Chadema hela ya kufanyia mikutano wanatoa wapi?

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Mimi kama raia wa Tanzania ningependa kufahamu hela ya kufanyia mikutano ya CHADEMA inatoka wapi?

Kwa utafiti mdogo nilioufanya mikutano ya kitaifa inayofanywa na viongozi wa CHADEMA si chini ya dola za kimarekani 5000. Lakini cha ajabu CHADEMA wanaweza kufanya mikutano mingi sana bila ya kupumzika.

Nina nia nzuri sana ya kufahamu haya jamani. Mimi ni mwanachama hai wa CHADEMA na ningeomba viongozi au wanachama wenzangu mnijulishe kuhusu hili.
 
sisi wana-CHADEMA tunakichangia chama ndio maana mkutano ukiisha kuna box linapitishwa mwenye nacho anatoa!!
pili Ruzuku inatusaidia.
 
Mimi kama raia wa Tanzania ningependa kufahamu hela ya kufanyia mikutano ya CHADEMA inatoka wapi?

Kwa utafiti mdogo nilioufanya mikutano ya kitaifa inayofanywa na viongozi wa CHADEMA si chini ya dola za kimarekani 5000. Lakini cha ajabu CHADEMA wanaweza kufanya mikutano mingi sana bila ya kupumzika.

Nina nia nzuri sana ya kufahamu haya jamani. Mimi ni mwanachama hai wa CHADEMA na ningeomba viongozi au wanachama wenzangu mnijulishe kuhusu hili.

Acha upumbavu, unatutajia dola za Marekani kututisha ama!? tupe mchanganuo makini wa hizo gharama afu tuchangie otherwise....
 
Wafadhili wanahusika mfano Sabodo, vyama rafiki na wananchi wapenzi wa CHADEMA.
 
Kwanza rekebisha kiasi cha pesa, umefanya makadilio ya chini sana kiasi cha kuhama kwenye uhalisia, kwa ufupi, mikutano ya CHADEMA ina husisha 'chopa', nadhani kwa makadilio ilipaswa uweke si chini ya milioni 100 kwa mkutano. Sasa uanze kuhoji, pesa wanatoa wapi?
 
fuata taratibu za chama za kupata taarifa kama ww ni mwanachama halali, acha majungu, umeweza kujua garama ya mkutano chanzo cha pesa unashindwaje? Mnafiki mkubwa ww.
 
Kama mimi, sijui CCM wanapata wapi pesa za kuhonga wapiga kura wakati wa uchaguzi, kwa CHADEMA labda viongozi watujuze zaidi...pia viongozi wa CCM naomba wanijuze pia..
 
Tunachangia sisi wananchi wapenda mabadiliko
 
Kwanza rekebisha kiasi cha pesa, umefanya makadilio ya chini sana kiasi cha kuhama kwenye uhalisia, kwa ufupi, mikutano ya CHADEMA ina husisha 'chopa', nadhani kwa makadilio ilipaswa uweke si chini ya milioni 100 kwa mkutano. Sasa uanze kuhoji, pesa wanatoa wapi?

Unajitekenya afu unacheka kwa sauti!!!
 
Kwanza rekebisha kiasi cha pesa, umefanya makadilio ya chini sana kiasi cha kuhama kwenye uhalisia, kwa ufupi, mikutano ya CHADEMA ina husisha 'chopa', nadhani kwa makadilio ilipaswa uweke si chini ya milioni 100 kwa mkutano. Sasa uanze kuhoji, pesa wanatoa wapi?

mkuu unaijua milioni mia wewe? acha mzaha kwenye mijadala kama hii!
 
Kwanza rekebisha kiasi cha pesa, umefanya makadilio ya chini sana kiasi cha kuhama kwenye uhalisia, kwa ufupi, mikutano ya CHADEMA ina husisha 'chopa', nadhani kwa makadilio ilipaswa uweke si chini ya milioni 100 kwa mkutano. Sasa uanze kuhoji, pesa wanatoa wapi?
na wewe huo mchanganuo umeutoa wapi? Acha bra bra mkuu...
 
Mimi kama raia wa Tanzania ningependa kufahamu hela ya kufanyia mikutano ya CHADEMA inatoka wapi?

Kwa utafiti mdogo nilioufanya mikutano ya kitaifa inayofanywa na viongozi wa CHADEMA si chini ya dola za kimarekani 5000. Lakini cha ajabu CHADEMA wanaweza kufanya mikutano mingi sana bila ya kupumzika.

Nina nia nzuri sana ya kufahamu haya jamani. Mimi ni mwanachama hai wa CHADEMA na ningeomba viongozi au wanachama wenzangu mnijulishe kuhusu hili.

Kwa nini umefanya utafiti kwa kutumia Dola za Kimarekani?
 
Sisi wafuasi wake tunachanga.. Kukiwezesha chama chetu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
acha umbea, nini kazi ya ruzuku ya chama ni kuwaelimisha watz.
GO GOG GO GOG GOG TUNAOMBA KIELEWEKE 2015 CHINI YA MAKAMANDA WA CDM
 
Hata CCM wangeweza fanya mikutano,tatizo wana CCM ubinafsi wanawaza matumbo yao tuu
 
Back
Top Bottom