Chadema Ingeshindwa, ingekuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Ingeshindwa, ingekuwaje?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MAMMAMIA, Apr 2, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru uchaguzi umemaliza na mshindi ameshatangazwa. Pongezi CDM, pongezi Nassari, pongezi wana Arumeru kwa kushinda, mlistahiki - Hongera sana!

  Lakini wakati wa kampeni, tuliwasikia viongozi wa vyama vikuu vilivyokuwa vinachuana kila kimoja kikidai kuwa na haki kuliko chengine, kiasi cha kutambiana "piga, ua (more or less), lazima tushinde na tukishindwa hatukubali".

  Mshindi kapatikana, je CCM wameyakubali matokeo? Na hawatazua zengwe lolote?
  Na kama ingekuwa kinyume chake, CCM walitangazwa washindi, CDM wangechukua hatua gani?

  Naomba wanavyama, wapenzi na mashabiki husika watoe maoni yao.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kuna watu wamejipatia credit kwa kutabiri kuwa usiku lazma kuwe na giza.
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haijashindwa kwa hiyo hakuna maoni....
   
 6. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  ungesikia ccm wameiba kura.
   
 7. U

  Ubongo Silaha Senior Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kupata jawabu la swali lako tuangalie historia
  • Chadema walishindwa Biharamulo
  • Chadema walishindwa Kiteto
  • Chadema walishindwa Busanda
  • Chadema walishindwa Igunga
  Kote huko waliamini haki haikutendeka, na kote huko hawakuleta vurugu japo hawakuridhika
  Historia hiyo inakuambia Chadema ni chama cha aina gani
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ushindi wa chadema Arumeru ni ushindi mkubwa sana kwa Jakaya Mrisho Kikwete na CCM kwa mwenye kufahamu.
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  CHADEMA walishasema, kama watashindwa basi washindwe kwa halali na hawana shida juu ya hilo. Ambacho CHADEMA walisema hawakubali ni matokeo ya kuchakachua. Na ushahidi upo kwamba CCM walifanya kila mbinu kutaka kuingiza kura za bandia, ni bahati tu kwamba vijana wa CDM walisimama imara. Hii yaweza kuwa ni ushahidi kwamba hata Igunga, Biharamulo na Busanda pia CCM iliingiza kura za bandia. As far as CDM wameshajua mbinu ya CCM na wamejua namna ya kujilinda basi yafaa wadumishe mfumo waliouanzisha. Bila kusahau kumpeleka Lusinde mahakamani.
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kweli hii ni system at work. Jakaya anafaidika vipi na huo ushindi wa CHADEMA?
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  .....nadhani ungeongeza kwa kumuelewesha muulizaji kuwa experience ni mwalimu mzuri sana. inamfundisha mtu kutorudia pale alipofanya makosa awali (kwa mfano kutozuia vema wizi wa kura). experience iliyotokana na hizo by-elections ulizozitaja hapo juu product yake ni hii success story ya arumeru!
   
 12. S

  SARAMBA Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijajua lengo lako au pengine tumeishi kwa kudhani kuwa bila MAGAMBA tutakufa na jua kali. Jibu tumezoea kuonewa hivvyo tunge na tunaendelea kujipanga kwa 2015.
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  KAma hapo juu.

  Ni angalizo zuri.

  Ikiwa kuna uhakika hakukupita uchakachuaji, huyasikii hayo. Mara ngapi CDM imeshindwa na pale wanapokuwa wanahakika wameshindwa kihalali huwasikii kusema lolote?

  Pengine suali ulilifahamika vibaya, lakini hayo uliyoeleza ndiyo ambayo nimekuwa nikiyaona na lengo langu lilikuwa kuwachokonoa wenye mawazo tafauti na hayo.

  Hapa mimi si katika ya hao wenye kufahamu. Ufafanuzi plz!

  Hili la mwisho nimelipenda. Licha ya kuwa CDM imeshinda, lakini kwa matusi aliyomwaga Lusinde, kuna ulazima wa kumshitaki ili iwe funzo kwa wale wote wanaohisi "mdomo choo ni mtaji."

  Pamoja sana Mkuu. Mara zote nimekuwa ni mwenye msimamo wa kuwa karibu na wapinzani wako ili kujua mbinu zao.

  Lengo langu mkuu lilikuwa/ni kusikia upande wa pili wangesema nini ili tupate kuwarushia madongo ya hoja; bahati mbaya inaonesha wamenuna kiasi ambacho leo JF wanaiona chungu.
   
Loading...