chadema inaota ndoto za mchana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chadema inaota ndoto za mchana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 10, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  SERIKALI imesema propaganda zinazoenezwa na CHADEMA katika maandamano ya kutaka kuiondoa madarakani serikali ni sawa na ndoto za mchana. Hatua hiyo inatokana Tanzania kutawaliwa kwa kufuata mifumo mizuri ya kiuchumi, kidemokrasia, utawala bora na haki za binadamu. Pia, imeelezwa kuwa nchi ambazo viongozi wake wameondolewa madarakani kwa shinikizo la wananchi ni zile ambazo haziongozwi kwa kufuata misingi ya kidemokrasia.
  Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa kituo cha televisheni cha ITV.
  Akizungumzia uwezekano wa serikali kuondolewa madarakani kama wafikiriavyo baadhi ya watu, alisema kuwa suala hilo haliwezekani kutokea nchini, kwani kuna namna ya kuondoana madarakani.
  "Hakuna haja ya kuhangaikia suala hilo kwa hapa nchini kwa sababu halitafanikiwa labda katika nchi ambayo haina mfumo wa utawala wa kidemokrasia na ni aghalabu kutokea kwa Tanzania, kwani likitokea dunia haitakaa kimya kutokana na demokrasia iliyopo hapa," alisisitiza.
  Membe alitoa wito kwa wananchi kutokubali kupumbazwa na watu wachache wanaotaka kutoa picha nchini na duniani kuwa nchi imeshindwa kutatua matatizo wakati Tanzania ni ya kidemokrasia na inaheshimika duniani.
  Membe alisema kuwa serikali haijashindwa kutatua matatizo na inafanya hivyo kila mara inapohitajika pia wananchi wanatakiwa kufahamu hakuna 'mbinguni hapa duniani', hivyo wasidharau kile kinachofanikishwa kwani matatizo yaliyopo si ya kuwakatisha tamaa.
  "Haifai watu kuona hatujafanya chochote duniani, si vizuri kwa watu kutoa maneno kama tupo Palestina, their not fair to us," alisema Membe.
  Katika hatua nyingine, Membe aliweka kuwa kipindi hiki ndicho mwisho wake wa safari yake ya kisiasa jimboni Mtama, na kuongeza si haki kwa watu kumuwazia kuwa atagombea urais mwaka 2015 kutokana nafasi aliyokuwa nayo.
  Alisema kuwa kabla ya kupata wadhifa huo kuna wengine 12 waliowahi na nchi tangu ipate Uhuru imeongozwa na marais wanne, hivyo hicho si kigezo.
   
 2. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  je hayo ni ya kweli wanachadema?
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  tukuulize ww mtoa habari.we unadhani jibu sahihi ni lipi????
   
 4. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ulitaka aseme CHADEMA wakombozi wa kweli? kwani Membe hapendi kuwa waziri wa mambo ya nje? kwani hajasoma alama za nyakati za kale kuwa Ben alikuwa waziri wa mambo ya nje akawa rais na JK alifuata kuwa waziri wa hiyo wizara akawa rais? Anamatumaini bado trend ni hiyo hiyo !
   
 5. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  asante kwa kunisaidia,tuko pamoja mkuu
   
 6. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  kapate dozi Loliondo kwanza
   
 7. M

  Mndamba Namba 1 Senior Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kashaga unataka kutuambia nini sasa?unatunga mtihani hlf unaomba usaidiwe kutafuta majibu?we c utakuwa kilaza?hoja yako haina mashiko wala uweredi mi nilidhani kuvaa suti na miwani ya jua utakuwa smart hata kichwani kumbe bure kabisa vp na wewe umehongwa nini?cheo au?
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  huyu kachaga sijui haeleweki yaani yupo kama popo,aliweka thread yake kwenye hoja mchanganyiko akimponda dr mwakyembe kuhusu tuhuma za kuuawa,..baadae akageuka akaanza kumsifia,na huku nako kaweka pumba zake,.mi naona huyu ni malaria sugu au makamba(senior)...
   
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Chadema haifanyi kazi yake kwa kuangalia Wasira, Membe na wengineo wameseme nini, Chadema ni chama chenye viongozi na wana sera zao na watatekeleza mambo yao kwa manufaa ya taifa na wananchi wake!!!!!! bla bla za viongozi waandamizi wa ssm hazina nafasi ktk sera za Chadema.Viongozi wa ssm wanapenda kutega sikio eti Slaa, Mbowe, Halima,Tindu, Kabwe........ wamesemaje leo kuhusu serikali????????? Chadema haina muda huo. Sisi (Chadema) ni kazi kazi.
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Taratibu Mzee Kashaga, Wenyewe Chadema wamo humu jamvini; labda watakuwa wameenda lunch break, wakirudi jiandae kupokea mvua ya mwae!
   
 11. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  nchi kamwe haiwezi kupewa wahuni kama wa chadema,chadema wanachofanya sasa sio misingi iliyowekwa na waasusi wa chama kama mzee wetu mzee MTEI! CHADEMA POROJO NYINGI KULIKO SERA,SLAA NA MBOWE WANAPASWA KUWAAMBIA WATAWAFANYIA NINI WANANCHI AU KUTOA SULUHISHO LA MATATIZO YALIYOPO LAKINI WAKIENDELEA NA POROJO ZA MAMBO YA DOWANS,HIVI KUNA MTZ ASIYEJUA ISHU YA DOWANS ASA HIVI? SASA WANASHADADIA NINI?
   
 12. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama kuna watanzania waelewa wataipa kura Chadema;
  tumegundua mambo mengi sana....
  waongo sana,
  wapenda fujo,
  hawaheshimu sheria,
  walaghai,
  wachonganishi,
  wajasiliamali kupitia siasa,
  wabaguzi,(ukanda/ukabila,udini),
  wachochezi,
  wakulupukaji,
  wana tamaa sana.
  UKITAKA KUAMINI HAYA...
  Muulize KAFULILA atakupa full UKWELI.
  TUNAWAJUA SANA in AND out.
   
 13. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  I hope kwa akili zako CCM wanaendeleza ya mwasisi wa Chama chao hayati Mwalimu Julias Nyerere!!
   
 14. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kafikirie upya na utagundua watu wenye sifa hizo wapo chama gani.

  CHADEMA Kimesikika kwa watanzania ndio maana sasa mafisadi mnahofu kuu, sikuwahi kufikiri kwamba ipo siku nitashuhudia familia ya CCM ikikumbwa na Hofu ama kweli Chadema wamefanya kazi na bado, mimi namalizia mpango wa kwenda wilayani kwetu kufungua tawi la chadema na wazee wote wa ccm nitahakikisha wanahubiri sera za chama cha ukombozi Chadema.

  Chadema kaza buti safari bado ndefu kijiji hadi kijiji mpaka kieleweke, na hatutasumbuka na mafisadi ambao kwa sasa wamekimbilia Loliondo!! kwa mchungaji kula dawa za magonjwa sugu!
   
 15. M

  Msindima JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi neno sahihi ni kulupuka au kurupuka?
  Aise hivi ni chama gani kinaongoza kwa kuwa na watu wenye tamaa na kujilimbikizia mali ambazo si halali?
   
 16. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Eti nini? Mifumo mizuri ya kiuchumi?? Utawala bora??? Tanzania hii ya hapa kando ya bahari ya hindi au kuna Tanzania nyingine? Mifumo mizuri ya kiuchumi iko wapi na inamsaidia nani? Yale yale ya kula majani, 'hapa siyo mbinguni' ila kila siku kutembeza bakuli kuombaomba Ulaya! Au ulaya ndo Mbingu ya akina 'Maembe'? maana hata akiba zao wanaficha huko.
   
 17. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Acha uongo, Chadema sio wabaguzi, si wachochezi wala hawakulupuki, wewe ndio mchochezi kwa post zako zinazoonyesha uvivu wa kufikiri kwa wewe hapo. Chadema hawapo Kanda moja kama unavyofikiri Chadema wapo kanda zaidi ya moja, kama unabisha muulize Kafulila.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unajua ni vigumu sana kumwambia kipofu ukubwa wa Tembo, maumbile yake na pengine hata rangi yake kwa sababu mtu huyo ni kipofu..Mimi hadi leo hii nashindwa kabisa kuelewa kwa nini CCM wameshindwa kabisa kujibu swala la kisiasa kama chama badala yake wanalisukuma kwa serikali kuwatia hofu wananchi kuhusu Mapinduzi au machafuko yatakayotokana na Maandamano ya Chadema. Upofu huu umenza lini jamani?

  Chadema kama chama inatumia fursa yake kisiasa kuonyesha udhaifu wa sera za CCM ambazo zimetufikisha hapa. Na wazungumzaji wake wakubwa ni Mwenyekiti wa chama (Mbowe), katibu wake pamoja na viongozi wengine wa chama kuwaonyesha wananchi jinsi sera za CCM zilivyoshindwa kufanya kazi lakini maajabu ni kwamba CCM chini ya JK na Makmaba wameshindwa kabisa kujibu hoja hizi badala yake wamelisukuma swala kwa serikali ili wananchi Wadanganyika waendelee kuamini kwamba Chadema inataka mapinduzi baridi ya serikali iliyopo.

  Kama mnakumbuka JK wakati anaingia madarakani alisema wazi kwamba matatizo ya Umeme na maji yamerithiwa toka kwa Mkapa..Na ni majuzi tu JK mwenyewe amekiri kwamba yeye hataweza kuyaondoa matatizo ya nchi hii kama walivyoshindwa Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Sasa mimi sielewi ni sababu zipi zilizompa nguvu ya yeye kugombea Urais? Yeye alitegemea kufanya nini kilicho bora ikiwa leo matatizo hayo yanazidi kuwa makubwa zaidi na makosa sii yake ila amerithi?

  JKalituahidi kuleta Umeme wa dharura 2005, na mikataba iliyowekwa ilikuwa ya muda mfupi tu miaka miwili au mitatu, leo hii yupo madarakani miaka sita bado tunategemea Umeme wa dharura na bila shaka ile mikataba ya Watsira, Songas na Dowans imeshakwisha hivyo imeongezwa muda kwa sababu serikali yake haikuwa tayari na mkakati wowote wa kuchukua nafasi hii ya dharura.

  Halafu kibaya zaidi ni pale wanaposifia maendeleo hali nchi hii haijawahi kutokuwa na umeme, maji au miundombinu chakavu na mibovu kama wakati huu, sasa huo uzalishaji unaweza kuleta maendeleo utatoka wapi?.

  Sasa kama rais mwenyewe kwa kauli yake aliwaahidi wananchi kwamba ukosefu wa umeme ni swala la muda tu, leo miaka sita shida imezidi zaidi kutokana na mahitaji zaidi ya umeme, maji na kadhalika. Watu wamekosa tumaini hata la Afya zao kiasi kwamba anatokea Mlokole huko Loliondo anawavuta wagonjwa wote toka Hospital zetu kwenda kutibiwa huko bado serikali haioni jinsi wananchi walivyokosa tumaini hata la maisha yao kiafya. Watu wanaondoa na wagonjwa waliokuwa ICU wenye masindano mikononi, wengine wako ktk hali mbaya zaidi lakini wanaamini watapona wakienda Loliondo kuliko kuendelea kutibiwa Muhimbili..

  Hizi zote ni alama za Nyakati, CCM zisomeni kwa makini na mfahamu kwamba chama kama chama kimeshindwa kuongoza nchi kutokana na sera zake mbovu, ilani za uongo na kadhalika kwani hizi ndizo zinazosababisha maendeleo au matatizo zaidi. Watendaji serikalini hutekeleza tu sera na ilani za chama tawala hivyo Chadema hawailaani serikali wala utawala uliopo madarakani isipokuwa kuwaonyesha wananchi kwamba sera na ilani za chama CCM hazifai na ndizo chanzo cha matatizo yoote haya..

  Mwisho, Nawaomba viongozi woote waliopo serikalini wasitake kutumia unazi kujibu hoja za Chadema kisiasa..Zungumzeni kwa niaba ya chama kutetea sera na ilani ya chama chini ya kiongozi wenu JK ambaye ni mwenyekiti sio kutumia viongozi wa serikali kina Membe kutishia wananchi hali mkijua fika kwamba Chadema kama chama kimewakalia kooni..

  Matatizo yoote ya utawala wa JK ni ya kujitakia mwenyewe, huyu ni mtu ambaye sisi Watanzania wengi tulikuwa na imani naye Na sote kwa ujumla Waislaam na wakristu tulimpa kura zetu mwaka 2008 kwa asilimia 80, leo tena ashindwe kuongoza basi liwe na mchawi na hakuna mwingine isipokuwa Chadema na udini sijui nini hali wachawi wake anakula nao sahani moja. Kwa hali tulokuwa nayo leo hii Tanzania, hata kama Chadema isingekuwepo mimi naamini kabisa maandamano yangekuwepo tena bahati sana haikuwa ya CUF au NCCR - Mageuzi, enzi zao wakiwa vyama mbadala. Maandamano kama haya wangekufa wengi watu sana..
   
 19. elimumali

  elimumali Senior Member

  #19
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  100% ni ya kweli. They are Day dreaming.
   
 20. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa kauli kama hizo anafaa kwenda kwa babu yangu Loliondo kaka Asante
   
Loading...