Chadema huu ni wakati wa mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema huu ni wakati wa mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Jul 5, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Natoa rai kwa uongozi wa Chadema wakae chini na kuwafunda wabunge wao kwani inaonekana wamekosa uelekeo wawapo mjengoni.

  Tumefuatilia kwa karibu tukagundua wabunge wao wanaongoza kwa kuanzisha mijadala ambayo inasababisha wananchi waanze kususia kusilikiza vikao vya bunge. Wengi wao wamegeuza bunge kuwa ni kijiwe cha kutoa porojo. Chondechonde wabunge wa Chadema kumbukeni mpo mjengoni kuwakilisha mawazo ya wananchi na wala sio kuhamasisha uvunjwaji wa sheria mkiwa bungeni.

  Mbunge wangu John Mnyika kumbuka una deni kubwa la kutekeleza ahadi ulizozitoa manzese, sinza, ubungo, bonyokwa, kimara; punguza kupoteza muda kwa kuomba mwongozo BADALA YA kuwakilisha mawazo ya wanaUBUNGO.

  Tafadhali CHADEMA badilikeni!!!
   
 2. G

  Gramsa Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wee mpuuzi tu. Huonikama ndugu yenu Mchemba ndio anaanzisha malumbano yasiyo na msingi. Wewe ndio unaanza kubwabwaja janvini na upuuzi wako.
   
 3. e

  ebeka New Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magamba utayajua tu. ulitaka mnyika aunge mkono asiliamia mia kwa mia?
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Watafanyaje sasa wakati wamegundua huo ndiyo mtaji wa umaarufu wao?
   
 5. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Mimi kwa maoni yangu nafikiri CHADEMA au labda baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawaelewi maana siasa!
  Nitaelezea kwa nini, kwa mfano Mbunge wa CHADEMA anapoweka bayana msimamo wake kwamba anapinga muungano wetu jinsi ulivyo, kwangu mimi kosa kubwa sana kisiasa hata kama ni kweli una matatizo lkn kujitokeza na kuupinga moja kwa moja kunaweza kuwagharimu sana CHADEMA hapo baadae kwenye Uchaguzi, kwa maana CCM wanaweza kutumia hilo na kuwaambia wananchi kwamba CHADEMA wanataka kuvunja muungano!

  Mimi nilikuwa naona kwamba hata kama wanataka kuubadilisha muungano wetu jinsi ulivyo ni bora wangeweka hiyo sera kapuni na kujishughulisha na mambo mengine yanayo wagusa wanachi moja kwa moja, halafu wakitokea wakashinda uchaguzi ndipo wanapoweza kuanza kuleta hayo mambo ya Muungano na ikiwezekana kubadilisha!

  Najua wengi mnaweza mkapinga hili lkn nawahakikishia CHADEMA wakiendelea hivi itawagharimu sana, hata sera ya Majimbo hawapaswi kuiongelea na kuanza kuikampenia, kwa ni ni rahisi sana kwa CCM kuweza kuupotosha umma na kuutisha na hatimaye kushawishi umma kwamba CHADEMA wan nia ya kubadilisha mfumo wetu wote wa maisha na kuleta mfumo mpya tusioujua, na kama kawaida ya binadamu anaogopa mabadiliko hivyo wananchi wengi wanaweza kuungana na CCM kuwapinga!
  Mimi naona ni bora haya mambo ya muungano na majimbo wasingeyatoa sasa hivi kwa wananchi bali wangesubiri mpaka washinde ndipo waanza kuyafanyia kazi! Maoni yangu
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe kweli ni kijakazi wa Chama Cha Mabwepande
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​du sasa ndio umeongea nini unaongea kama komba au lusinde
   
 8. D

  DoPe Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana m4c wanachokipigania ni wananchi wa tanzania kuelezwa ilikuwa kuwa aje mpaka tukaungana na sio mengine. Unajua watanzania wengi wao wanachojua ni kuchanganywa kwa udongo basi,,; kumbe nyuma ya pazia kuna mengi..(
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kweli we mleta maada unaonekana hauna Mungu kabisa, kwani nani kakuambia anataka muungano? Muungano kwa faida ya nani wakati sasa hivi majority of people wanataka kusikia maisha bora 2 and not otherwise, pia kumbuka kwamba hiki ni kizazi kingine ambacho kinatamani kuona mabadiliko na sio propaganda za magamba wenzio na ninakuhakikishia kuwa Muungano HAUTAKIWI tena kwani watu tumechoka kwa lawama za wazenji.
   
 10. M

  Mkojo Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM wakweli, wewe umezoea kudaganywa! basi bakia hivyo hivyo na hakikisha hata watoto wako wadanganye tu ili wawe kama wewe hapo baadae
   
 11. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Weka CV yako kwanza ndo tukusikilize pumba zako
   
 12. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,205
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni bora uweke sera zako wazi bila kificho kuliko kuficha mambo baadae ubadilishe sera hiyo ni mbaya sana hayo mambo ya kuficha vitu hayana msingi wowote kwa maendeleo ya taifa hili.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pengine huelewi kwa nini Chadema wanapinga muungano uliopo na wanataka nini.. Hoja ya Chadema ni kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika hivyo wanachokitaka ni kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo sii kwamba wanapinga muungano isipokuwa wanapinga muundo wa muungano huu.

  Kama ilikuwa swala la ulinzi bila shaka chini ya Serikali ya Jamhuri Mapinduzi yatalindwa zaidi na chama chochote kitakacho ingia madarakani badala hili kuwa jukumu la mfumo wa chama kimoja yaani CCM (TANU na ASP). Kama nchi zote zilizofanya muungano na kulinda maslahi ya Kitaifa badala ya kutegemea chama kimoja ama kundi fulani la watu kuwa waasisi na walinzi wa muungano huu. Kizazi hicho kinakwisha na vijana wengi wa leo hawafahamu malengo wala nia ya kuwa na serikali hii na chama kimepokea maombi ya Wazanzibar ambao walizitaka serikali tatu toka uchaguzi wa mwaka 2000 na Chadema haikuwa nyuma kuunga mkono. Kwa nini leo wabadilishe?

  Hivyo basi kama kuna utata ktk kuunda serikali tatu iwekwe wazi, watu wapime, waumize vichwa jinsi gani tunaweza kuuboresha muungano wetu Kikatiba bila kujali chama gani kitakuwa madarakani. Na swala la Majimbo pamoja na kwamba lina utata mkubwa lakini kulingana na WATU yaani sisi wenyewe na viongozi wetu inaonyesha wazi majimbo yaliyokuwa nyuma ktk maendeleo hayataweza kuendelea kamwe chini ya mfumo uliopo..
  Mapendekezo ya Chadema ni kuwepo na serikali za Majimbo kwa kuzingatia hali halisi ilojitokeza. Hili ni pendekezo lao, binafsi yangu ningependelea zaidi kuwa na serikali za mikoa (county) ambazo zitapewa madaraka kamili ya kujiendesha kupitia kodi zao. watakusanya kodi zao na kati ya kodi hizo fungu litakwenda mfuko wa Taifa.

  Mathlan kodi ikiwa asilimia 17, zitaganywa kama ifuatavyo Nane(8) ya mkoa na tisa(9) ya Jamhuri ya Tanzania. Hivyo kila mkoa kwa pato lake la asilimia 8 watapanga mipango yao na bajeti zao kimkoa wakati wakiomba serikali kuu fungu la maendeleo kupitia mchango wao wa asilimia 9 ambazo zitalenga zaidi miundombinu na miradi mikubwa ya Kitaifa kama ujenzi na uimarishaji wa Usafiri TRA, ATC, Umeme (Tanesco, Maji (Dawasco), Mawasiliano na kadhalika. Kutokana na ombi la kuwepo Madaraka mikoani ni ktk kujaribu kuweka jukumu la kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi mikononi mwa wananchi wenyewe kufuatia sera za chama kilichopata ushindi ktk uchaguzi sehemu hiyo, hivyo sera na nguvu ya kodi yao kuwa sababu ya maendeleo yao na kadhalika badala ya kuendelea kuitegemea serikali kuu ambayo inaendesha miradi yake kisiasa zaidi.

  Ni imani yangu hakuna mikoa hafifu isipokua ukiritimba na urasimu ndio umepoteza umuhimu wa uwekezaji ktk mikoa kama ya Singida, Rukwa, Songea n.k.kila mkoa una utajiri wake, lakini tumeshindwa kuiwezesha isipokuwa ile yenye utajiri wa haraka haraka kwa manufaa ya viongozi wetu. Mradi wa Mtwara utachukuliwa kuiboresha Dar ama ni mradi wa kiongozi @10%..Mfano mwingine, Singida leo hii ilitakiwa kuzalisha Umeme wa upepo au miali ya jua, kuboresha kilimo cha mafuta ya alizeti na kadhalika lakini hakuna hata mpango huo kwa sababu tunategemea serikali kuu.

  Tazama Mgogoro kama huu wa Madaktari haukutakiwa kuwa wa nchi nzima hata kidogo. Kama majimbo yanaweza kukusanya fedha vizuri sioni sababu ya sehemu kama Shinyanga, Mtwara na Mara kuwa nyuma ktk maendeleo wakati wao ndio wanachangiaji wakubwa wa pato la Taifa iwe ktk madini au ukulima. Sioni sababu ya Tanzania yetu kuwa na Hopitali moja tu kubwa nchi nzima (MNH) ilojengwa toka enzi za Nyerere..Hivyo swala la majimbo linaweza kuwa suluhisho ikiwa tuta jihadhari na negatives zake maana kupanga ni kuamua..
   
 14. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Tena cdm wakisema waziwazi kuwa watauvunja muungano baada ya kupata madaraka watapata kura nyingi sana.kwa sababu watz wengi hawautaki muungano kwa sababu hauna faida kwao na kura nyingi zitatoka zenji ambao wamepinga waziwazi kuwa hawautaki. usione watanganyika wamekaa kimya ukadhani kuwa wanaupenda muungano la hasha ni kwa vile tu hawana hulka ya kusema hovyohovyo.usitishwe na viongozi wa ccm wanao utetea huo muungano ni kwa manufaa yao binafsi sana sana ya kichama.muungano ukifa ccm haipo.kwani kipande kimoja ni tanganyika (tanu) na kingine znz (asp) na ndio wenye sera ya muungano.cdm hakuna sera ya muungano.
   
 15. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  jf.gif jamiiforus
   

  Attached Files:

  • jf.gif
   jf.gif
   File size:
   61.9 KB
   Views:
   1,578
 16. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nilijua mtanishambulia tuu kwa maneno, lakini nilichotaka kusema ni kwamba, Siasa sio fair game na maisha ni hivyo hivyo pia, kuna mambo katika siasa ni lazima upime kwanza uzito wake na kufikiria kwanza kabla ya kuongea, katika kila nchi kuna vitu sensitive sana, na wewe unapokuwa mwanasiasa ni lazima ujue ni kitu gani hicho? kwa mfano ukabila au udini kwa nchi yetu ni moja ya vitu sensitive na ni kwanini ni sensitive hata mimi sijui lakini ndiyo mazingira tuliyolelewa, kwa hiyo unapoanza kukampenia kwa mfano majimbo hata kama uko sawa rahisi kwa CCM kuweza kugeuza hiyo sera ya majimbo na kuwaambia watz kwamba CHADEMA wanataka kuwagawa wananchi na amini msiamini watanzania wengi wataamini CCM wanaweza hata kuanza kuonyesha cinema za vita za Kenya au Nigeria au Burundi kutumia kuwatisha wananchi na matokeo yake CHADEMA kupoteza kura nyingi.

  Pili kuhusu muungano nao pia hivyo hivyo ni sensitive ikumbukwe kwamba muungano uliletwa na Nyerere sasa unapoanza kukampeni kwa kuupinga kama mwanasiasa ina maana unakosoana na Nyerere na hapa kwetu ukianza vita na mambo ya Nyerere hata kama uko right kiasi gani, huwezi shinda kwa hiyo CCM wanaweza kutumia huo mwanya na kuwaeleza wananchi kuwa wewe ni Anti Nyerere na matokeo ya hiyo propaganda sijui kama utayapenda!
   
 17. l

  leloson Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu kwel lusinde aka komba! kwaiyo unaona kuwadanganya wananchi ndio approach nzuri! that z a poor perspective. CHADEMA ukweli ni principo whether unaukataa au vinginevyo' AMKA WW.
   
 18. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hee....kwani wananchi wakijua kwamba cdm wakiingia madarakani watavunja muungano itakuwa na madhara gani....hakuna mtz hata wewe anayeona faida yoyote ya muungano zaidi ya wazenji kuinyonya bara.....kweli wewe nakuona akili yako ndogo sn...muungano unafaida gani km mbara haruhusiwi kuwekeza zenji zaidi wabara wanachomewa makanisa na kuchomewa bar zao?...leta hoja za maana kidogo
   
 19. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ni vigumu sana kuelimishwa ukaelimika, ubongo wako utakuwa umejaa kamasi. Watu wamejitahidi kukuelimisha lakini bado unashikilia misimamo ya kijinga tu.
   
 20. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [h=6]Jumuiya Ya Uamsho na Mihadhara Ya Kiislamu Zanzibar

  [/h][h=6] TUME YA KUKUSANYA MAONI HUKO - MUYUNI LEO ASUBUHI.

  Taarifa za maoni kutoka Muyuni ambako Tume ilikuweko asubuhi leo: Waliotoa maoni wote ni 109, katika hao walozungumza waliotaka Muungano wa Mkataba wa Serikali mbili huru zenye mamlaka kamili (Zanzibar na Tanganyika) ni 47, waliotaka Serikali tatu ni sifuri, na waliotaka mfumo wa sasa uendelee ni 16. Waliotoa maoni kwa maandishi na kutaka mfumo wa sasa uendelee ni 25 na waliotaka Muungano wa Mkataba ni 20.
  [/h]
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...