Prince Tumbo
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 910
- 247
Chama Cha Deokrasia na Maendeleo kwa sasa tayari kimeifilisi CCM kisiasa, haina hoja yoyote madhubuti na kilichobakia ni kudhibiti na kupigana kuisambaratisha CHADEMA. Kauli za viongozi wake kama wasira, Nape na Mwigulu zinaongozwa na UOGA NA HOFU, na zimebeba mikakati ya kitoto ambayo baadhi imeshaonekana tayari.
Kukubalika kwa CHEDEMA kwa wananchi ndiko kumewafadhaisha hawa watu kwa sasa ku-act kama watoto, kuonekana wakiimba CHADEMA....CHADEMA.....CHADEMA.....kila waliko na mikutano. Hii ni ishara mbaya kwa CCM ambacho kinatakiwa kushughulika na changamoto zinazowakabili wananchi. Hii ina maana kwamba CCM imegeuza sera zake bila kujua na kuifanya CHADEMA ndio changamoto yake na kusahau kuwa kinapaswa kuwaambia wananchi kitamalizaje matatizo yao.
CHADEMA wameifilisi CCM, na haina namna bali kuendelea na propaganda ambazo nazo tayari wananchi tumeshazigundua. Bado kitambo, wako tayari kufanya mambo mabaya zaidi na hatutaamini macho na masikio yetu....