasi hiki hata kwa damu. Unajua saivi wananchi wameanza kupoteza matumaini sababu wanaona ni kama CHAMA kinachowafanya wateseke sana, maana wakiandamana tu wanapigwa na kunyanyaswa sana, na CCM inawapaka matope mbaya kupitia polisi nyinyi mnasema tuna Mungu bila kujishughulisha?

Amkeni wekeni mikakati ya kukabiliana na nguvu hii ya CCM ya kuhakikisha CHADEMAinayeyuka kabla ya 2015. Mkikaa mkapanga mikakati yenu hata ikitangazwa tu kwenye vyombo vya habari adabu itarudi.



Jibu la LOGO


Dr. amejibu bila woga.

Logo naye anajiachia tena:-


Makene naye ametirirka:-


Logo anaongea na Makene,

 
Well noted brother. Nakubaliana nawe kamanda,ila hata wao haya wanayowafanyia cdm ipo siku watakuwa pembeni. walianza na ukabila, wakarudi na udini ,wakaja na ukanda na sasa wamekuja na ugaidi. Yalifeli na hili la ugaidi litafeli. Acha waendelee kuigandamiza cdm kwakuwa wameshindwa kuwaletea maisha bora watanzania
 
Dawa ni kubadili mfumo wa siasa zenu sio kulalamika.Haraka ya kwenda ikulu na kutofuata utawala wa sheria itawagharimu.
 
Mkuu umeandika jambo la msingi sana,maana baada ya kisa cha Mwangosi,chadema imesitisha mikutano yake ambayo kwa kiasi kikubwa imeweza kufungua wananchi macho na kupenda kudai haki zao,mfano suala la gesi mtwara ambalo wananchi wamelipigania kwa maslahi ya wanyonge
 
Chadema iko hatarini ndani kwa ndani,wa kuiua wako hoko huko kwenu.
 

mkuu ninachoamini hata kama chadema haitakuwepo ila haya matatizo yaliyopo ambayo chadema imeyaibua na kuelimisha watu na wakapata kuelewa ccm haitaishi milele tatizo la ccm linapambana na chadema pasipo kupambana na matatizo
 
mkuu ninachoamini hata kama chadema haitakuwepo ila haya matatizo yaliyopo ambayo chadema imeyaibua na kuelimisha watu na wakapata kuelewa ccm haitaishi milele tatizo la ccm linapambana na chadema pasipo kupambana na matatizo
Logo na WanaJF,

Kwanza nikubali kuwa CHADEMA hujali ushauri tunaopewa, na uwe mzuri au mbaya, wenye nia njema au la, hakuna ushauri usiofanyiwa kazi.

Hata hivyo, ushauri unawake kuwa ushauri, hula haugeuki kuwa Amrit, hivyo, si lazima ushauri kukubaliwa na kutekelezwa. Hata hivyo, Sina uhakika ni kwa kiasi gani umefanya utafiti wa kina kabla ya kutushauri. Inaelekea, bado una mawazo ya zamani ya maandamano, ya mikutano ya hadhara na kadhalika.

Aidha unaposema wananchi wanakata tamaa sina hakika unazungumzia wananchi wepi. Chadema kila siku, na kila eneo inatwanga M4C, Chadema kila kukicha inashinda chaguzi ndogo mbalimbali za vijiji na vitongoji hata mahali ambapo makao makuu hatujafika! Sasa ni wananchi gani na wa wapi unazungumzia! Inaelekea bado unafikiri ki 47"
 

Mh Katibu mkuu, kwa hiyo unaridhika na kasi ya ukuaji wa chama? I thought you would aim to grow at a much higher pace than that!

Sikupenda sana ulivyo down play mawazo ya Logo kwamba anafikiri ki 47!.

Hii inawatisha vijana wako kutoa ushauri kwa kuhisi kudhalilishwa kama msemo ulioutumia hapa.
 
Wanataka kutuaminisha kwamba kuna Tatizo kumbe mulishawaamusha wananchi muda mwingi wamejitambua wanaedneleza libeneke
 

Unatafuta sifa za mkizi wewe,kwani huyo Logo hasomi ,hapiti hapa JF na kuona jinsi vijana wanavyojitolea kwani kuwa wa mwaka 47 si ni neno tu
 
Kila kitu ukikisikia halafu ukaingia kichwa kichwa..utaumia ndugu yangu..ccm huwa wanapata shida sana kwa kuona kila jambo linavyotokea halafu cdm hawakurupuki kuwajibu..huwa linawapa shida sana..mbinu ni kutulia na kujipanga wapi pa kuanzia..mimi ninaimani sana na safu yote ya cdm...najua kila wakitoka wanatoka ni kitu kipya ambacho kinawaweka ccm kwenye wakati mgumu sana...
 
Sasa ni wananchi gani na wa wapi unazungumzia! Inaelekea bado unafikiri ki 47"
Shida mkishakuwa madarakani mnasahau kuwa hawa wanaofikiri ki 47 ndio wanaokubali kupigwa mabomu na virungu kwa ajili ya kuwaweka nyie madarakani. Ungeweza kutumia kauli nzuri isiyoonyesha namna yoyote ya dharau kwa wananchi wako na siyo kumwambia eti anafikiri ki 47.
 
Nimeshafafanua mara nzingi sana hapa JF.

Nanasema tena na tena kwa sababu kama walivyosema wahenga "Revision est mater studiorum"...


mkuu post zako nyingi unatumia nguvu kubwa kubadili ukweli kuwa uongo.cha muhimu unatakiwa kuamini ni kuwa kuna matatizo ya wananchi na haya hayatatuliwi kwa kupambana na chadema ila kwa kutengeneza ajira kwa vijana na kupunguza ugumu wa maisha kwa kupambana na mfumuko wa bei
 
Chadema kila siku, na kila eneo inatwanga M4C, Chadema kila kukicha inashinda chaguzi ndogo mbalimbali za vijiji na vitongoji hata mahali ambapo makao makuu hatujafika! Sasa ni wananchi gani na wa wapi unazungumzia! Inaelekea bado unafikiri ki 47"

Mwongozo wa Mkuu Invisible
Dr. anamaanisha nini?
 

He! Ok... True, Verified User huh? Kumbe!

Ngoja sasa leo nikwambie hili wewe mwenyewe uso kwa uso.

Punguzeni Upole hapo Kinondoni.... Tumechoka!
 
Lakin dk.slaa alisema walisimamisha wajipange na ukifka mwez wa tatua au wa nne kama ckosei ndo mpaka 2015,
 
Heshima kwako Dr.W. SLAA,nimesikitika sana kwa majibu ya kitoto na kipuuzi haya uliyoyajibu,kama kweli wewe ndo umejibu basi I THINK IS HIGH TIME kwa wewe kuwaachia hiki kijiti cha ukatibu mkuu waendeshe wengine mheshimiwa wangu,umepoteza uwezo wako wa kufanya utafiti kabla ya kujibu,umejibu kwa dharau ya hali ya juu tena kwa ubabe.

Sikutegemea kama unaweza mwambia mwanachama unayemuongoza kuwa anafikiria ki 47" hata sijui unamaanisha nini,je hujui kilichotokea karibuni kwenye mkutano alioufanya Tundu Lissu hapa DSM? walikuja watu wangapi? hukumbuki kauli alizozitoa kwa viongozi wa Chadema DSM? yote hayo ni dalili kuwa wanach wanapoteza imani na Chadema,iwe kwa matukio ya kweli au kwa kutengenezewa na Wapinzani wa CDM lakini matukio hayo yanashiria negative impresion for CDM,unazungumzia kushinda kwa uchaguzi wa vitongoji? Hoja ya kitoto sana hii mzee wangu,maana hakuna asiyejua overall ya uchaguzi huo ni CCM inaongoza kwa mbali na kama ndio ungekuwa ni uchaguzi mkuu basi CCM WANGEKUWA WANARUDI TENA MADARAKANI,

Pia naanza kupata hisia za kuwa si mtu wa kushikilia msimamo wa CHAMA CHAKO, NAONA UNAMJIBU KUWA ANA MAWAZO YA KIZAMANI TU KWA SABABU ANASHAURI MTUMIA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA WAZI..JE NI NANI ASIYEJUA KUWA CDM TUNAAMINI KATIKA MAANDAMANO? MARA NGAPI MMEKUWA MNATUSISITIZA TUHUDHURIE MAANDAMANO?(NGUVU YA UMMA)..

HILI LA KUTUAMBIA KUNA VITONGOJI CDM IMESHINDA HATA MAKAO MAKUU HAMJAFIKA -mzee umenishangaza sana kwa kweli siamini kama ni wewe umejibu kitoto hivyo,nataka nikuhakikishie kuwa WANANCH HAWACHAGUI VIONGOZI KWA SABABU NYIE MNAOJIITA WA MAKAO MAKUU MMEFIKA ILA NI KWA SABABU WANAIMANI NA WAGOMBEA WANAOKUWA WAMEGOMBEA MAENEO HAYO PAMOJA NA IMANI YAO KWA CHAMA(CHAMA SIO MAKAO MAKUU TU). NINA SEHEMU NYINGI SANA AMBAZO NYINYI MNAOJIITA MAKAO MAKUU MMEFIKA NA BADO CHAMA KIKAMWAGWA VIBAYA SANA,..USIWE NA JAZIBA KWENYE UKWELI,SAIZI HATA UKIPITA VIJIWENI WALE WATETEZI WA CDM WAMEPUNGUA AU WAMEKUWA NEUTRAL...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…