Mimi kwa maoni yangu nafikiri CHADEMA au labda baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawaelewi maana siasa!
Nitaelezea kwa nini, kwa mfano Mbunge wa CHADEMA anapoweka bayana msimamo wake kwamba anapinga muungano wetu jinsi ulivyo, kwangu mimi kosa kubwa sana kisiasa hata kama ni kweli una matatizo lkn kujitokeza na kuupinga moja kwa moja kunaweza kuwagharimu sana CHADEMA hapo baadae kwenye Uchaguzi, kwa maana CCM wanaweza kutumia hilo na kuwaambia wananchi kwamba CHADEMA wanataka kuvunja muungano!
Mimi nilikuwa naona kwamba hata kama wanataka kuubadilisha muungano wetu jinsi ulivyo ni bora wangeweka hiyo sera kapuni na kujishughulisha na mambo mengine yanayo wagusa wanachi moja kwa moja, halafu wakitokea wakashinda uchaguzi ndipo wanapoweza kuanza kuleta hayo mambo ya Muungano na ikiwezekana kubadilisha!
Najua wengi mnaweza mkapinga hili lkn nawahakikishia CHADEMA wakiendelea hivi itawagharimu sana, hata sera ya Majimbo hawapaswi kuiongelea na kuanza kuikampenia, kwa ni ni rahisi sana kwa CCM kuweza kuupotosha umma na kuutisha na hatimaye kushawishi umma kwamba CHADEMA wan nia ya kubadilisha mfumo wetu wote wa maisha na kuleta mfumo mpya tusioujua, na kama kawaida ya binadamu anaogopa mabadiliko hivyo wananchi wengi wanaweza kuungana na CCM kuwapinga!
Mimi naona ni bora haya mambo ya muungano na majimbo wasingeyatoa sasa hivi kwa wananchi bali wangesubiri mpaka washinde ndipo waanza kuyafanyia kazi! Maoni yangu
Pengine huelewi kwa nini Chadema wanapinga muungano uliopo na wanataka nini.. Hoja ya Chadema ni kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika hivyo wanachokitaka ni kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo sii kwamba wanapinga muungano isipokuwa wanapinga muundo wa muungano huu.
Kama ilikuwa swala la ulinzi bila shaka chini ya Serikali ya Jamhuri Mapinduzi yatalindwa zaidi na chama chochote kitakacho ingia madarakani badala hili kuwa jukumu la mfumo wa chama kimoja yaani CCM (TANU na ASP). Kama nchi zote zilizofanya muungano na kulinda maslahi ya Kitaifa badala ya kutegemea chama kimoja ama kundi fulani la watu kuwa waasisi na walinzi wa muungano huu. Kizazi hicho kinakwisha na vijana wengi wa leo hawafahamu malengo wala nia ya kuwa na serikali hii na chama kimepokea maombi ya Wazanzibar ambao walizitaka serikali tatu toka uchaguzi wa mwaka 2000 na Chadema haikuwa nyuma kuunga mkono. Kwa nini leo wabadilishe?
Hivyo basi kama kuna utata ktk kuunda serikali tatu iwekwe wazi, watu wapime, waumize vichwa jinsi gani tunaweza kuuboresha muungano wetu Kikatiba bila kujali chama gani kitakuwa madarakani. Na swala la Majimbo pamoja na kwamba lina utata mkubwa lakini kulingana na WATU yaani sisi wenyewe na viongozi wetu inaonyesha wazi majimbo yaliyokuwa nyuma ktk maendeleo hayataweza kuendelea kamwe chini ya mfumo uliopo..
Mapendekezo ya Chadema ni kuwepo na serikali za Majimbo kwa kuzingatia hali halisi ilojitokeza. Hili ni pendekezo lao, binafsi yangu ningependelea zaidi kuwa na serikali za mikoa (county) ambazo zitapewa madaraka kamili ya kujiendesha kupitia kodi zao. watakusanya kodi zao na kati ya kodi hizo fungu litakwenda mfuko wa Taifa.
Mathlan kodi ikiwa asilimia 17, zitaganywa kama ifuatavyo Nane(8) ya mkoa na tisa(9) ya Jamhuri ya Tanzania. Hivyo kila mkoa kwa pato lake la asilimia 8 watapanga mipango yao na bajeti zao kimkoa wakati wakiomba serikali kuu fungu la maendeleo kupitia mchango wao wa asilimia 9 ambazo zitalenga zaidi miundombinu na miradi mikubwa ya Kitaifa kama ujenzi na uimarishaji wa Usafiri TRA, ATC, Umeme (Tanesco, Maji (Dawasco), Mawasiliano na kadhalika. Kutokana na ombi la kuwepo Madaraka mikoani ni ktk kujaribu kuweka jukumu la kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi mikononi mwa wananchi wenyewe kufuatia sera za chama kilichopata ushindi ktk uchaguzi sehemu hiyo, hivyo sera na nguvu ya kodi yao kuwa sababu ya maendeleo yao na kadhalika badala ya kuendelea kuitegemea serikali kuu ambayo inaendesha miradi yake kisiasa zaidi.
Ni imani yangu hakuna mikoa hafifu isipokua ukiritimba na urasimu ndio umepoteza umuhimu wa uwekezaji ktk mikoa kama ya Singida, Rukwa, Songea n.k.kila mkoa una utajiri wake, lakini tumeshindwa kuiwezesha isipokuwa ile yenye utajiri wa haraka haraka kwa manufaa ya viongozi wetu. Mradi wa Mtwara utachukuliwa kuiboresha Dar ama ni mradi wa kiongozi @10%..Mfano mwingine, Singida leo hii ilitakiwa kuzalisha Umeme wa upepo au miali ya jua, kuboresha kilimo cha mafuta ya alizeti na kadhalika lakini hakuna hata mpango huo kwa sababu tunategemea serikali kuu.
Tazama Mgogoro kama huu wa Madaktari haukutakiwa kuwa wa nchi nzima hata kidogo. Kama majimbo yanaweza kukusanya fedha vizuri sioni sababu ya sehemu kama Shinyanga, Mtwara na Mara kuwa nyuma ktk maendeleo wakati wao ndio wanachangiaji wakubwa wa pato la Taifa iwe ktk madini au ukulima. Sioni sababu ya Tanzania yetu kuwa na Hopitali moja tu kubwa nchi nzima (MNH) ilojengwa toka enzi za Nyerere..Hivyo swala la majimbo linaweza kuwa suluhisho ikiwa tuta jihadhari na negatives zake maana kupanga ni kuamua..