Mafilifili kuwa mkweli; halafu ni vema ukashare na wenzako kile ambacho ndani ya nafsi yako unaona ni sahihi, ukweli na inakupa amani.
Kama kweli unafuatilia mjadala wa bunge bila kuwa na ushabiki wowote wa kichama utagundua kuwa wabunge wa CHADEMA daima hujikuta wakipandwa jazba kwa sababu kuu mbili. 1. KUONEWA NA KITI CHA SPIKA/ MWENYEKITI au 2. KUPANDISHWA HASIRA NA MATENDO NA KAULI ZA WABUNGE WA CCM.
Tangu kuanza kazi kwa bunge hili kinachoonekana ni mkakati wa makusudi wa kuhakikisha hoja za msingi zinazotolewa na wabunge wa upinzani hasa CHADEMA na NCCR (ingawa kwa NCCR mara zote waathirika ni Kafulila, Machali na Mkosamali) zinapingwa tu. Rejea tangu mkutano wa kwanza wakati wa kuunda kambi ya upinzania Anne Makinda bila haya wa utu akajifanya kuleta tafsiri mpya ya kambi ya upinzani. Kumbuka ndicho kipindi msemo wa "meseji senti" na kuitana "mdogo wangu, dada yangu, nk" ulipoingia bungeni lakini walipoutumia wa CCM kiwemo Mkuchika, Lukuvi, nk Spika hakuona kama kanuni zilikiukwa!
Ilipokuja mswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ndio balaa. CHADEMA na wengine wakizungumzia mtu badala ya suala kabla hata msemaji hajamaliza sentensi Spika/ mwenyekiti humwambia kaa chini! au leta ushahidi. Lakini CCM walipomaliza siku 3 wakimzungumzia Lissu hawakukemewa!
Job Lusinde mashatumia maneno ya kuudhi na yenye uchochezi mara nyingi kama "funga milango tupigane," wabunge wapimwe akili, Manyanya anakuja na kauli ya " Ulimboka ni Hitler", Sitta naye akaja na " wapinzani ni wanafiki, kazi yao unafiki nafiki tu!, Hawa wote na wengine hawajawahi kupewa onyo na spika wala kuambiwa wafute kauli zao. Kwa maana hiyo kauli hizi zipo katika kumbukumbu za bunge.
Juzi hapa Mnyika kusema "tumefika hapa kutoka na udhaifu wa Rais..." akafukuzwa nje kama mhalifu.
Angalia mgogoro wa madaktari unavyojadiliwa. Akisimama wa CHADEMA, NCCR, anaambiwa "unawashwa! unataka umaarufu! huruhusiwi kujadili suala lillilo mahakamani" Lakini Manyanya, Nchemba na wengine wa CCM akiwemo PM wakizungumzia ni OK.
Mafilifili, nimekusihi uwe mkweli kwa nafsi yako. CHADEMA wamefikishwa hapo kutokana na kuonyeshwa dharau ya wazi kuanzia kwa kiti hadi kwa wabunge wa CCM na mawaziri wa serikali. CHADEMA kwa kuona kuwa hawatendewi haki na aliyepaswa kusimamia na kulinda haki yao (Spika) ama anajifanya haoni na mara nyingine ameeshiriki kuwakandamiza wafanye nini???
EJL