CCM ndo huwaomba manyang'au wajiuzuru, CHADEMA huwa inawatimua na mfano mzuri ni Kafulila na wenzake...Nyie CDM hamna ubavu wa kumfukuza Shibuda; maana mlipomchukua mlifikiri mmefanikiwa; lakini sasa akiwa ndani au nje ya CDM atawamaliza maana mmemeza ndoano. Hahaha! Tusubiri maana ndoa sasa imekuwa ndoano.
Naona una ushauri mzuri ungewapa kina Nape mapema wala Rostam yasingemkuta.Haya ndio matatizo ya siasa zetu, sijasikia kwingine kokote Mbunge akijadiliwa kuwa na msimamo tofauti na wengine katika chama chake. Shibuda, huko ni matatizo tu, hiyo ni kampuni na ni usultani tu huko, si kama chama cha siasa cha kawaida, kama ulikuwa hujui sasa ndio utajuwa.
Badala ya watu kujadili strategies wanakwenda kumjadili mtu.
Labda wananchi wawe vilaza, mataahila, mtindio wa ubongo au mazezeta ndo watamchagua huyu kilaza anayetetea tumbo lake badala ya hao wananchi waliomchagua lakini vinginevyo ujue akitimliwa huu ndio mwisho wake na hata yeye anatambua hilo
kafurila alitoka akasiliba sana lakini bado wabunge waliongezeka.sembuse huyu ambaye hana hata mwaka chadema!.asepe tu.miammmmmh!patamu hapa na kama alibahatika kuyajua mengi ya CDM basi atabwabwaja pindi atakapo timuliwa.Nadhani anaweza kufanya kama Kafulila.
mmmmmh!patamu hapa na kama alibahatika kuyajua mengi ya CDM basi atabwabwaja pindi atakapo timuliwa.Nadhani anaweza kufanya kama Kafulila.
sio fukuza tupa nguo njee ya geti toshaCDM ilikuwepo kabla ya Shibuda na itaendelea kuwepo. Chadema ni ya wananchi na wakiamua hawamtaki basi hawamtaki. Hata kama ni kukosa jimbo.
Sifahamu sana taratibu na Katiba ya cdm zinavyosema lakini mimi ninamtazamo tofauti kidogo na wengi wa wachangiaji waliotangulia. Kwenye wengi pana mengi na kutofautiana mitazamo ni kawaida. Kosa la Shibuda ni kwenda kinyume na makubaliano/msimamo. Tunaruhusiwa kutofautiana ila tukishakubaliana lazima tuwe na msimamo mmoja. Na hapo ndipo alipokosea Shibuda. Chama kijadili na kitoe adhabu kulingana na taratibu/katiba yake
Tofauti yangu na wachangiaji wengi ni kuhusu tolerance/uvumilivu. Cdm inajijenga kwa gharama kubwa ikiwa ni pa1 na kushawishi wananchi wajiunge nacho. Itakuwa ni ajabu sana kama hawataweza kuvumiliana na kurudishana kwenye mstari pale mwanachama anapopotoka na badala yake ni kutimuana na kutupiana maneno ya kashfa. Chama ni Imani na wanaweza kuwa na imani inayofanana lakini hawawezi kuwa na approach/ mtazamo unaofanana. Nilazima wavumiliane na kukumbushana misingi ya chama hadi kufikia malengo.
Kwa mtazamo huo basi, nashauri Shibuda apewe ONYO tu, akirudia wampe adhabu!
Wanasiasa aina ya Shibuda ni mzigo mkubwa kwa ustawi wa Taifa.