CHADEMA ijihadhari na goli la mkono kwenye uchaguzi wa ubunge wa Kinondoni na Siha

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Ikiwa imebaki wiki moja kamili hadi kufikia ile tarehe 17 ya mwezi huu uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kinondoni na Siha kufanyika, ni lazima chama cha upinzani cha Chadema kiwe makini sana na mbinu zinazoweza kufanywa na CCM katika kutaka "kuwapora" ushindi wao unaoelekea wa dhahiri wa ubunge katika majimbo hayo mawili.

Maeneo ambayo CCM wanaweza yawekea mikakati ya kuweka figisu figisu ni haya yafuatayo.

1. Mawakala wa Chama cha Chadema ni lazima wahakikiwe mapema na kuhakikishwa kuwa ni "wafia chama" na majina yao kupelekwa mapema ili zisiwepo bila za kutaka kuwaemgua.

2. Chadema ihakikishe kuwa vituo vya kupigia kura haviwi "siri" ya Tume ya uchaguzi, ili viwe na uwazi ili kuepusha wapiga kura mamluki kutoka maeneo mengine nje ya Kinondoni na Siha

3. Katika siku hizi za mwisho za kampeni timu ya kampeni ya Chadema ijikite katika kuelezea itawafanyia nini wakazi wa Kinondoni iwapo itaaminiwa na wakazi hao kwa kupewa kura na ijiepushe na lugha za "vijembe" kwa wapinzani wake, kwa kuwa tunafahamu kuwa Jeshi la Polisi liko upande wa CCM na ndiyo maana limeamua kuirekodi mikutano yote ya kampeni wanayoifanya Chadema, ili wapate sababu za "kumdesqualify' mgombea wa Chadema katika kipindi hiki cha lala salama

Mkishakiwa makini na hayo niliyowatip, basi ni dhahiri ushindi ni wenu na wao CCM ambao ni mabingwa wa kuwanunua wapinzani, mchezo huo utafikia MWISHO na hawatarudia tena kuwanunua wapinzani.
 
Ikiwa imebaki wiki moja kamili hadi kufikia ile tarehe 17 ya mwezi huu uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kinondoni na Siha kufanyika, ni lazima chama cha upinzani cha Chadema kiwe makini sana na mbinu zinazoweza kufanywa na CCM katika kutaka "kuwapora" ushindi wao unaoelekea wa dhahiri wa ubunge katika majimbo hayo mawili.

Maeneo ambayo CCM wanaweza yawekea mikakati ya kuweka figisu figisu ni haya yafuatayo.

1. Mawakala wa Chama cha Chadema ni lazima wahakikiwe mapema na kuhakikishwa kuwa ni "wafia chama" na majina yao kupelekwa mapema ili zisiwepo bila za kutaka kuwaemgua.

2. Katika siku hizi za mwisho za kampeni timu ya kampeni ya Chadema ijikite katika kuelezea itawafanyia nini wakazi wa Kinondoni iwapo itaaminiwa na wakazi hao kwa kupewa kura na ijiepushe na lugha za "vijembe" kwa wapinzani wake, kwa kuwa tunafahamu kuwa Jeshi la Polisi liko upande wa CCM na ndiyo maana limeamua kuirekodi mikutano yote ya kampeni wanayoifanya Chadema, ili wapate sababu za "kumdesqualify' mgombea wa Chadema katika kipindi hiki cha lala salama

Mkishakiwa makini na hayo niliyowatip, basi ni dhahiri ushindi ni wenu na wao CCM ambao ni mabingwa wa kuwanunua wapinzani, mchezo huo utafikia MWISHO na hawatarudia tena kuwanunua wapinzani.
Kampeni meneja nadhani ndio wajibu wake na timu yake. Ndio maana lazima hivi vyama viwe na kitengo cha mitandao kupata some useful information kama hizi. Umetoa tahadhali kubwa sana. Wataiona na kuifanyia kazi?
 
Kwa kuwa naamini Chadema wamewabana vilivyo vyama "ndugu" vya CCM na CUF Lipumba, kiasi ambacho wanatafuta pa kutokea, lakini hawapaoni!
 
Acheni blabla mmeanza kutafuta visingizio ili mtakapo shindwa muwe na visingizio kibao, kinondoni hamtapata labda nguvu mzipeleke siha
 
Mtoa mada ni kama amenusa kushindwa
Ni vigumu sana chadema kushinda kinondoni na siha labda wajaribu 2020
Safari hii visingizio hakuna kwa sababu mlitangaza kususia dakika za mwisho mkakurupuka
 
Nachofahamu ni kuwa Bashite na huyo Ali Hapi sijui ni moja ya wanakamati ya kununua wapinzani. Maana yake lazima wafanye chochote kile ili wamfurahishe bosi wao, hawatapenda waombe msamaha kama yule wa Mbeya. Hivyo CDM hapo Kinondoni jiandaeni kila idara!
 
Nasikia Salumu anataka kujitoa kuepusha aibu ya mwaka
Wewe Umeongea vice versa..........

Mwenye njia ya kujitoa haswa haswa ni Maulidi Mtulia baada ya kuona kwenye uchaguzi huu, Chadema wamejipanga katika kila idara kuhakikisha hakuna goli la mkono litakalofungwa na CCM
 
Mtoa mada ni kama amenusa kushindwa
Ni vigumu sana chadema kushinda kinondoni na siha labda wajaribu 2020
Safari hii visingizio hakuna kwa sababu mlitangaza kususia dakika za mwisho mkakurupuka
Nikulize? Mtulia na morel wamesahau nini bungeni?
 
CDM mbona ilishakufa kitambo tu
CCM ndiyo ilishakufa siku nyingi sana.....

Kinachowabeba hao CCM kwa sasa ni Tume ya Uchaguzi na Polisi

Hivyo vyombo vya dola vikiamua kufanya kazi yao kwa weledi, mbona CCM ni wepesi zaidi ya karatasi ya tissue
 
Back
Top Bottom