jogoo_dume
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 2,196
- 1,940
- Thread starter
- #21
Hivi kuna watu waongo nchi hii zaidi ya watawala wa nchi hii?
Uthibitisho wa hilo ni majuzi tu tulimsikia Mkurugenzi wa shirika la Umma la serikali ya CCM, shirika la umeme la TANESCO Engineer Mramba alipoongea kwa kujiamini kupita kiasi kuwa suala la mgao wa umeme litakuwa historia baada ya gesi ya Mtwara kupitia kwenye bomba jipya lililojengwa na wachina kuanza kufika Dar na hivyo kufanya mitambo mitatu ya kufua umeme ya Kinyerezi na Ubungo kuanza kuzalisha umeme unaofikia megawati zaidi ya 300 ambazo tayari zimeshaanza kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Sasa huu mgao wa umeme wa 'kufa mtu' unaoendelea kote nchini haijawa uthibitisho kuwa viongozi wanaoongoza kwa uwongo hapa nchini ni kutoka serikali hii ya chama tawala cha Sisiem?
Katika vitu ambavyo vinaniudhi ni huu uongo tunaoambiwa kuhusu umeme, ninategemea umeme kufanya shughuli zangu za kuniingizia kipato, hivyo nakwama sana. Hii ni point moja kubwa ambayo ccm wameipoteza.