johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,963
- 141,963
Wale wahenga wenzangu tulioishi wakati wa mfumo wa chama kimoja enzi za mwalimu Nyerere mtanielewa kirahisi.
Kwa sasa Chadema ndio chama cha upinzani kilichobaki chenye nguvu kidogo kiasi cha kuwapa promo baadhi ya viongozi wa CCM. Lakini nawahakikishieni kuwa bila upinzani hakuna umaarufu wa individuals ndani ya CCM. Kwa mfano kwa sasa tumeshasahau kama CCM ina Naibu katibu mkuu aliyemrithi Dr Mwigulu. Vivyo hivyo 2021 tutawasahau kabisa Katibu mkuu na mwenezi wa chama kwa kuwa chama kitakuwa kimeshika hatamu.
Chama kikishika hatamu watu maarufu wanabaki kuwa ni viongozi watendaji serikalini kama ilivyokuwa kwa Sokoine na Salim A. Salim.
Hapa tunakumbushana tu maana kuna vijana wadogo humu Jf. Bila kuwa na vyama imara vya upinzani hata umuhimu wa chama tawala hupungua serikali ndio inakuwa kila kitu.
Maendeleo hayana vyama!