CHADEMA Hatuitaji kuwatenganisha hawa Vijana

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,742
2,000
Ben Saanane, Habib Nchange, Juliana Shonza, Mwampamba, Exaud Mamuya, Gwakisa, Sanga na Zitto ZK

Nimejitahidi sana kupitia post zilizowekwa humu jukwaani, kwa mtazamo wangu hawa vijana hapo juu wapo katika kundi maalum lililoandaliwa kuihujumu na kuiua CHADEMA nayasema haya kwa sababu zifuatazo
1. Tumeshuhudia kundi moja likitoa maelezo likijionyesha moja kwa moja linatumika na viongozi wakuu kwa ajili ya kumuangamiza Zitto ikiwa ni pamoja na kutaka kumuua tuuma ambayo ni kubwa sana na ni mbaya sana kwa uhai wa chama

2. Pia tumeona kundi lingine likiwa limeegemea upande wa Zitto na likionyesha mbinu na mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika eti kuleta Demokrasia katika Chama na hili likionyesha Zitto alikuwa akubaliana na viongozi wenzake wa Juu (Mwenyekiti na Katibu Mkuu)na akiwa katika mbinu ya kuanzisha chama kingine (CHAUMA)

3. Hii inaonyesha hawa vijana wamejipanga vyema kulitumia hili jukwaa ili kuuchonganisha uongozi wote wa Juu wa CDM na mwisho wa siku wakose kuaminiana, kuheshimiana.kwani haiingii akilini kama kweli ni mwanachama muadilifu wa CHADEMA watoe maelezo kama haya tuliyoyasoma humu ambayo yalitakiwa yawe siri na utatuzi wake ufanyike kwenye vikao vya ndani vya chama.

4. Pia ningependa kukumbushia ile kauli ya Ndg. Steven Wassira kuwa CDM itakufa kabla ya 2013 hii inajionyesha haya mambo yamepangwa na waliopewa jukumu hilo ni hawa vijana akiwemo na ZITTO kwani tumeshuhudia wengine wakiingiza suala la Ukanda ambalo limezungumzwa sana na Viongozi wa CCM wakati wakiishambulia CDM

5. Pia nimeshuhudia pale Ben Saanane alipokuwa akisakamwa na hawa wenzake yeye alikuwa anagonga Like! Ikimaanisha anawaunga mkono kwa kutoa hicho walichopanga.

** Wito na maoni yangu Uongozi wa Juu wa chama ulitafakari hili na ikiwezekana kuchukua maamuzi magumu ambayo yatakitetelesha chama kwa muda mfupi lakini kukifanya kuwa Imara kwa muda Mrefu na kuheshimika kuliko kama ilivyo sasa ambapo chama kimekuwa kama jumuiya ya Kambale hajulikani baba, mama wala mtoto wote wana masharubu.
Nawasilisha!!!!
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
Hivi Jmushi best yangu mbona sijamuona kwenye sakata hili la hawa vijana....?mwenye jibu anaisaidie
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,028
2,000
Nakuunga mkono mwanzisha mada hii;
Imani yangu ni kwamba wale wanaotumiwa na CCM kuvuruga CHADEMA hao si wana CDM halisi na si wapenda maendeleo ya jamii, si wanamapinduzi. Uongozi wa juu ufanye kazi yao; si kuwafukuza kwenye chama bali ni kukaa nao na kuwapa worning; wakikaidi basi wavuliwe uongozi na wala si kuwafukuza. Kuvuliwa uongozi ina maana hawatakuwa na access ya siri za chama.
Kiongozi mzuri huwa hafukuzi - bali hutumia juhudu zake zote kuhakikisha yule asiye mwadirifu anabadirika na kuwa kwenye mstari.

Ila sasa kuna watu wanaonekana waziwazi kuwa ni wavurugaji, m2 kama Matata wa Mwanza; huyu jamaa labda kwa kuwa serikali inaongozwa na magenge ndo maana anakumbatiwa.
 
jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,941
2,000
ni kweli huwezi kuwatenganisha hawa ila kama utamwadhibu zitto na juliana ambaye anadai kuhujumiwa na dr Slaa utaibua mengi sana maana kwa maelezo ya hawa wasaliti maswali ni mengi kuliko majibu!
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,445
2,000
wote hawa ni wa kuwasafisha watokomee walikotoka
wapo vijana wenye mwamko na maono ya kulikomboa taifa
na sio wale wanaoamini katika ndumba na tamaa za mali
Chadema fenyeni maamuzi magumu pitisheni fagio hawa wote waliondika
ouvu wao hapa hata kama wamejuta hawafai tena,Mungu ameshaumbua mapema
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Hivi Jmushi best yangu mbona sijamuona kwenye sakata hili la hawa vijana....?mwenye jibu anaisaidie

jmushi1 hajaonekana ktk thread nyingi tuu na si hii kma unavyopenda.Watu wapo busy ndugu yangu,kuwa Jf ni sehemu ya uzalendo tuu na si kazi au nyumba ya kulala.
 
Nyamigota

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
365
0
Huyu Juliana hana lolote kuhusu tuhuma zake dhidi ya Dr. Slaa, kinachomsumbua huyu Dada ni kukubali kutumikia kundi hili la Wasaliti badala ya kuendana na dhamira ya Chama kama Wenzake akina Heche na Munishi. Zitto kama anahitaji kurudisha heshima yake ni lazima arejee uchapakazi wake aliokuwa nao wakati akifukuzwa Bungeni mwaka 2007 na aache mara moja kujitafutia umaarufu kupitia kundi hili la vijana Wasaliti. ajifunze viongozi wenzake kama akina Vincent Nyerere, Godbless Lema na akina Wenje wanavyojituma kujenga Chama bila kujitafutia umaarufu binafsi.

Nawakilisha.
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
jmushi1 hajaonekana ktk thread nyingi tuu na si hii kma unavyopenda.Watu wapo busy ndugu yangu,kuwa Jf ni sehemu ya uzalendo tuu na si kazi au nyumba ya kulala.

Pamoja na hayo kaka lkn sio kwa hot issues kama hz zaa masalia kwa jembe lile...kwasababu ukimsoma vzr mambo mengi anayojengeaga hoja humu JF yanauhusiano sna na hz issue za masalia..so najiuliza kakosa vp..
 
mzalendo mtanganyika

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
309
250
Ben Saanane, Habib Nchange, Juliana Shonza, Mwampamba, Exaud Mamuya, Gwakisa, Sanga na Zitto ZK

Nimejitahidi sana kupitia post zilizowekwa humu jukwaani, kwa mtazamo wangu hawa vijana hapo juu wapo katika kundi maalum lililoandaliwa kuihujumu na kuiua CHADEMA nayasema haya kwa sababu zifuatazo
1. Tumeshuhudia kundi moja likitoa maelezo likijionyesha moja kwa moja linatumika na viongozi wakuu kwa ajili ya kumuangamiza Zitto ikiwa ni pamoja na kutaka kumuua tuuma ambayo ni kubwa sana na ni mbaya sana kwa uhai wa chama

2. Pia tumeona kundi lingine likiwa limeegemea upande wa Zitto na likionyesha mbinu na mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika eti kuleta Demokrasia katika Chama na hili likionyesha Zitto alikuwa akubaliana na viongozi wenzake wa Juu (Mwenyekiti na Katibu Mkuu)na akiwa katika mbinu ya kuanzisha chama kingine (CHAUMA)

3. Hii inaonyesha hawa vijana wamejipanga vyema kulitumia hili jukwaa ili kuuchonganisha uongozi wote wa Juu wa CDM na mwisho wa siku wakose kuaminiana, kuheshimiana.kwani haiingii akilini kama kweli ni mwanachama muadilifu wa CHADEMA watoe maelezo kama haya tuliyoyasoma humu ambayo yalitakiwa yawe siri na utatuzi wake ufanyike kwenye vikao vya ndani vya chama.

4. Pia ningependa kukumbushia ile kauli ya Ndg. Steven Wassira kuwa CDM itakufa kabla ya 2013 hii inajionyesha haya mambo yamepangwa na waliopewa jukumu hilo ni hawa vijana akiwemo na ZITTO kwani tumeshuhudia wengine wakiingiza suala la Ukanda ambalo limezungumzwa sana na Viongozi wa CCM wakati wakiishambulia CDM

5. Pia nimeshuhudia pale Ben Saanane alipokuwa akisakamwa na hawa wenzake yeye alikuwa anagonga Like! Ikimaanisha anawaunga mkono kwa kutoa hicho walichopanga.

** Wito na maoni yangu Uongozi wa Juu wa chama ulitafakari hili na ikiwezekana kuchukua maamuzi magumu ambayo yatakitetelesha chama kwa muda mfupi lakini kukifanya kuwa Imara kwa muda Mrefu na kuheshimika kuliko kama ilivyo sasa ambapo chama kimekuwa kama jumuiya ya Kambale hajulikani baba, mama wala mtoto wote wana masharubu.
Nawasilisha!!!!

[napenda kukupongeza mkuu kwa mada tenye tija na muono wa maendeleo ambayo umeitoa. ki ukweli hoja hii ni nzito na tena inahitaji uwezo mkubwa kuichambua (conscious mind) kimsingi sina maneno na vipengele ambavyo umeviweka ila ninataka kuiangalia zaidi point namba 4 ambayo iko highlighted in red.
ni ikweli ulio thabiti tena haupingiki kwamba CCM imekuwa ikiamini kuwa iko a next step ever.....na ndiyo maana nashawishika kusema mkakati na mpango wote unaoendelea unakila sababu ya kuhusishwa na mkono wa chama hiki kikongwe. kimtazamo siasa nyingi za nchi znazoendelewa zimejazwa kila aina ya ulaghai na matukio ya kupangwa ndani ama juu ya chama kingine (UPINZANI) na hapa ndipo usemi wa politics a date game huthibitika.
Aidha kauli ya WASSIRA juu ya uhai wa CDM ni tata na ambayo inatakiwa iangaliwe kwa mashika tena kwa sura ya undani. kimtazamo hakukuwa na sababu ya chama kinaachoongoza dola kutoa kauli ambazo hazna tija kama hizi tena waziwaz huku kikitoa na wakatii kama si chenyewe ambacho kinatekeleza mkakati fulani unaolenga KUKIBOMOA, KUKIUA, NA HATA KUKISAMBARATISHA kwa njia yoyote chuini ya matakwa yake.
mwisho namnukuu mhshimiwa ZZK aliyewahi kuandika kupitia JF kuwa " hhuwezi kum-maliza zito kisiasa bila kuiua CDM ama kuiua CDM bila kum-maliza zitto,,,,,,,, kauli kama hii inathibitisha mawazo kuwa ZZK asingekuwa mshenzi kufkiri kuihujumu CDM huku akiamini mtaji wake kisisasa unafadhiliwa na kudhaminiwa na CDM.
HITIMISHO
jambo hili lapaswa litzamwe kwa undani san la sivyo litaathiri na kukisambaratisha chama hchi kikuu cha upizani na strugle yao yote ku-end up in vain,,,,,I believe being mor wise and precise CDM wont allow this.]
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Huu uchambuzi wako ni wa kusadikika.

Ni maoni binafsi na sio uchambuzi. Yaani umeweka mawazo kuwa hitimisho la mijadala ile badala ya kutumia mijadala ile kuhitimisha hoja husika.

Kwamba kuna watu wenye kutaka kutengeneza makundi, hilo liko wazi kama jua. Kwamba kuna wasaliti hilo sasa limethibitishwa. Kwamba kuna mkakati wa CCM kuingamiza CHADEMA kwa kutumia watu wa ndani na/au nje hilo nalo limepata ushahidi mkubwa zaidi, hasa kwa ndani. Na kadhalika .....

Sasa wewe unapohitimisha kuwa wale vijana wanachonganisha viongozi, je mahusiano ya viongozi wa juu wa CHADEMA kabla ya wiki hii ulikuwa unayajua yakoje? Pia ni kwa nini Zitto aungwe mkono na watu wale wale ambao wanawatukana na kuwadhalilisha viongozi wenzake? Ni kwa nini hali iko vile ilivyokuwa?

Rudi studio mkuu.
 
THE GAME

JF-Expert Member
May 30, 2010
584
500
bora wote wenye malengo mabaya na cdm wapigwe chini tujue tupo na wazalendo wa kweli.
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Pamoja na hayo kaka lkn sio kwa hot issues kama hz zaa masalia kwa jembe lile...kwasababu ukimsoma vzr mambo mengi anayojengeaga hoja humu JF yanauhusiano sna na hz issue za masalia..so najiuliza kakosa vp..

jmushi1 atakuja, huwa si mtu wa kukimbia hoja yoyote.
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Tatizo la watanzania wengi sio wafatiliaji wa mambo na mara nyingi wanapenda sana kuconclude kwa ujumla jumla pasipo kuwa na data za kutosha.
Hivi kama Ben asingesema haya sasa ni wapi sisi tungejua? Achen kuptosha umma hapa Ben hana hatia yeyote.
 
JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
0
Piga chini masalia wote nashauri asibakie hata mmoja wakatafute Chama chao cha chauma au ccm bila kujali ni nani na anatoka wapi. Zitto yuko tayari kwenda ccm siku nyingi na negotiate ilishafanyika in return ya Urais kupitia ccm ili kummaliza slaa na kutunza interest za mafisadi. Hawafai
 
MAULA

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,056
1,250
Da siasa hata mi czielewagielewagi
Znakua kama mapenzi hivi mo ukwel ndan yake
 
Anne deo

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
505
250
Pamoja na hayo kaka lkn sio kwa hot issues kama hz zaa masalia kwa jembe lile...kwasababu ukimsoma vzr mambo mengi anayojengeaga hoja humu JF yanauhusiano sna na hz issue za masalia..so najiuliza kakosa vp..

sure..ata molemo simuoni kabisa jamvin
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,742
2,000
Tatizo la watanzania wengi sio wafatiliaji wa mambo na mara nyingi wanapenda sana kuconclude kwa ujumla jumla pasipo kuwa na data za kutosha.Hivi kama Ben asingesema haya sasa ni wapi sisi tungejua? Achen kuptosha umma hapa Ben hana hatia yeyote.
Ben kayazungumza haya kimkakati ili wote kwa pamoja wayaanike waliyokuwanayo, yeye amekuwa kama chanzo na hawa wengine ni vichocheo lakini lengo lao ni moja.
 
mashila

Senior Member
Oct 2, 2012
158
195
mi naona maamuzi magumu yanahitajika mapema sana, najua kuwa itateresha chama kwa mda ila itakifanya kidumu kwa mda mrefu sana, na wapo vijana wengi sana wenye moyo wa kujenga chama sio hao waroho wa madaraka na wanaotumiwa kama kondom then wanatupwa. Daima mungu yupo upande wetu na tutashinda daima
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom