Niseme tu kuwa hoja zako zinajikita katika upinzani kupata mwanya/uwanja mpana wa kutangaza sera zake. Nakubaliana na wewe kwa hilo. Ni mapungufu katika dhana pana ya demokrasia....
...Sababu ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni hila na nongwa, na ni hiyo ninayokuambia katiba kutoa nguvu kubwa kwa rais kiasi kwamba anaweza kufanya maamuzi kwa kutegemea hisia zake. Kwenye mahali taasisi zilizo na nguvu msajili wa vyama vya siasa alipaswa kumuambia rais hapa unakosea kwa kuminya uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake. ...
Niseme tu kuwa hoja zako zinajikita katika upinzani kupata mwanya/uwanja mpana wa kutangaza sera zake. Nakubaliana na wewe kwa hilo. Ni mapungufu katika dhana pana ya demokrasia.
Hata vile, uwanja finyu (mitandao ya kijamii na vyombo vya habari) walio nao upinzani, na wafuasi wao, hata humu JF, hawautumii kunadi na kuelezea sera mbadala zenye tija kwa maendeleo ya nchi. Isipokuwa hutumia mianya hiyo kukebehi, kutukana, kulaumu nk Rais Magufuli na Serikali yake. Mfano mzuri nivwa hivi karibuni kwenye kampeni za uchaguzi wa marudio Kata 43, ambapo kampeni za upinzani hazikulenga kuleta mabadiliko kwenye kata hizo, dhidi ya Serikali. Walitumia muda mwingi kuilaumu Serikali. Kuna ushahidi wa kutisha kuthibitisha hilo.
Kama kweli upinzani una nia ya dhati ya kutawala Tanzania na kuiongoza kwenye mabadiliko chanya ya maendeleo, hakuna sababu ya kulumbana na Serikali kwa maneno ya kejeli na lawama, ilakutekeleza kwa vitendo sera na ilani yao ya uchaguzi katika majimbo wanayoongoza.
BINADAMU HUJIFUNZA KWA MIFANO
JE, hiyo nafasi finyu ya kujinadi inatumika kwa faida au ndiyo hiyo ya kufitinisha wananchi na Serikali kama mataji wa kisiasa!... Kuuza sera ni kazi ya chama, hata mimi hili nimekuwa nikiwataka wapinzani wakipata nafasi hata ndogo waonyeshe kipi wanaweza kuwafanyia wananchi kimaendeleo badala ya kujikita kwenye siasa za madaraka tu. Huu ni udhaifu wa wazi wa wapinzani, ila kupitia mijadala ya aina hii watarekebishika. ...
... wananchi ndio waamuzi na sio [CLOR=RED]ukatili na unyama huku ukiratibiwa na vyombo vya dola[/COLOR]. Kibaya zaidi ni uporaji wa ushindi kwa washindi halali.
... Kwenye halmashauri wanazoongoza wapinzani kuna ubunifu unaoonekana japo wanakutana na wakati mgumu kutokana na aina ya siasa zetu kutompa mpinzani wako nafasi ya kung'aa. ...