Chadema ina nguvu sana kisipuuzwe

Chadema ina nguvu sana kisipuuzwe

dala dala

Senior Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
107
Reaction score
109
Bila kuficha kuonesha hisia zangu za kisiasa, ni ukweli usiopingika kuwa CDM kwa sasa ina nguvu kubwa sana hapa nchini. Endapo chaguzi zitafanyika kwa mazingira ya haki na usawa sioni chama chochote kitakachothubutu kushindana nacho hasa upande wa Tanzania Bara. Kwa maoni yangu ipo haja kuheshimu matakwa ya wananchi hasa kuhusu kile wanachoamini kuwa Chama kitakachowavusha kuelekea ngazi nyingine ya Maendeleo. Yalitokea Zambia, Malawi, Kenya, Afrika Kusini, na kwingineko kwa hiyo si ajabu yakatokea hapa Tanzania. Mabavu sio suluhu, ila nguvu ya wenye nchi (Wananchi) ndio jibu. Changamoto waliyonayo CDM ni kututoa Watanzania hofu ya haya yafuatayo; 1: Ina Mipango gani ya kuivusha nchi kuelekea uchumi imara unaogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania ambaye siku zote amekuwa mhanga wa harakati za uchumi wa kibeberu? 2. Ina Mkakati gani wa kushughulikia tatizo linalokuwa kila siku la ukosefu wa ajira kwa nguvu kazi ya taifa yaani VIJANA? Nini msimamo wa Chama katika kushughulikia Raslimali za Taifa (Gesi na Madini mengineyo?) na mwisho, ni vema tukajua mikakati iliyopo katika kuboresha huduma za kijamii mfano Afya, Elimu na Maji. Kama uchaguzi ungefanyika leo, nisingeona tabu kuwapa CDM kura yangu.
 
Tumeanza na mungu tutamaliza na mungu
 
waache waendelee kulala na kupanga kufungua kesi za kughushi,kuratibu na kufadhili mauaji kwa watanzania na viongozi wa cdm!!!siku zao zahesabika
 
CHADEMA ime invest kwenye mioyo ya wananchi.
CCM wame invest kwenye ugaidi, mabomu, na smg za polisi.

Hiyo ndiyo tofauti iliyopo kati ya chadema na ccm.

CCM wanatakiwa wajue kuwa maisha ya watanzania ni bora kuliko siasa, hivyo wanatakiwa kuheshimu uamuzi wa wengi
 
watu wanayoiangusha chdm ni wabunge. akina slaa, zitto, ndesamburo na mdee kipindi kile walikua wachache lkn walijikita kwenye kujenga hoja na watanzania wakavutiwa na hoja zao. matunda yake ni kwamba idadi ya wabunge iliongezeka mwaka 2010. tatizo la akina sugu, wenje, msigwa, lissu, lema nk... ni utangulizaji wa jazba kuliko kujenga hoja kwa nidhamu kama ile ya 2005-2010. kwa hali hii, sidhani kama chdm kinaimarika. chama kinakimbiwa na watu makini kwa ss hivi. anaekataa hili basi ana sbb zake
 
Nakubaliana na wewe, lakini swala la kupigania rasilimali zetu si la Chadema peke yake bali ni kwa kila muumini yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu bila shaka wewe ni mmojawapo. Tushirikiane kuwaondoa hawa ngedere kwa nguvu zetu zote.
 
Bila kuficha kuonesha hisia zangu za kisiasa, ni ukweli usiopingika kuwa CDM kwa sasa ina nguvu kubwa sana hapa nchini. Endapo chaguzi zitafanyika kwa mazingira ya haki na usawa sioni chama chochote kitakachothubutu kushindana nacho hasa upande wa Tanzania Bara. Kwa maoni yangu ipo haja kuheshimu matakwa ya wananchi hasa kuhusu kile wanachoamini kuwa Chama kitakachowavusha kuelekea ngazi nyingine ya Maendeleo. Yalitokea Zambia, Malawi, Kenya, Afrika Kusini, na kwingineko kwa hiyo si ajabu yakatokea hapa Tanzania. Mabavu sio suluhu, ila nguvu ya wenye nchi (Wananchi) ndio jibu. Changamoto waliyonayo CDM ni kututoa Watanzania hofu ya haya yafuatayo; 1: Ina Mipango gani ya kuivusha nchi kuelekea uchumi imara unaogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania ambaye siku zote amekuwa mhanga wa harakati za uchumi wa kibeberu? 2. Ina Mkakati gani wa kushughulikia tatizo linalokuwa kila siku la ukosefu wa ajira kwa nguvu kazi ya taifa yaani VIJANA? Nini msimamo wa Chama katika kushughulikia Raslimali za Taifa (Gesi na Madini mengineyo?) na mwisho, ni vema tukajua mikakati iliyopo katika kuboresha huduma za kijamii mfano Afya, Elimu na Maji. Kama uchaguzi ungefanyika leo, nisingeona tabu kuwapa CDM kura yangu.
tuambie kwanza mikakati ya hichi chama kinachotawala yaani ccm alafu baadae ulinganishe na mikakati ya chadema kama kweli wewe ni msema kweli
 
Bila kuficha kuonesha hisia zangu za kisiasa, ni ukweli usiopingika kuwa CDM kwa sasa ina nguvu kubwa sana hapa nchini. Endapo chaguzi zitafanyika kwa mazingira ya haki na usawa sioni chama chochote kitakachothubutu kushindana nacho hasa upande wa Tanzania Bara. Kwa maoni yangu ipo haja kuheshimu matakwa ya wananchi hasa kuhusu kile wanachoamini kuwa Chama kitakachowavusha kuelekea ngazi nyingine ya Maendeleo. Yalitokea Zambia, Malawi, Kenya, Afrika Kusini, na kwingineko kwa hiyo si ajabu yakatokea hapa Tanzania. Mabavu sio suluhu, ila nguvu ya wenye nchi (Wananchi) ndio jibu. Changamoto waliyonayo CDM ni kututoa Watanzania hofu ya haya yafuatayo; 1: Ina Mipango gani ya kuivusha nchi kuelekea uchumi imara unaogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania ambaye siku zote amekuwa mhanga wa harakati za uchumi wa kibeberu? 2. Ina Mkakati gani wa kushughulikia tatizo linalokuwa kila siku la ukosefu wa ajira kwa nguvu kazi ya taifa yaani VIJANA? Nini msimamo wa Chama katika kushughulikia Raslimali za Taifa (Gesi na Madini mengineyo?) na mwisho, ni vema tukajua mikakati iliyopo katika kuboresha huduma za kijamii mfano Afya, Elimu na Maji. Kama uchaguzi ungefanyika leo, nisingeona tabu kuwapa CDM kura yangu.
tuambie kwanza mikakati ya hichi chama kinachotawala yaani ccm alafu baadae ulinganishe na mikakati ya chadema kama kweli wewe ni msema kweli,na utuambie kwa miaka yote wanaoongoza wamefanikiwa?
 
kama ni nguvu ya matusi hapo sawa mkuu nakubaliana na wewe
 
watu wanayoiangusha chdm ni wabunge. akina slaa, zitto, ndesamburo na mdee kipindi kile walikua wachache lkn walijikita kwenye kujenga hoja na watanzania wakavutiwa na hoja zao. matunda yake ni kwamba idadi ya wabunge iliongezeka mwaka 2010. tatizo la akina sugu, wenje, msigwa, lissu, lema nk... ni utangulizaji wa jazba kuliko kujenga hoja kwa nidhamu kama ile ya 2005-2010. kwa hali hii, sidhani kama chdm kinaimarika. chama kinakimbiwa na watu makini kwa ss hivi. anaekataa hili basi ana sbb zake
uongo wenu ndio unaipaisha chadema kwa nini hamtaki kusema ukweli? kama ni chama kisichopendwa na watu wengi kwa nini ccm wanatumia polisi? mbona hatuoni polisi kutumiwa kwa vyama vingine kama TLP,DP,NK. jipe moyo lakini mwaka 2015 uchaguzi ukiwa wa haki utashangaa, au jumapili uchaguzi ukiwa wa haki utashangaa
 
Nguvu za CHADEMA ni nguvu za Mungu. CCM hata mfanye nini hamuwezi kutupandia vichwani mwetu. Nawachukia CCM kama navochukia kinyesi cha chooni.
 
watu wanayoiangusha chdm ni wabunge. akina slaa, zitto, ndesamburo na mdee kipindi kile walikua wachache lkn walijikita kwenye kujenga hoja na watanzania wakavutiwa na hoja zao. matunda yake ni kwamba idadi ya wabunge iliongezeka mwaka 2010. tatizo la akina sugu, wenje, msigwa, lissu, lema nk... ni utangulizaji wa jazba kuliko kujenga hoja kwa nidhamu kama ile ya 2005-2010. kwa hali hii, sidhani kama chdm kinaimarika. chama kinakimbiwa na watu makini kwa ss hivi. anaekataa hili basi ana sbb zake

pole sana ni mtu gani makini alieikimbia chadema ?? Mtaje basi??
 
Bila kuficha kuonesha hisia zangu za kisiasa, ni ukweli usiopingika kuwa CDM kwa sasa ina nguvu kubwa sana hapa nchini. Endapo chaguzi zitafanyika kwa mazingira ya haki na usawa sioni chama chochote kitakachothubutu kushindana nacho hasa upande wa Tanzania Bara. Kwa maoni yangu ipo haja kuheshimu matakwa ya wananchi hasa kuhusu kile wanachoamini kuwa Chama kitakachowavusha kuelekea ngazi nyingine ya Maendeleo. Yalitokea Zambia, Malawi, Kenya, Afrika Kusini, na kwingineko kwa hiyo si ajabu yakatokea hapa Tanzania. Mabavu sio suluhu, ila nguvu ya wenye nchi (Wananchi) ndio jibu. Changamoto waliyonayo CDM ni kututoa Watanzania hofu ya haya yafuatayo; 1: Ina Mipango gani ya kuivusha nchi kuelekea uchumi imara unaogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania ambaye siku zote amekuwa mhanga wa harakati za uchumi wa kibeberu? 2. Ina Mkakati gani wa kushughulikia tatizo linalokuwa kila siku la ukosefu wa ajira kwa nguvu kazi ya taifa yaani VIJANA? Nini msimamo wa Chama katika kushughulikia Raslimali za Taifa (Gesi na Madini mengineyo?) na mwisho, ni vema tukajua mikakati iliyopo katika kuboresha huduma za kijamii mfano Afya, Elimu na Maji. Kama uchaguzi ungefanyika leo, nisingeona tabu kuwapa CDM kura yangu.

Kiongozi!

Mbona hilo wanalijua kwa herufi kubwa!! Unafikiri hizi songo mbingo wanazozianzisha CCM ni za nini? Kwa sasa wanacho kiomba ni kuhakikisha mbinu zao chafu za kizandiki zina fanikiwa. Kitu ambacho hakitafanikiwa. WaTanganyika wamesha shtuka kabisa. Kipimo walicho kuwa wanakisubiria ni uchaguzi wa Madiwani. Matokeo ya kura za ujumla yamewatia kiwewe si mchezo.
 
ccm ,ccm hapana huna jipya ccm..umetunyonya vya kutosha...sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,ccm mbona Mwl alikuacha mwema na kila mtanzania akakufurahia?..sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,ccm umekuwa chama cha biashara ,tena zile haramau,ukaacha kuhusudu haki..sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,ccm,walokufa wengi tena mikononi mwako,wale waliokukosoa uliwaona wasaliti..sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,tumekuchoka kwa zako siasa chafu,maovu wayapanga tena kwa waadilifu..sitamani kukuona wala kukusikia ccm
ccm ungekufa leo,wala nisingelia,utajiri wa tz waugawa kwa wachache,sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,ccm busara umekosa,ukaitupa sheria,dola waitumia bila hata ueledi,sitamani kukuona wala kukusikia ccm.
ccm,ccm,ccm kejeli wazidisha hata kwenye mambo ya msingi,elimu na afya didimia sababu ccm,sitamani kukusikia ccm.
 
watu wanayoiangusha chdm ni wabunge. akina slaa, zitto, ndesamburo na mdee kipindi kile walikua wachache lkn walijikita kwenye kujenga hoja na watanzania wakavutiwa na hoja zao. matunda yake ni kwamba idadi ya wabunge iliongezeka mwaka 2010. tatizo la akina sugu, wenje, msigwa, lissu, lema nk... ni utangulizaji wa jazba kuliko kujenga hoja kwa nidhamu kama ile ya 2005-2010. kwa hali hii, sidhani kama chdm kinaimarika. chama kinakimbiwa na watu makini kwa ss hivi. anaekataa hili basi ana sbb zake
Wabunge hawaendi mjengoni kuimba taarab ila kuwakilisha wananchi. Kwa mbunge mpinzani kuongea kwa jazba sio ajabu kwani serikalini kumejaa madudu. Sikiliza hoja anayotoa mbunge sio kuangalia usanii.
 
kama ni nguvu ya matusi hapo sawa mkuu nakubaliana na wewe

Ndg yangu Stroke, kama ni matusi nadhani hicho Chama shindani kwa CDM kimechafuka zaidi kwenye eneo hili. Tumesikia matusi mazito Bungeni (MB wa Kigoma Mjini), MB wa Mtera na wengineo. Pia matusi ni hurka ya mtu tu sina hakika kama Chama makini kinafundisha Wabunge wake kutukana. Bado katika mizania ya Siasa za sasa CDM ni tishio. Jiulize kwanini Watawala hawana muda tena na CUF au NCCR Mageuzi isipokuwa CDM? Kwa yeyote mwenye uwezo wa kuchambua mambo (Being analytical) ataungana na hoja yangu ya Msingi kuwa CDM ina Nguvu Sana Hivyo Watawala Wasikipuuze. Hila yoyote dhidi ya CDM si mtaji kwa watawala bali SIASA SAFI ndiyo itawarudisha Watanzania kujaribu kusikia nini kinazungumzwa na watawala wa sasa!
 
pole sana ni mtu gani makini alieikimbia chadema ?? Mtaje basi??

simaanishi vigogo wa chdm au watu maarufu. namaanisha raia wa kawaida walio makini ktk kufuatilia mambo ya kisiasa nchini. hata wimbi la wanachuo kujiunga na chdm limepungua. unaweza kukataa lkn nikupe mfano mmoja. ktk uchaaguzi wa madiwani wiki iliyopita, ktk kata 22, ccm imeshinda kata 16. kata 6 zimechukuliwa na cuf na chdm. kama umaarufu wa chdm umeongezeka, kwa nn haijashinda angalau kata kumi hadi 15? siasa hupimwa kwa ushindi ktk chguzi na siyo makelele kwenye mitandao
 
Acheni kudanganyana. CHADEMA haina uongozi wenye weledi, huwezi tegemea hawa form four F na watu wa divinity waongoze taifa hili. Wabunge wao wengi wana elimu za mashaka. On top, CHADEMA ni chama kinachostawi kwenye migawanyiko na sio kwenye umoja. Ndio maana wanachochea migawanyiko ya kidini, kanda, na kikabila ili kubaki politically relevant!
 
Hii inadhihirisha jinsi CCM na viongozi wake walivyo vilaza. sasa kama viongozi wa chadema ni form four F na watu wa divinity amboa pia ni wachache wasio na weledi lakini wanawatoa mapovu CCM na viongozi wao wasio form four F na divinity, wenye weledi na wengi. Unapata conclusion gani?

1. Je hao waliofeli walifeli kimakosa na waliofaulu wamefaulu kimakosa? au
2. Nchi hii inatakiwa kuongozwa na watu wachache ambao hawana weledi na wawe Form four F na divinity!

Ifike mahali mkitumwa muwaulize 'mabwana' zenu "tukaandike nini?" wasiwaachie hivi hivi mnapwaya sana!
 
Back
Top Bottom