Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kwa watu wanaonijua vyema, nina karama na uwezo wa kusoma siasa za nchi fulani na kutabiri mabadiliko ambayo wengi wanakuwa bado hawajayaona. Haya si majisifu, nasema tu ukweli.
Nilifanya hivyo kwa Obama kabla hajawa maarufu sana, nilifanya hivyo kwa Uhuru Kenyatta wakati huo anashika nafasi za chini katika chaguzi kuu, nilifanya kwa Trump wakati wengine bado walikuwa wanamuona msindikizaji, nilifanya hivyo kwa Muslim Brotherhood kule Misri kabla hata vuguvugu la Arab Spring halijatokea na nilifanya hivyo kwa CHADEMA miaka mingi iliyopita.
Muslim Brotherhood ilikuwa ni taasisi isiyo rasmi iliyojijengea misingi katika kila sekta ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Ni movement iliyokuwa imejijenga katika mioyo ya wamisri kwa muda mrefu. Ni movement iliyounganisha watu waliokuwa wanadai haki na usawa katika jamii.
Hakuna sehemu ambapo MB hawakuwepo, hata katika majela kwa sababu huko viongozi na wafuasi wao wengi walikuwa wanafungwa.
Wakati sahihi ulipowajia, MB wakachukua nchi kupitia chama kilichokuwa chini ya mwamvuli wao kwa sababu kulikuwa hakuna mbadala aliyekuwa na nguvu zaidi yao.
Naiona CHADEMA wakifuata mkondo huo huo.
Baada ya kupigwa marufuku kufanya siasa kwa miaka mitano, ilienda underground na kufanya maandalizi ya kuhamasisha, kuelimisha na kuwaandaa watu kwa ajili ya mabadiliko katika ngazi za msingi kabisa. Matokeo yake ndiyo tunayaona katika uchaguzi huu wa 2020.
Uchaguzi huu ni ngazi muhimu sana kwa CHADEMA katika kujiimarisha zaidi katika kila kona na sekta ya nchi hii. Wasirudi nyuma!
Maeneo machache ya kuboresha ili wafikie lengo hilo:
Haya nitakuja kuyaeleza siku nyingine ila itoshe tu kusema CHADEMA baada ya ushindi wasibweteke hata kwa sekunde.
Kuna njia nyingi zinaweza kutumika kuwakwamisha na kuwachafua, inabidi waanze kuzitambua mapema mbinu hizi kabla hata ya kupewa madaraka.
Mwisho, baadhi ya mabadiliko wanayopanga kufanya itabidi wayacheleweshe kwa muda wasije wakawa wanajifunga wenyewe vitanzi.

- Inabidi waende mbali zaidi na kujenga mahusiano na vyama vingine vya siasa ndani na nje ya Afrika.
- Wajipenyeze zaidi katika vyombo vya dola hasa Polisi na JWTZ na watafute jinsi ya kuonyesha wanakubalika huko. Mfano, CHADEMA kitaaminika zaidi na kuwa na nguvu zaidi kama kitaanza kuwa na support ya wazi kutoka kwa wanajeshi wastaafu. Wawape hawa wastaafu nafasi chache katika chama na zile za kugombea mfano Ubunge.
- Sura ya kitaifa. Chama kifanye juhudi za makusudi kutafuta na kuwapa nafasi mbalimbali za juu za uongozi wa chama watu wa makabila tofauti na pia kuwasogeza karibu Waislamu. Hili la Waislamu linawakwamisha sana CHADEMA na sijui kwa nini hawalifanyii kazi. ACT imechukua wafuasi wengi ambao kimsingi CHADEMA wangeweza kuwapata muda mrefu sana kama wangeweka nia ya dhati.