CHADEMA ilipoongoza Halmashauri Hakukuwa na Mitandao ya wizi

CHADEMA ilipoongoza Halmashauri Hakukuwa na Mitandao ya wizi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,586
Reaction score
287,272
Hili kila mtu anapaswa kulielewa , na kwa kweli Chadema inapaswa kupongezwa kwa hili .

Nadhani hata Vipofu wameanza kuona Chama Cha Wezi ni kipi .

Screenshot_2023-08-27-16-20-08-1.jpg
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Ukweli ni Huu : Chadema ilipoongoza Halmashauri Hakukuwa na Mitandao ya wizi,ispokuwa tumbo zao zilishiba na kunenepeana kwa vitambi.​

Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
na msisahau yakipatikana mafanikio atawasanifu kuwa alipokaribisha wawekezaji wa Bandari alipata Upinzani mkubwa hadi kwny Taasisi za Kiimani baada ya kushawishiwa na makundi maslahi yaliyokuwa yanafaidika na mfumo mbovu wa uendeshaji , the future is uncertain anaweza akajuta au wakosoaji wa Leo ndio wakajuta

mf waliosusia mchakato wa Katiba mpya kumnyima legacy ya Katiba mpya Jakaya sasa hivi wako busy kwny vikao vunavyoongozwa na Kinana na Lipumba walau matokeo ya Rais yapingwe Mahakamani na Tume huru iwepo wakati yote hayo yalikuwepo kwny Katiba mpya waliyoikataa na kususa
 
Kwa kitu kibovu kama mkataba wa bandari tutegemee majuto kama Mkapa alivyojuta kwenye ubinafsishaji
 
Hawa washauri waandae mkataba wanaodhani ungefaa ili tuusome na tuishauri Serikali Ione tulichokikusudia bila hivyo kila siku kila mtu atakuja na lake na hatutafikia muafaka.

Chanzo cha mkataba mbovu ni watu wetu inawezekana ni kutokana na uwezo wao katika mambo ya mikataba au mashinikizo lakini vinginevyo mambo ya biashara hayajawahi kuwa fair hata siku moja ndiyo maana unanunua kwa bei rahisi na unauza kwa bei kubwa au unapo ajiri au kupata kibarua lazima utahakikisha unamlipa kidogo kulingana na atakavyo zubaa vivyohivyo kwenye mkataba wa DP WORLD lazima walipokaa kujadili waliangalia fursa ya akizubaa tunampiga.

Tatizo hili limetoa fursa kwa wale mahasimu wa Serikali kupata agenda na watajificha kwenye kichaka cha Mkataba wakati ukweli ni kwamba katika maeneo ya mikataba nchi yetu imeingia mikataba mingi ambayo Ina dosari kubwa kubwa nyingine ni kutokana na wawakilishi wetu kupewa rushwa na mingine ni uwezo mdogo katika masuala ya mikataba.

Kosa kubwa lilianza pale ambapo Bunge lilipoamua kujadili kisanii mkataba huu au vyovyote utakavyouita.

Kosa la Pili ni kutekwa na wanasiasa waliokuwa na kiu yakutafuta agenda ya kutokea.

Kosa la tatu watu wa Dini kuingia kichwakichwa kuunga mkono hoja iliyobeba agenda za wanasiasa na kuitakasa.

Kwa vyovyote vile kuna makundi yameibuka kunawanao pinga,wanaounga mkono hoja na wasiofungamana na upande wowote na mbaya zaidi wote hawataki kugeuka jiwe la chumvi.

Nionavyo Mimi kutoboa ni ngumu na hili ni tatizo linalotukumba waafrika kwa karne nyingi kila Siku ni kupingana na kupigana kitendo kinacho haribu ustawi wa wananchi wasio na hatia.

Hatuwezi wote tukawa CCM au CHADEMA wala hatuwezi watu wote tukawa Waislam au Wakristo nk ni lazima tukubali kuto kukubaliana.

Mungu amewapa kipaji baadhi ya watu kuwa na uwezo wa kuumba maneno na kushawishi wengine kuamini kila wanachokiongea hali inayopelekea watu hao kuwa radical na wanaweza kuleta athari kubwa katika jamii na kudunisha maendeleo ya nchi.

Nchi zote zenye migogoro zinaishia kuwatesa watu wasio na hatia.

Nini kifanyike? Inawezekana mkataba huu siyo mbaya kiivyo au ni mbaya sana basi liundwe jopo la wabobevu wa mambo ya mikataba wasaidie kuweka njia nzuri na kama hakuna wabobevu basi wakodiwe kutoka mataifa yaliyoendelea ili wasawazishe kwenye kasoro zenye athari kwa nchi kama zipo.

Ni wakati muafaka pia kuwa na katiba mpya ili mambo yetu muhimu yawe ndani ya sheria mama.
 
Back
Top Bottom