CHADEMA imejiua yenyewe haijauawa na CCM

Amakweli nime ipa salute idara nyeti ya cdm yaani kitengo kwa kuwafanya wana wa Lumumba kuipa promo cdm

Jua halizimwi kwa kufumba Macho. KILA anaempinga Lowassa anaitwa Ccm na kila anaemsapoti Dr.Slaa leo unamwita Team Lumumba, tatizo lipo na lazima lisemwe. Usijifanye ni Mjuzi sana wa Siasa. Mara Slaa yupo Mikoani kwenye Kura za Maoni mara yupo Likizo n.k Uongo unasambaa haraka lakini pia hufifia haraka sana. Leo wale walokuwa wanamuona Slaa ni Mkombozi ndo wanamwita Mroho wa Madaraka, anatawaliwa na Kimada, mara anatumiwa na RC, yote yanawezekana kwa kuwa mnapenda sana watu na kuwaamini mpaka mmewakodisha wafikiri na kuamua kwa niaba yenu ndo mana hamuamini kama nao wanaweza kakosea kuamua
 
Hapa naongelea sononi iliyosababishwa na Mbowe na kamati yake kumuuzia chama Lowassa. Jua kuwa wananchi wengi wanaumia na kushangazwa

Unashindwa kwenda kuondoa sonono kwa ndugai anaye watandika wanachama wenzake unakuja cdm?mtu wa ajabu sana gambaz
 
Kwa hiyo kunijua kwako kunasaidiaje kuongeza pato la taifa? Na utaendelea kuota hivyohivyo kunijua ila kama unashida ya kunijua sio kitu ni pm tu.

Wewe uwanja huu haukufai maana wewe ni team act
 
Ni bahati mbaya sana kuwa a principled CHADEMA imekufa kwa tamaa ya madaraka ya viongozi wa juu. CHADEMA kilikuwa chama kwenye mioyo ya watu wengi. Pamoja na juhudi za CCM kujaribu kukiua CHADEMA haikuwezekana kwa kuwa watu walikiamini kutoka moyoni. Lakini sasa viongozi wa CHADEMA wao wenyewe wamekiua CHADEMA kwa mikono yao wao wenyewe kama mwanamke mpumbavuu anayevunja nyumba kwa mikono yake mwenyewe.

Imani kwa CHADEMA imetoweka kabisa mioyoni mwa watu wengi na hiki ndicho kifo chake. Watu walikiamini CHADEMA kama chama cha kuwakomboawananchi dhidi ya ufisadi kwa nadharia na kwa vitendo. Sasa CHADEMA wamepoteza identity yao kabisa na watu wamepoteza imani yote kwa CHADEMA kwa sababu ya tamaa ya kuingia ikulu kwa gharama yoyote bila kujali misingi ya chama.

Wakulaumiwa kwa kifo cha CHDEMA ni ni viongozi wa CHADEMA wenyewe wala siyo CCM. Poor Mbowe na kamati kuu yako. Tumetoa maonyo mengi mno kwa CHADEMA kujitenga na Lowassa lakini viongozi wakaamua kuweka pamba masikioni. Kukuana kukubalika kwa CHADEMA kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na unseen heroes ambao walitumia muda na raslimali zao zingine kuitetea CHADEMA bila kutumwa na yeyeto yule. Kwa sasa hakuna namna ya kuitetea CHADEMA wamejimaliza wenyewe.

Sasa kama kimekufa si ndio ufurahi ..ila tambua oktober 25 wananch watafanya maamuz aidha kuwajaribu cdm unaosema wamekufa au kuwarudisha nyie maccm
 
Subiri uone mafuriko ya chama kilichokufa kuanzia j5 ....kama kimekufa ccm c mnatakiwa mfurahi sasa mnajifanya washauri wakubwa .....ccm inaelekea kibla uchaguzi huu ...
Subiri ngoma ianze, ndo kwanza tune imeanza, si umemsikia Nape.
Kwa mtaji wenu wa makapi yaliyokatwa , jiandae kuendeshwa puta.
 
Mpende msipende mtakuwa wapinzani maana moto wa cdm ni salamu tosha kwenu kujiandalia pahala
Huo moto unaosema ni ule wa principled CHADEMA, siyo wa CHADEMA iliyouzwa kwa Lowassa. Baadaye utaelewa mbele ya safari.
 
Kama unapenda kuelewa utajibu nilichokuuliza vingenevyo utajua mbele ya safari my hoja yangu.

Nimeeleza mara kueleza,kuwa wewe huna cha kuieleza cdm,endelea kutumikia ccm na ni haki yako lkn habari ya kutudanganya hapa umenoa,
 
Ccm kumkata lowassa ni hasara mara nyingi zaidi ya madhara ya cdm kumpokea lowassa!
Ukicancell effect in both sides utakuta bado cdm kuna chanya wakati ccm zero!
 
Siasa za mwaka huu.ccm inasaidia kuutangaza ukawa na Lowasa.kila kona lowasa.mpaka darasa la kwanza wanamuongelea lowasa.
 
Watanzania wanataka mabadiliko na inapopatikana njia ya njia ya kufikia kiu ya mabadiliko ni vyema ikatumika
 
Kuidondosha CCM ni mchakato na lazima uwe mchakato safi siyo wa kukumbatia mafisadi na hivyo kuua msingi wa CHADEMA kupendwa na watu.

Mkuu cdm haikuhusu,wewe tumia nguvu na akili yako kuisaidia ccm,kasaidie majimboni huko wanatoana roho
 
Ccm kumkata lowassa ni hasara mara nyingi zaidi ya madhara ya cdm kumpokea lowassa!
Ukicancell effect in both sides utakuta bado cdm kuna chanya wakati ccm zero!
Mkuu chama kinajengwa na principles. Hao wanaomfuata Lowassa unajua wanafuata maadili kama ilivyokuwa kwa principled CHADEMA?
 
Back
Top Bottom