CHADEMA imeshinda chaguzi kwa nguvu ya umma sio Tume ya Uchaguzi. Tusidanganywe

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
586
1,000
Miaka yote Chadema imeshinda chaguzi kwa kutumia nguvu ya Umma tu sio Tume ya Uchaguzi wala mbeleko nyingine yoyote.

Mbowe na Vijana wake wanataka kuwadanganya Watanzania kwa kutoa visingizio hafifu. Hakuna uchaguzi ambao haujawa na matukio ya vurugu tangu nimeingia kwenye siasa za upinzani. Watu wamefungwa, wameuawa, wamedhalilishwa, wametezwa na kufanyiwa kila lililo baya.

Ukweli ni kuwa

1. chama hakina fedha za kushiriki uchaguzi. Unahitaji zaidi ya 1.6 bilioni kushiriki uchaguzi uliotangazwa na ni fursa kubwa ya kufanya siasa kwa wale wanaolalamikia uminywaji wa demokrasia.

2. Nguvu ya Umma imekufa. Mgawanyo wa fursa za viti Maalum ngazi ya Ubunge na Udiwani, dhuluma katika Chaguzi za ndani , mgawanyo wa kinyonyaji wa ruzuku na tofauti kubwa ya kipato kati ya viongozi wa makao makuu na ngazi za chini vimewavunja moyo Makamanda wengi. Hawako tayari kuumia au kufa kwa ajili ya Chama tena maana wamegundua wanawanufaisha wachache

3. Woga wa viongozi wa Sekretarieti.
Sekretarieti inaongozwa na waoga, wasaka fursa wenye kuangalia Pesa tu. Hawako tayari kurisk maisha yao kwa ajili ya Chama. Matokeo take wanamdanganya Mwenyekiti na kumtia hofu.

4. Kamati kuu Butu.

Kamati kuu ya sasa ni rubber stamp. Akishaamua Mh. Mbowe, John Mrema, Regy wengine wanaitikia tu. Wachache wanaohoji wanatiwa msukosuko na wengine hususan Maprofesa wameamua kukaa kimya maana hawasikilizwi wala kupewa heshima

Wanachama Wabunge na Viongozi wasipochukua hatua Chama kinakufa na wote tutakuwa tumepoteza muda na rasilimali nyingine.
 

Dereck2020

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
369
500
Hakana jina kubwa haka kapumbavu hivyo wahuni wa MACCM wamegoma kukanunua sasa kamebaki kuja humu kufanya uzushi huku kakilipwa buku 7 na chama cha wahuni.

Huyu naye poyoyo mwingine. Naogopa kupata ban lakini unastahili ile lugha ya upande wa pili isiyo na mipaka wala haina cha bubu babu na shangazi mjomba mkwe au watoto ndeziii
Kuna mijituzzzzzz kha
 

Elevat Kapela

JF-Expert Member
Dec 9, 2017
536
1,000
Daaaaaah. Tanzania ni nchi pekee duniani ambapo darasa la saba, kidato cha NNE, kidato cha sita wote ni wachambuzi wa siasa. Huyu naye anachambua siasa za chama ambacho hakifahamu vizuri. Endelea kufanya hivi lkn kumbuka umri unaenda.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,420
2,000
Hakana jina kubwa haka kapumbavu hivyo wahuni wa MACCM wamegoma kukanunua sasa kamebaki kuja humu kufanya uzushi huku kakilipwa buku 7 na chama cha wahuni.

Hivi hili liliposema Lema kapigwa na Jacob halikufungiwa kwa uongo ule? JF siku hizi inawalea sana wazushi kama huyu.
Eti anataka Chadema iendelee kutangazwa ushindi kwa damu kama vile enzi za makaburu?
Tumechoka!
 

chibuga mugeta

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,047
2,000
Benson Mramba WE SI NDIO ULILETA UMBEA ETI BONY KAPIGANA NA LEMA, YOU KWA NN UNA TABIA ZA KINAFIKI HIVI, HUO UMAARUFU UNAOUTAFUTA KINAFIKI HIVI HAUTAKUFIKISHA POPOTE, we ni mnafiki saaaana tena muongo saaana shame on you nakupuuza sana nahc unavuta cha Kilimanjaro
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,065
2,000
Kuna kitu kimoja huwa kinanishangaza sana. Ni kwanini msaliti huwa anakuwa mbaya kwa taasisi aliyoisaliti kuliko wale wabaya wa taasisi ambao hawakuwahi kuwa ndani ya taasisi hiyo? Kwa mfano, msaliti aliyeisaliti dini au dhehebu lake hulinenea mabaya kuliko ambao hawakuwahi kuwa katika dhehebu hilo; sijui kwanini? Kuna siri gani hapa. Vivyo hivyo katika ndoa; vivyo hivyo katika siasa na kwingineko. Hata Lucifer, yule msaliti mkuu, kutwa kucha ni kuhubiri uongo kuhusu habari za Mbinguni. Ni ajabu kwa kweli.

Hebu mabingwa wa saikolojia tusaidieni; ni frustrations? Ni ku-justfy support ya huko alikokimbilia au anakotaka kwenda? Au ni kitu gani hasa? Kwani ukiondoka kimya kimya au hata ukaaga kabisa kuna tabu gani? Msaliti daima kinywani mwake hutoka machukizo!
 

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
8,915
2,000
Hivi poyoyo liliposema Lema kapigwa na Jacob halikufungiwa kwa uongo ule? JF siku hizi inawalea sana wazushi kama huyu.
Eti anataka Chadema iendelee kutangazwa ushindi kwa damu kama vile enzi za makaburu?
Tumechoka!
Angesema lissu awagomea polisi mngemshushia pongezi za kufa mtu ila kaeleza maoni yenye chembe za uhalisia ni poyoyo makarai bwana!
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Ni vizuri ukajijenga kwanza kisiasa na kuwa maarufu ukiwa unawafuasi wengi nyuma yako.
Ni vizuri ukajitahidi kuwa asset ili uwe na impact kwenye jamii ili jamii husika ikufuatilie kila siku.

UKIYAFANYA HAYO HAPO JUU KUNA JAMAA WATAKUFUATA NA KUWEKA UKWASI MEZANI ILI WAFANYE USAJILI, KWA SASA BADO NI MCHEZAJI WA RIDHAA WATAKUTUMIA TU NA KUISHIA KUFA NJAA NDUGU YANGU.
 

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,460
2,000
Benson Mramba Ukisha maliza kuandika upupu wako mwishoni malizia na ushindi kwa mtutu wa bunduki, maana kama si mtutu wa bunduki CCM indesha fariki muda mrefu sana lakini msimu wa uchaguzi utadhani polisi nao wamesimika mgombea wao maana huwa wako bize kweli na mitutu
 

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
586
1,000
Mkuu Benson Mramba , wewe umesita lini kuwa kijana wa Mbowe? Au kwakuwa huna jina kubwa la kutangazwa ukihamia CCM?(JOKING). Hivi, huzioni changamoto katika mfumo wa uchaguzi hapa nchini?
Nguvu ya umma ndio imekuwa silaha duniani kote kukabiliana na changamoto za watawala sio kususa.

Tanzania tumepata Mengi sana kwasababu ya nguvu ya umma ya Chadema.

Mchakato wa Katiba mpya, maboresho ya sheria mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi. Hata waliohamia Chadema walifuata nguvu ya Umma ndio maana hawakuiogopa serikali
 

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
586
1,000
Hivi poyoyo liliposema Lema kapigwa na Jacob halikufungiwa kwa uongo ule? JF siku hizi inawalea sana wazushi kama huyu.
Eti anataka Chadema iendelee kutangazwa ushindi kwa damu kama vile enzi za makaburu?
Tumechoka!
Ilikuwa ni tetesi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom