CHADEMA imeshinda chaguzi kwa nguvu ya umma sio Tume ya Uchaguzi. Tusidanganywe

Kwa hiyo unahitaji kuona mbinu ile ile ya kulinda kura itumike watu waumie na kufa ndio furaha yako..

Adui yetu ni CCM sio CDM, sasa wewe uko bize kupambana na CDM hapa jibu ni jepesi na wewe ni CCM..
Mkuu huyu Kiazi hata hao MACCM hawamtambui. ndio maana kutwa anaacha number ya simu wamtumie bando.
 
Chama cha siasa ili kiwe imara kinahitaji mbinu mbadala na resources ambaza humo ndani ya resources kuna watu na vitendea kazi vyao(Pesa) Kama Hakuna au kuna ukata lazma kifail.
 
tindo, nitakubaliana na wewe kuwa nimepotoka au ninapotosha kwa makusudi, kama utarejea Ibara au kifungu chochote cha Katiba ya JMT (1977) inayominya demokrasia!

Mwengeso muogope Mungu, Baba wa Taifa aliwahi kusema kwa katiba hii angeweza kuwa dictator kwani inampa madaraka makubwa kutawala nchi. Kama baba wa taifa aliwahi kukiri tena bila kutaja vifungu kwamba katiba hii haifai iweje wewe uone iko sawa?

Huenda mimi sio bingwa wa kutaja vifungu vya katiba kwani hapa nilipo siko nayo mkononi, lakini kwakuwa wewe unayo hapo mkononi nionyeshe ndani ya hiyo katiba kifungu kinachoruhusu rais wa nchi kushitakiwa akiwa ama akitoka madarakani. Baadhi ya mapangufu makubwa kabisa ya katiba yetu ni kumpa rais madaraka makubwa kiasi kwamba anakuwa juu ya sheria na hata katiba yenyewe kiuhalisia. Nina hakika nitakuwa sawa kabisa, ukimuacha Mwl.Nyerere hatujawahi wala hatuna rais muadilifu. Sasa kama hatuna wala hatujawahi kuwa na rais muadilifu huku katiba imempa rais madaraka ya kuwa baada ya Mungu ni yeye hiyo katiba huwezi kuona mapungufu yake?
 
Mambo ya chama kufa nimeanza yaskia toka Wasira ni waziri na mbunge lakin hadi leo chama kipo na yeye sio mbunge wala waziri

Pia hata Magu alitabiriwa ccm kumfia lakini tunaona yanayotokea leo

So achana lamli chonganishi..
Mhh!
Sijui ulikuwa unaijua NCCR Mageuzi ya Lyatonga Mrema, Je unazijua enzi CUF "ngangari". Enzi za Cuf Maalim au Lipumba kukohoa tu...Buguruni na Kidongo Chekundu kunalipuka.
Wahenga walisema, ajidhaniaye amesimama......malizia mwenyewe.
 
Mwengeso muogope Mungu, Baba wa Taifa aliwahi kusema kwa katiba hii angeweza kuwa dictator kwani inampa madaraka makubwa kutawala nchi. Kama baba wa taifa aliwahi kukiri tena bila kutaja vifungu kwamba katiba hii haifai iweje wewe uone iko sawa?

Huenda mimi sio bingwa wa kutaja vifungu vya katiba kwani hapa nilipo siko nayo mkononi, lakini kwakuwa wewe unayo hapo mkononi nionyeshe ndani ya hiyo katiba kifungu kinachoruhusu rais wa nchi kushitakiwa akiwa ama akitoka madarakani. Baadhi ya mapangufu makubwa kabisa ya katiba yetu ni kumpa rais madaraka makubwa kiasi kwamba anakuwa juu ya sheria na hata katiba yenyewe kiuhalisia. Nina hakika nitakuwa sawa kabisa, ukimuacha Mwl.Nyerere hatujawahi wala hatuna rais muadilifu. Sasa kama hatuna wala hatujawahi kuwa na rais muadilifu huku katiba imempa rais madaraka ya kuwa baada ya Mungu ni yeye hiyo katiba huwezi kuona mapungufu yake?

Yaani katika Katiba ya JMT (1977), inayotumika kwa sasa, mapungufu nakubwa yake ni ya madaraka ya Rais! Du!

Ni kweli Ibara ya 46(1) inasema: Wakati wowote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

Lakini Ibara ya 46A(1) inasema: Bila kujali masharti ya ibara ya 46 ya Jatiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

Katiba iliyopendekezwa, ibara 96(1) pia inasema: Wakati Rais akiwa madarakani, hatashtakiwa wala mtu yeyote hataendesha mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa ajili ya lolote la jinai. Lakini ibara ya 97(1) nayo inatoa nafasi kuwa: Bunge linaweza kupitisha azimio la kumwondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii.

Hata Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa ilikuwa ina ibara hizo hizo ya 93 na 95.

tindo, kwa utu uzima wako na elimu yako naamini unajua umuhimu wa kuweka kinga kwa Rais aliyeko madarakani dhidi ya mashtaka, haijalishi ni wa chama kipi. Hata maandiko matakatifu yasema: Tumpe Kaisari Kilicho cha Kaisari na Mungu kilicho cha Mungu - Is 45:1,4-6; Thes 1:1-5; Mt 22:15-21

Kwa hiyo siyo sahihi unaposema kwamba katiba imempa rais madaraka ya kuwa baada ya Mungu ni yeye[/I.

Kati yangu na wewe ni nani anayepotosha.

TUWE MAKINI KWA HOJA ZETU.
 
Mleta mada kama ccm imefika dau basi chapa mwendo acha kurusharusha miguu... Mahangaiko yote haya yanaonyesha uko tayari kwenda ila jamaa wamekukaushia kwani huna impact yoyote...wakuchukue kwa mkopo mkuu
 
Mkuu Benson Mramba , wewe umesita lini kuwa kijana wa Mbowe? Au kwakuwa huna jina kubwa la kutangazwa ukihamia CCM?(JOKING). Hivi, huzioni changamoto katika mfumo wa uchaguzi hapa nchini?
Mkuu mwanasheria msomi kama mnavyoitwa.
Kuna hoja kubwa jamaa kaziweka.
Tutambue kwamba kususuia ni kupoteza zaidi, unakosa kuitumia fursa ya kukipa uhai chama kwa kufanya siasa za majukwaani.

Pili tukubali kwamba hayo mapungufu yanatatuliwa kwa kuwasilisha hoja bungeni ya kufanyia mabadiliko sheria husika. Lakini wakati wa kampeni ndio wangeshitaki vizuri kwa wananchi na kuipa shinikizo serikali na wabunge wa CCM. Hivyo fursa hii sasa wataipoteza na wakipeleka bungeni kule wao wapo wachache watashindwa na vile hakuna bunge live wenzao hawataogopa kuchukiwa na umma.

Mramba hajasema kama hakuna mapungufu.
 
Mhh!
Sijui ulikuwa unaijua NCCR Mageuzi ya Lyatonga Mrema, Je unazijua enzi CUF "ngangari". Enzi za Cuf Maalim au Lipumba kukohoa tu...Buguruni na Kidongo Chekundu kunalipuka.
Wahenga walisema, ajidhaniaye amesimama......malizia mwenyewe.
Chadema isefe wakati ina wabunge 5 ije kufa leo
 
Chadema isefe wakati ina wabunge 5 ije kufa leo
Ninachosema ni kwamba, tahadhari hii sio ya kupuuza. Ifanyiwe kazi na Chadema.
Na Chadema ya leo sio ile ya 2010-2015.
Wajitathimini, kujikosoa na kujirekebisha.
 
Mkuu Benson Mramba , wewe umesita lini kuwa kijana wa Mbowe? Au kwakuwa huna jina kubwa la kutangazwa ukihamia CCM?(JOKING). Hivi, huzioni changamoto katika mfumo wa uchaguzi hapa nchini?
Ukiwa kama wakili msomi,umefanya nini ili kwenda mahakamani kupinga dhulma na hayo matokeo?
Kulia mitandaoni hakusaidii,fungueni kesi ya madai au ya kikatiba,hata kujaribu tu kutingisha muhimili mnaishia kulalamika mitandaoni
 
Mkuu mwanasheria msomi kama mnavyoitwa.
Kuna hoja kubwa jamaa kaziweka.
Tutambue kwamba kususuia ni kupoteza zaidi, unakosa kuitumia fursa ya kukipa uhai chama kwa kufanya siasa za majukwaani.

Pili tukubali kwamba hayo mapungufu yanatatuliwa kwa kuwasilisha hoja bungeni ya kufanyia mabadiliko sheria husika. Lakini wakati wa kampeni ndio wangeshitaki vizuri kwa wananchi na kuipa shinikizo serikali na wabunge wa CCM. Hivyo fursa hii sasa wataipoteza na wakipeleka bungeni kule wao wapo wachache watashindwa na vile hakuna bunge live wenzao hawataogopa kuchukiwa na umma.

Mramba hajamasema kama hakuna mapungufu.

Kama kuna mwananchi ambaye hajaona ukatili na unyama wanaofanyiwa wapinzani basi atakuwa ni mtoto chini ya miaka 7. Kususia pia ni njia moja wapo ya kudhibitisha kwamba kuna shida maana kama ni kushitaki kwa umma imeshafanyika sana. Au mnataka mpaka watu waanze kuuna ndio mjue na kuamini kuna tatizo? Kama mnaamini kukubalika na wananchi ni lazima mkiuke njia zetu za kupata madaraka kistaarabu basi sisi tunasema chaguzi za hivyo ni za wati washenzi tu.
 
mwengeso Kwanza nikupongeze kwa kupoteza muda wako kujibu hoja yangu tena kwa kutaja vifungu kabisa. Hongera sana. Sasa tuje kwenye uhalisia, unasema mapungufu ya katiba ni madaraka ya rais tu? Hakika mapungufu mengi ni kwenye mambo y utawala ambapo mapungufu yake kwenye taasisi ya urais ndipo yanajionyesha zaidi. Leo hii hakuna taasisi za kiutawala inayoweza kufanya kazi bila kujali hofu ya rais ni kwanini hayo yanatokea. Ukiachia bunge tena kwa mbali taasisi nyingine zote viongozi wake ni wateule wa rais. Mfano Mahakama, jeshi la wananchi, polisi, gavana wa bank kuu, Takukukuru, tume ya uchaguzi, hizi ni kwa uchache.

Taasisi hizo nilizotaja ni nadra kufanya majukumu yake bila macho hasa kufumbia macho udhaifu wa rais. Katika mazingira haya kuniambia rais anaweza kuogopa kutolewa madarakani na bunge kwa vile vifungu ni kama kuonan watoto. Wote ni masahidi bunge linavyotii na kuonyenyekea serekali hata kwa madhaifu ya wazi. Kuna wakati Mh. Zitto alipitisha petition ikitaka kumuwajibisha PM, kilichotekea hofu iliyowakumba wabunge wa ccm hata kumsogelea tu Zitto ilikuwa shida. Sasa hiyo ni kumuwajibisha tu PM watu wameogopa hivyo huyo rais?

Nitakupa mifano michache kukuonyesha nchi sio katiba yenye nguvu bali rais kwanza kisha katiba. Juzi tuliona rais akiwapokea madiwani waliohama cdm kwenye hafla ya kijeshi na watu wa aina yako mkakaa kimya. Kibaya zaidi anayedhaniwa kuwa nyuma ya huo mchezo mchafu akapandishwa cheo huku tuhuma zake tena za kurekodiwa zikiwa mezani Takukuru. Mbona tumeona chaguzi za ccm wahusika wakikamatwa na Takukuru kwa tuhuma tu, iweje huyu kapata na cheo kabisa? Hayo ni madhaifu ya katiba ambapo madaraka ya rais yanatumika kwa utashi wake.

Hayo niliyotaja ni baadhi tu ya mapungufu ya katiba hii japo yapo mengi, ila zaidi ya nusu ya mapungufu ya katiba yetu yamejikita katika nguvu za rais huku zikitengeneza taasisi dhaifu.
 
Jitahidi lakini huko ccm hakuna anayekufahamu hivyo hukuna anayeweza hata kukupa elfu kumi. Wenzako akina Kafulila wanafahamika na wananchi nchi nzima, sasa wewe ulikuwa unashinda ofisini kupika chai nani anakufahamu? Tafuta namna nyingine ya kutoka, hii ya kuichafua cdm wala haikutoi. Bora zamani Polepole alikuwa anaingia humu jf, sasa hivi hathubutu anashinda twitter na instagram. Huku ujumbe wako hautoonekana. Ukiona hauleweki nenda kwenye ofisi za gazeti la uhuru kesho andika makala ya kuiutusi cdm na Mbowe, nina hakika utaweka kwenye front page kuonyesha cdm imechokwa na wala sio huku jf.
Hakuna anayeichafua CDM. Kuna wahalifu wachache wamemzunguka Mwenyekiti ndio wanaoichafua Chadema
 
Kwanza nikupongeze kwa kupoteza muda wako kujibu hoja yangu tena kwa kutaja vifungu kabisa. ...ASANTE

Hakika mapungufu mengi ni kwenye mambo y utawala ambapo mapungufu yake kwenye taasisi ya urais ndipo yanajionyesha zaidi. Leo hii hakuna taasisi za kiutawala inayoweza kufanya kazi bila kujali hofu ya rais ni kwanini hayo yanatokea. ...

Mfano Mahakama, jeshi la wananchi, polisi, gavana wa bank kuu, Takukukuru, tume ya uchaguzi, hizi ni kwa uchache.

Taasisi hizo nilizotaja [ni nadra kufanya majukumu yake bila macho hasa kufumbia macho udhaifu wa rais. Katika mazingira haya kuniambia rais anaweza kuogopa kutolewa madarakani na bunge kwa vile vifungu ni kama kuonan watoto. ...
Nasikitika sana tindo kwa hoja zako za hisia nje ya misingi mikuu ya kiutawala. Pia nashangaa unavyotuhumu viongozi, wenye heshima zao katika jamii, mbali ya uwezo wao kitaaluma, kwamba wanafanya kazi kwa woga wa aliowateua! Je, upande unaoutetetea ndivyo viongozi huko wanavyofanya kazi zao kwa kumfurahisha BWANA.

Inatia aibu kama kuna viongozi ambao wanawajibika kwa sababu ya mtu na siyo Katiba, Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo.

Nitakuelewa kama utaweka Ibara/Vifungu vya Katiba, Sheria, Kanuni au Taratibu zinazombana kiongozi yeyote kutekeleza ya Mkuu wake wa kazi.

TUONDOKANE NA HISIA katika masuala mazito ya kiutawala.
 
Mwengeso ww unazungumzia job description, wakati mimi nazungumzia uhalisia. Simtuhumu mtu kwa kumdhalilisha pls don't get me wrong bali kwenye mapungufu nasema ukweli bila woga waka kujipendekeza. Sina upande ninaoutetea bali nazungumzia ukweli hivyo kama ww uko hapa kutetea upande huwezi kukiri udhaifu. Unajua ww uko kwenye ajira ya serekali na kwa kuwa uko ndani ya box basi huna uwezo wa kuona tunachoona wengine. Na hata kama unauona unautazama kwa jicho la mtoto wako na jicho la mtoto wa kambo. Toka nje ya box uweze kuona.

Mwengeso ujue sisi ni watu wazima kama ulivyo ww na ndio maana hata kama tunatofautiana kimawazo lakini tunaheshimiana. Unapotuona watu wazima wenzio tunasema kuna mambo hayaendi sawa usitukejeli kwa kusema tunataka uhuru usio na mipaka kisa ww au kundi unalolitetea unafaidika nalo. Angalieni malalamiko ni nini, na wapi ni madai halali yafanyiwe kazi, mengine tunaweza kusubiri kwani muafrika na madaraka ni tatizo. Udhaifu huu wa kiafrika tunaujua lakini usipite kipimo mpaka kuanza kufanyiana unyama sisi kwa sisi kisa madaraka.
 
Mwengeso ww unazungumzia job description, wakati mimi nazungumzia uhalisia. ...

.... Angalieni malalamiko ni nini, na wapi ni madai halali yafanyiwe kazi, mengine tunaweza kusubiri kwani muafrika na madaraka ni tatizo. Udhaifu huu wa kiafrika tunaujua lakini usipite kipimo mpaka kuanza kufanyiana unyama sisi kwa sisi kisa madaraka.
Hakuna ibara/kifungu chochote cha Katiba kinachompa mtu nguvu juu ya wengine. Hakuna ibara/kifungu cha Katiba kinachomfanya mtu kuwa mtumwa wa mtu mwingine. Hivyo, udhaifu wa mtu mmoja mmoja, au kwa makusudi au kutokujua, kujiweka mnyonge, kusiwe ni sababu ya kile unachhokiita malalamiko.

Inasikitisha pale viongozi wa siasa wanapowafanya wananchi, wapiga kura, ngazi za kupata madaraka. Wakishapata madaraka wanawatumia kubaki madarakani. Hiyo ndiyo inaitwa POLITICAL POWER.

Nasisitiza kiongozi anayefanya kazi kwa woga hata kama Katiba itabadilishwa vipi atabaki hivyo hivyo na unyonge wake. Na msingi wa unyonge ni KUTOKUJIAMINI (elimu duni au/na umaskini wa fedha na fikra).

Kama hutotaja ibara/vifungu vya Katiba vinavyominya haki na uhuru wa Mtanzania, tutaendelea kubishana kinadharia tu.
 
Kumbe unabishana mimi nilidhani tunapeana elimu. Sasa kama unabishana naona nikupe ushindi maana ni dhahiri unatafuta ushindi. Sina tabia ya kubishana huwa ninapima hoja na kuangalia uhalisia katika maisha. Sasa wewe kwa kuwa ni mtu wa ofisini utaishia kuniletea vifungu vinasemaje huku utekelezaji ni tofauti. Mimi naangalia matendo na sio vifungu vinasemaje, japo kutoka kwenye vifungu ndio tunapoanzia kupima utekelezaji. Mfano mwepesi Rais kapiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote kama huna muwakilishi eneo husika. Je kuna kifungu kinachompa mamlaka ya kuzuia vyama vingine kujijenga na kupata wanachama nchi nzima? Mwengeso toka nje ya box uone uhalisia. Hili tatizo la kukariri vifungu ndio linalokabili nchi yetu, unakuta mtu ni msomi lakini hana ubunifu hata chembe, akiingia ofisini anafanya kazi za daily routine mwaka mzima bila kuweka wazo jipya.
 
Kumbe unabishana mimi nilidhani tunapeana elimu. ..

... Hili tatizo la kukariri vifungu ndio linalokabili nchi yetu, unakuta mtu ni msomi lakini hana ubunifu hata chembe, akiingia ofisini anafanya kazi za daily routine mwaka mzima bila kuweka wazo jipya.
Kubishana ni moja ya majadiliano. Kupeana elimu si kujadiliana.

Kufanya kazi nje ya vifungu, ndiyo msingi wa kufanya kazi kwa mazoea, wewe waita (daily routine). Matokeo yake ndiyo haya ya umaskini katika nchi tajiri.

Utakubaliana na mimi kwamba mikutano ya hadhara hupunguza muda wa kufanya shughuli za maendeleo. Ulimwengu wa sasa kuna njia nyingi za kuwafikia na kuwashawishi watu kujiunga na chama, si cha siasa tu.
 
Ukiona mnapeana elimu bila kujadiliana basi hiyo sio elimu hayo ni mahubiri. Umewahi kuona mkutano wa hadhara watu wakiswagwa kwenda kusikiliza? Kuna mtu amewahi kwenda kuomba msaada serekalini wa kulisha familia yake kisa alienda kwenda mkutano wa hadhara? Hizi live tunazoziona kila siku kwenye TV mbona hatuambiwi kwamba zinazuia watu kufanya kazi, maana tuliambiwa bunge live linazuia watu kufanya kazi. Sababu ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni hila na nongwa, na ni hiyo ninayokuambia katiba kutoa nguvu kubwa kwa rais kiasi kwamba anaweza kufanya maamuzi kwa kutegemea hisia zake. Kwenye mahali taasisi zilizo na nguvu msajili wa vyama vya siasa alipaswa kumuambia rais hapa unakosea kwa kuminya uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake. Msajili angetafuta utaratibu mzuri wa vyama vya siasa kufanya mikutano aidha ya ndani wangalau mara moja kila mwezi siku ya mwisho wa juma (jumamosi au jpili) ili kupata wanachama wapya. Usifumbie macho ukweli hata kama unavunjwa na mkono unaokulisha.

Kwa hii post yako kaka Mwengeso naona unaanza kuishiwa na ile nguvu yako ya ushawishi wa hoja ninayoifahamu, sasa unaanza hoja za nguvu kwa ajili ya kusaka ushindi. Kama ni ushindi mbona nilishakupa?
 
Back
Top Bottom