Kwanini Hao waondolewe katika madaraka ya Juu?
1. Mbowe: Hana jambo jipya kwa watanzania, nimtu anaepigania zaidi umaarufu wake na maslahi yake, kuliko maslahi
ya Taifa, na hili lipo wazi hata wanao muunga mkono wanajitahidi tu kufanya hivyo ila ukweli wanaujua.
2.Dr Slaa: mafia alitaka kumuua zitto ref mwampamba na ya rwakatare.
3.Rwakatare: Anatekeleza mambo maovu ya kuua wasio na hatia kwa maagizo ya wakubwa.
4.Tundulisu: anatetea uovu wa rwakatare.
Nilipoanza kusoma mwanzoni, nilishawishika na mawazo yako, lakini nilipofikia kwenye sababu za kwanini waondolewe, nikapoteza imani kama wewe ni mpenda mabadiliko au ni mmoja wa wale wanaomtumikia khafir ili kufanikisha malengo yao.
Katika sababu zote ulizotaja hakuna yoyote ya msingi na yenye ukweli. Kwa kuwa umezitaja kutokana na hisia.
katika pendekezo lako la kwamba watolewe hujaweza kupambanua ni akina nani wanafaa na kwanini? Inawezekana hapa kuna watu mnachezo beats za mtu fulani ambaye anatafuta kwa hali na mali kushika madaraka ya juu ya chama au mnamhofia mtu fulani ndani ya CHADEMA na hivyo mnatafuta kila sababu ya kumtoa ili mpate kukimaliza chama.
CHADEMA imepita katika misukosuko mikubwa na migumu tangu ya wakati wa Wangwe, lakini ni timu hii hii unayosema leo haifai ndiyo iliyoivusha CHADEMA katika mazingira magumu na ya shida hata kukiwezesha CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Leo inakuwaje tuseme hawa ndiyo wanakiua chama? Tunataka kusema wamesahau machungu na magumu waliyoyapitia katika kukikuuza chama kwa pesa zao za mfukoni, wakati huo kikiwa hakina hata ruzuku?
Hivi kuna yeyote anayefahamu taabu adha na shida walizokutana nazo akina
Zitto, mbowe, Bob Makani (RIP)
slaa na wengineo wengi katika harakati ya kukijenga chadema? Mimi nasema hawa wachache ndiyo wanaojua uchungu wa chadema, na wanajua wamepitia mangapi magumu. Demokrasia ya ndani ya chama ndiyo iamue kwamba waendelee au hapana na si hisia za mtu mmoja tu anayekuja na sababu zisizo na msingi na kusema hawa watoswe. Hatutakuwa wepesi kudanganyika kirahisi kiasi hicho.