CHADEMA, huu ni wakati wa kufanya maamuzi magumu...

Status
Not open for further replies.
Haya malumbano yao yanatusababishia tuanze kuvuta kumbukumbu za Viongozi wote wa CDM waliopoteza maisha ki ajabu ajabu. Yaelekea hii michezo yao ya kuuana imekuwa ikifanyika sana ndani ya CDM! Ngoja tuone na mwisho wa hii muvi ya Ben na Zitto!!

Katika swala la kipuuzi narudia tena la kipuuzi nililoona wanarushiana hawa wanasiasa mawazo finyu humu JF bahati mbaya wanatoka upande wa kumtetea ZZK ni hili la KUUANA.

Na wewe umeingia kwenye mtego huu am very sorry for u.

Hv hata tukiamua kujadili hoja hii unaweza kudhibitisha kuwa ni kweli nati za matairi zililegezwa sio swala la kutunga ili kuchafuana tuu?je na kama ni kweli inamaana wabaya wa ZZK kutaka kumfanyia hila hiyo wapo CDM tu hawawezi toka CCM,na mwisho je dereva, sijui kama na walinzi anao huyozito pamoja na wapambe wake hao wanaosema wameona nati za matairi zimelegezwa hadi adui analegeza matairi ya bosi wao wenyewe wanakua wapi nijuazwa kulegeza nati za matairi ni kazi ya muda mrefu zaidi.

Acheni siasa zisizo na mshiko kwa wenye akili hizi ndio mwendelezo wa propaganda za chacha wangwe..

Tena mafya wa CCMwenye nyenzo na utaalamu wa juu wanaweza kutumia mwanya huu kumaliza mtu CDM ili isemekane kauwawa na kikundi flani cha CDM.

Acheni siasa za kipuuzi na zenye kuhataisha maisha ya watu hizi shame on u all under this argument.
 
Waacheni wayatoe madonge yao..inasaidia uma kujua tuna viongoz wa aina gani..by the way ni upepo tu
 
Kwenye hil indugu yangu tuiweke CCM pembeni; hili ni la CDM tu. Kwani hawa watu wameshikiwa mapanga na bunduki na CCM kichwani? Au tunafikiri wamekaa kama maroboti ya kisiasa ambao wenye kuyaendesha wako Lumumba? Kuilalamikia CCM kwa yanayoendelea CDM ni sababu tosha ya kwanini CDM inahitaji kufanya kitu. Haiwezekani CCM wapike Lumumba chakula kiive Rufiji!
Hakika walipofika CDM wamelea wenyewe!!Naomba Mwanakijiji ebu jaribu kuwajenga CDM waachane na I dont sijui nitumie neno gani ili nieleweke vizuri!!nasema hivi daima chini ya uso wa duniani katika siasa hizi za vyama vya ukinzani [Opposition] kumtamka CCM katika vita iwe ni Internally au Externally ni mapungufu kwa jumuhiya husika hivyo naweza kusema hawajui wanachokitafuta.

Binafsi kwa upeo wangu CDM wanapaswa kuwa wanajua TANGU CDM inaanzisha CCM ndie wakinzania wao na strategy zote ziwe ni kuangalia watawapiku vipi CCM na CCM wanajua toka CDM [Hata kama Mwalimu alismea inafaha] izaliwe watawaangalia kwa jicho la umakini na kuakikisha hawafiki popote na mkakati wa kuwazamisha melini.Hili la kusema CCM ndio kasababisha haya KUDADADEKI tena naona CCM wamechelewa sana !!!!!Mwanafunzi anasoma,lakini kipimo cha kusoma huko kuwa ameelewa ni kufaulu mitihani wake huwe wa majalibio au wa mwisho.Mtihani wa CDM ni CCM na Mwanafunzi ni CDM msahihisha na makaguzi kuwa umefahaulu vyema au vibaya ni MTANZANIA.

Hizi habari za ooooooooohhh CCM hivi au CCM vile this is full of shit go to war with full gadfly gadgets>Jukumu la CDM toka linazaliwa ni kujua adui yao number moja na mtihani wao number moja ni CCM na mikakati yake!!Wanapaswa kujua kucheza na CCM kwa kila mbinu,na swala si la kuwapigia wananchi kelele oooooohh CCM leleleelleelelleelele siamini watu wenye upeo wa elimu ya juu graduate awezi kujua kuwa mkate unaoutaka wewe na mwenzio anaoutumia.

Hivi mnategemea CCM wawape Nchi mikononi amjui kuwa madaraka ni ulevi [Opium] yataka busara za kimungu kama ZANU ya Kaunda kuyaachia.Hivyo CCM wakiwapa nyie mikononi kama Sadaka nyie wao wafanye nini, wawe kama KANU ya Moi.Ebu CDM waambie CDM waaache upuuzi wako vitani hawapaswi kumlalamikia CCM hata siku moja mwnafunzi halalamiki Mtihani kwa kuwa anajua Mtihani ndio shule yenyewe.

Ebu ona hili wenzao walivyo faster Mzee mmoja gwiji wa michezo alishachungulia Mchongo akaona umekaa namna ambayo unaweza ukaleta japo tashititi akaibuka na vyombo vya media Tanzania itegemee mpasuko na kubomoka kwa CDM.Yap kwa wenye akili huu ndio moja ya michezo ya kisiasa alichofanya ni kuwaanda Watanzania na wanacdm kisaikolojia uku akiwa tayari na ufahamu nini kinafuata.

CDM waache kuiangalia CCM kwa jicho la kulalama wajipange,waje na vitu vilivyo enda shule,uweiz kutegemea mpewe Nchi kwa style ya kutokujua hata kujipanga kimikakati [Strategy] kupambana na aliyepo mdadarakani tena anahistoria ya ukombozi, thats bull shit sysytem ya wapi hiyo duniani?.CDM wanapaswa kujiaminisha maeneo mengi kwamba wao sasa ni wakomavu, pevuka na kuwa na mikakati ya juu zaidi ya CCM tena yenye FAIDA kubwa kwa TAIFA zaidi ya CCM,kisha mfumo [SYSTEM] itapima kama wanastahiki kisha Wananchi waweke TIKI na kusema sawa.

Hii leleleleele dam Nchi sio leleleleele CDM!!!!!Nchi ni UHAI wa Watu na Familia zao,wanataka mtu watakae mwamini wakae kwenye majumba yao wakiwa salama.Hata Kama CCM ina madudu kama HAMJAWAAMINISHA kwa kushika [Strategy] na wao WAKO SALAMA majumbani mwao basi CCM ataendelea KUTAWALA tena kwa ridhaa ya umma.

Kwa wenye ufahamu wa mambo hata kama wananchi watataka mabadiliko lakini kwa wenye ufahamu wa mambo tena watanzania makini hawataruhusu eti BORA mabadiliko huku wakijua anaekwenda kupewa madaraka ajajianda na ajui anachokitaka.Mungu saidia kidogo Tanzania ni Nchi tofauti na Nchi nyingi sana Africa na hata Ulaya ya kutokukurupukia mambo ya kisiasa kwa mtindo wa fashion.Uzuri kila mtu anajua tizama kenya, tizama zambia, tumeona na kujifunza mengi.Kwa wasio jua Tanzania ni NCHI salama kwa Nchi zote za maziwa makuu tukiiingia sisi kwenye mchezo eti tujalibu tu hata kama wanachi wameichoka CCM, thubutu iyo haipo hakuna Nchi ya majalibio ya kutawala.

Kijana atapewa mke na familia yake baada ya kufundishwa jinsi ya kujituma mwenyewe na kuwathibitishia wanajamii yake kuwa ANAWEZA kumtunza mke wake na watoto wake pasipo msaada wa mtu yoyote,zaidi atapewa ushauri na wanajamii wenzie.
 
Kwa mtazamo wangu naamini kabisa CDM ndo kitazidi kuimarika. Dunia ya leo hatuhitaji mambo ya kufichaficha, ni bora kuwajua wanaotaka kuongoza nchi yetu kuanzia utosi hadi unyayo. Tukumbuke kuwa dhambi ya kufichana ndo inayotumaliza na kututesa sie wananchi, mfano mdogo tuangalie jinsi viongozi wetu wanavyosaini mikataba kwa kificho pasipo wananchi kuelewa lolote, yote hii imetokana na dhambi ya kulea mabaya kwa kificho kwa serikali iliyopo madarakani.
Wacha wavuane nguo tuwajue vizuri, hakuna sababu ya kurudi nyuma kama we unataka mapinduzi ya ukweli.
 
Katika swala la kipuuzi narudia tena la kipuuzi nililoona wanarushiana hawa wanasiasa mawazo finyu humu JF bahati mbaya wanatoka upande wa kumtetea ZZK ni hili la KUUANA.

Na wewe umeingia kwenye mtego huu am very sorry for u.

Hv hata tukiamua kujadili hoja hii unaweza kudhibitisha kuwa ni kweli nati za matairi zililegezwa sio swala la kutunga ili kuchafuana tuu?je na kama ni kweli inamaana wabaya wa ZZK kutaka kumfanyia hila hiyo wapo CDM tu hawawezi toka CCM,na mwisho je dereva, sijui kama na walinzi anao huyozito pamoja na wapambe wake hao wanaosema wameona nati za matairi zimelegezwa hadi adui analegeza matairi ya bosi wao wenyewe wanakua wapi nijuazwa kulegeza nati za matairi ni kazi ya muda mrefu zaidi.

Acheni siasa zisizo na mshiko kwa wenye akili hizi ndio mwendelezo wa propaganda za chacha wangwe..

Tena mafya wa CCMwenye nyenzo na utaalamu wa juu wanaweza kutumia mwanya huu kumaliza mtu CDM ili isemekane kauwawa na kikundi flani cha CDM.

Acheni siasa za kipuuzi na zenye kuhataisha maisha ya watu hizi shame on u all under this argument.

We are thinking on the same plate.
 
Naona wana CCM wenzangu mnafarijiana humu eti CDM inakufa sasa,huku wengine mkiigiza wana CDM mloanza vunjika moyo,tuendelee kujifariji.

Ila ninachojua CDM inapendwa sana, muulize mwenyekiti WA chama. Mwaka 2010 kama kungekuwa na tume huru CUF Zenji na CDM bara ndo walishinda uchaguzi.

Sherehe ya humu jamvini mnayofanya ni dua la kuku tu,tatua kero za wananchi WA Mwanza hasa wamachinga,cyo kupambanana meya hapo mtawarudisha chamani, sherekea tu Ila kura utakazo utashangaa
 
Vijana wa CHADEMA na Uongozi wa Taifa wa CDM wanakatisha tamaa na wanasikitisha pamoja na kuudhi kulikopitiliza; na hapa nazungumzia wa kambi zote zinazokinzana katika mjadala unaoendelea. Wanakatisha tamaa kwa sababu wanarudisha nyuma juhudi zote za yote tuliyoyafanya kufikia hapa tulipofikia.

Maana sasa inaonekana wanashindanisha nani ana akili zaidi kichwani, nani mjanja zaidi na nani anaweza kugundua unafiki wa mwingine.

It is pathetically shameful and somebody need to do something vinginevyo wengine tutaingilia kati kama kwenye mjadala wa "Urais na Ujana vs. Uzee".

If you guys can't we will help you. It is absolutely pathetic.

MMM
Tik Tak Tik Tak

Nadhani umeamua kutumua maneno makali ili watu wajirekebishe. Maana wote hawa wakiondoka kutakuwa na Furaha ccm lakini chadema ni kama mti Mkubwa umepigwa panga moja, maana tumekuwa tunawahisi na watu wote hata wa chini wanajua
 
Tusikate tamaa bado lingaliko tumaini kabisa tena kubwa,ili mbegu iote lazima ife
kwanza ndipo huota na kuzaa matunda mengi,Ili CHADEMA izae matunda lazima
magugu yafe ili iote mbegu mpya njema,bora yenye uzalendo wa kweli kwa Taifa
la Tanzania si kwa maslahi binafsi"
 
Mzee Mwanakijiji niko tofauti kidogo na mtizamo ulionao. Kinachoendelea CHADEMA ni wasaliti kuelekea kujirudi, kutambua makosa yao na hatimaye kuwa na move ambavyo ni very unified na strong. Ukiangalia nyuzi zote zilizoko humu JF kutoka kwa vijana wote wa CDM utaona jambo moja tu, wamekiri kusaliti chama na hata kushambulia uongozi wa juu wa chama.

Kinachofanyika sasa hivi si busara kuingia haraka na kuanza kutoa miongozo, CHADEMA kimeshakuwa chama cha umma, widespread na impact yake ni kubwa. Na naamini JF ni sehemu ya vijana hawa kumaliza na hata kushusha mori na mihemuko yao. Sifikirii kama mijadala inayoendelea sasa itapelekea watu kuchinjana na kukiua chama. Hakuna uwezekano wa hilo maana CDM si mtu mmoja mmoja, imeshavuka hatua hiyo kwa sasa.

Kitu pekee kinachotakiwa kufanywa na CHADEMA kwa sasa ni kuwaita chamani wale wote waliojitolea muhanga na kuanika usaliti wao.Kwangu mimi wote waliopost nyuzi zao jamvini wana kila sababu ya kuitwa kwenye round table na kueleza kila kinachoendelea na baadaye kufanya joint press conferences. Kila kitu kitakwenda sawa tu.

Kuna wakati huwa najiuliza kama Jamii Forum isingekuwepo CHADEMA na wimbi la vijana wake ingesimama kweli? Naona vikao na kuelezana ukweli ni tatizo kubwa. JF imesaidia kuficha hilo na ndiyo nguvu iliyonayo CHADEMA kwamba kila mtu anaposhiriki mijadala na viongozi wake wa juu basi anajiona ni sehemu ya chama na mtu muhimu sana katika kukipeleka chama kwenye mafanikio.

Let us go on observing the saga latter on everything will be waived. Kitu pekee cha kuwakumbusha CADEMA ni kwamba muda hauwangejei so lazima wajue kuushika muda wote na kuufuata.
 
Last edited by a moderator:
Hizo ndizo faida za mtandao. Mtandao umeijenga CHADEMA na mtandao huo huo ndio unaimaliza CHADEMA! Mkuu wacha watu wamwage nyongo. Nadhani taarifa zingine itabidi polisi wazifanyie kazi hasa linapokuja suala la vijana kutishina kuuana kwa njia mbalimbali. Watu wanalegeza nati za matairi ili mtu afe. Kuna kilio kiliwahi kutoka kwamba kiongozi mmoja wa CDM alilegezewa nati akapata ajali akafariki sasa na hizi zingine zinasema gari la Zitto lililegezwa nati! Wacha wasemane na kutajana yaishe.

Tusikubali kuamini kila kinachosemwa na hawa vijana.
hakuna anayekanusha uasisi na uendeshaji wa kikundi cha uasi.
sasa nani alikiwa msafi ndani ya kikundi cha uasi hilo ni jambo la lesser evil....ngumu sana.

tujiulize zile kampeni maalumu za kuwachafua Dr Slaa na Mbowe zilikuwa ni bahati mbaya au zilikuwa ni mpango mahususi??
 
uongozi wa chadema ukae hivyo hivyo utuachie wana jamii tuamue.alichokitaka na anchokitaka zitto ni kusikia wameitwa kwenye kikao halafu maamuzi magumu yafikiwe halafu atangaze kuondoka chadema na kisha mzee wassira aseme chadema imepasuka.tumeshamjua zitto ni msaliti! kwa sasa ni kumpa majukumu ya kichama zaidi yaani aende kwenye m4c akiwa na lema ....mchawi mpe mtoto amlee!
 
Mlachake hawa si vijana wadogo kwenye siasa, labda wadogo kiumri tu wanajua madhara ya malumbano yao kwa afya ya chama, lakini kuna msukumo kutoka nje kukidhoofisha chama kwa kuwatumia hawa vijana wafanyabiashara wa siasa! Shame on them! Imani yetu kwa CHADEMA haitetereki hata mkinunuliwa wote!
 
Last edited by a moderator:
Ninaomba isifikie chama kikaendeshwa na autopilot na nahisi huko ndiko kinapoelekea, kuna kausemi ka ZZK kuwa ukimgusa Zitto umeigusa chadema huwezi kumjeruhi Zitto ukaicha chadema salama. Mimi nashauri ZZK na kundi lake wote wanyofolewe kwenye uongozi wa chama wabakie na makundi yao, ili kama kweli kama wao wanavyolia na CCM na usalama wa Taifa wafe wote pamoja. Fujo walete wao halafu watafute wachawi, wamekwenda kujichanja kwa waganga na ninawaonea huruma sana albino kwani swala la uchawi tz linaendeana na na ama albino kama walivyowawinda eti ili kumaliza mpaka panya, kweli elimu ya Tanzania haiwezi kumkomboa mtanzania kama msomi anamwamini kibabu kizee kinakoishi kijijini kwa tabu kikiwa na ndunguri halafu kifua mbele unasema umechanjwa com on shame on u guys. Eti waliapishana kwa waganga wa kienyeji kimekuwa chama cha siasa au genge la washirikina inatia kinyaa sana na nimewadharau mno wote walioshiriki maovu hayo kwa ajili ya vyeo tu hapo ni chama tu je tukiingia magogoni si ndio wazee wote watahamia kivukoni kumlinda Rais.

Imani za kishirikina ndio chanzo kikubwa sana cha umasikini, vifo na nk. Wale wote ambao wanaamini ushirikina sio wabunifu, ni wavivu kwani kila kitu wanaamini kulogwa. Hawawezi kutafuta tatuzi la mambo, hii ndio sababu wanasisa wetu hawahangaiki kuimarisha huduma za afya kwani kila kitu wanaamini wamelogwa. Mshirikina ni mwoga na anaweweseka kwani ana imani zinazomtesha.

Hakuna ushahidi kwamba imani za kichawi zimeweza kumsaidia mwanadamu. Ndio maana wote na popote kwenye ushirikina ni masikini na baya zaidi wanasababisha wototo kufa kwa maradhi yanayotibika, badala watoto wapewe chanja na dawa za kutibu maradhi wanawafunga vitambaa vyeusi vilivyofungwa mavi ya punda.

Hapa sipati picha kwamba zito yeye kwao alivyoiga na nuclear ya kuulia mpaka panya kabeba nini. Sasa akishindwa Uraisi sijui itauawa wangapi, nafikiri panya wa ikulu watakoma kuringa.

Aibu sana na inasikitisha mno hao ndio vijana wasomi wanaoamini lazima wawe wevyeti wa chama na maraisi kwani wao ndio wasomi na wenye akili kuliko wote ndani ya chama.

Weka bench wote hawana faida tena, hakuna mwenye uchungu hata mmoja zaidi ya njaa za tumbo. Kuwalea ni kuuwa chama. Chama hakiwezi kuendekeza huu uchafu. Act now.
 
naona wana ccm wenzangu mnafarijiana humu eti cdm inakufa sasa,huku wengine mkiigiza wana cdm mloanza vunjika moyo. tuendelee kujifariji. Ila ninachojua cdm inapendwa sana, muulize mwenyekiti WA chama. mwaka 2010 kama kungekuwa na tume huru cuf zenji na cdm bara ndo walishinda uchaguzi.
sherehe ya humu jamvini mnayofanya ni dua la kuku tu,tatua kero za wananchi WA mwanza hasa wamachinga,cyo kupambanana meya hapo mtawarudisha chamani. sherekea tu Ila kura utakazo utashangaa

Hapo ndo mnakosea sana, unadhani wanaokipenda wanakipenda bila sababu? Kilichosababisha wakipende kama hakipo hawatokipenda tena.

Unadhani ni cha kwanza kupendwa? Watu siyo static, ni dynamic unapotaka kuendelea kupendwa unapaswa kujenga mazingira ya kupendwa zaidi. Ukifika mahali ukaridhika hapo ndo mwanzo wa kuporomoka.
 
Kweli Mkuu kuna tatizo kubwa sana la Comfidentiality ndani ya CDM na ndio litakipoteza chama. Nadhani vijana waanze kufanyiwa veting labda itasaidia.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom