Chadema hakuna wakumlaumu chama chenu mmekimaliza wenyewe

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,311
2,000
Wanaukumbi.

Ninachotaka kuchambua katika huu uzi haina utofauti na mitazamo ya magwiji wa siasa pamoja na wasomi mbalimbali, mgongano wa fikra, kimaono na kimtazamo ambao kwa sasa umeikumba Chadema, ni kiashiria tosha kwamba Chadema kama chama kinazamishwa na Chadema wenyewe.

Wasomi na wapenda amani ambao wapo mitaani na sehemu za kazi wakisema kwa nyakati tofauti kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua madaraka Zitto na wenzake hata bila kuwasikiliza ni kiashiria tosha kuwa chama hicho kinaelekea kufa kifo cha kawaida, Dr. Slaa alikaliliwaakisema hata katiba ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe, hakuna katiba itayaruhusu kufanya mipango ya siri, naye Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alikaliliwa akisema kuwa waraka huo unaeleza mbinu za uasi ambazo zililenga kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki za Chadema.

Kinachoonekana hapa si uhaini kama viongozi wa Chadema walivyotaka kuaminisha jamii bali ni mbinu za kutaka kudumisha uongozi wa kimla, usultani, udikteta, ukanda na kudhoofisha wanachama wa chama hicho amabao wanapigana kwa nia ya kupanua uwigo wa demokrasia ndani ya Chadema, Lissu anajaribu kuingiza vitendo vya malumbano ya kisheria ya mahakama na kuyapeleka kwenye chama, tumeona matokeo ya Kamati Kuu kule Kigoma yaliyomkuta Dr.Slaa na wapambe wake wameishia kupopolewa mawe na kukaribishwa na mabango.

Chadema lazima mkubali inapokalibia uchaguzi wowote ule wagombea wanaowania kuwaondoa walioko madarakani ni lazima watumie ushawishi au utaratibu wa kisiri ili mikakati yao isijulikane kwa wale waliopo madarakani, ni vigumu kuwakuta viongozi wa juu wa chama chochote cha siasa wakijadili maendeleo ya chama huku wamejiachia barabarani.

Tundu Lissu, anachofanya ni kulazimisha taaluma yake ya uanasheria iwe fimbo ya kutishia wanachama, wanachofanya ni kutaka kuwafunga midomo wanachama ambao walikuwa na ndoto za kuwania nafasi za juu wasithubutu.
 
Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,404
2,000
Aliyekudanganya Chadema inaisha ni nani au ndo matamanio yako. Tofautisha kati ya matamanio na uhalisia. Chadema is becoming stronger. Ona mtu wenu alivyoumbuliwa na dhambi ya usaliti itaendelea kumtafuna.
 
mary mary

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
869
0
CHADEMA inaisha? ndoto zenu za itakufa kabla ya 2015 zimeyeyuka mnaanza kutapatapa...anyway asanteni CCM kwa promo!
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
mkuu chadema mbona alishakufa angalia viashiria utajua ukweli huu chadema ni mfu kitambo sana hakuna wa kubisha.
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Sasa Kama CDM imeshajimaliza kuna haja gani ya kuianzishia thread? Vinginevyo bado ni tishio kwa mafisadi

hata marehemu wanayo nafasi yao kwenye jamii ndiyo maana mandela kafa lakini watu bado wanamkumbuka.
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
1,195
Una akili ya gani ?

Si ufurahi kama CDM inakufa, unalalama nini.

Hueleweki, shughulika na chama chako.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,863
1,250
Wanaukumbi.

Ninachotaka kuchambua katika huu uzi haina utofauti na mitazamo ya magwiji wa siasa pamoja na wasomi mbalimbali, mgongano wa fikra, kimaono na kimtazamo ambao kwa sasa umeikumba Chadema, ni kiashiria tosha kwamba Chadema kama chama kinazamishwa na Chadema wenyewe.

Wasomi na wapenda amani ambao wapo mitaani na sehemu za kazi wakisema kwa nyakati tofauti kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua madaraka Zitto na wenzake hata bila kuwasikiliza ni kiashiria tosha kuwa chama hicho kinaelekea kufa kifo cha kawaida, Dr. Slaa alikaliliwaakisema hata katiba ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe, hakuna katiba itayaruhusu kufanya mipango ya siri, naye Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alikaliliwa akisema kuwa waraka huo unaeleza mbinu za uasi ambazo zililenga kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki za Chadema.

Kinachoonekana hapa si uhaini kama viongozi wa Chadema walivyotaka kuaminisha jamii bali ni mbinu za kutaka kudumisha uongozi wa kimla, usultani, udikteta, ukanda na kudhoofisha wanachama wa chama hicho amabao wanapigana kwa nia ya kupanua uwigo wa demokrasia ndani ya Chadema, Lissu anajaribu kuingiza vitendo vya malumbano ya kisheria ya mahakama na kuyapeleka kwenye chama, tumeona matokeo ya Kamati Kuu kule Kigoma yaliyomkuta Dr.Slaa na wapambe wake wameishia kupopolewa mawe na kukaribishwa na mabango.

Chadema lazima mkubali inapokalibia uchaguzi wowote ule wagombea wanaowania kuwaondoa walioko madarakani ni lazima watumie ushawishi au utaratibu wa kisiri ili mikakati yao isijulikane kwa wale waliopo madarakani, ni vigumu kuwakuta viongozi wa juu wa chama chochote cha siasa wakijadili maendeleo ya chama huku wamejiachia barabarani.

Tundu Lissu, anachofanya ni kulazimisha taaluma yake ya uanasheria iwe fimbo ya kutishia wanachama, wanachofanya ni kutaka kuwafunga midomo wanachama ambao walikuwa na ndoto za kuwania nafasi za juu wasithubutu.

Hukua na la kuandika ? Mbona unakomaa na Chadema kaka .
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,371
2,000
Teh
MAGAMBA mtaweweseka sana mwaka huu

Rudi darasani ukasome "principles of organization reforming"
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Una akili ya gani ?

Si ufurahi kama CDM inakufa, unalalama nini.

Hueleweki, shughulika na chama chako.

CCM ilipoamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi haikulenga vyama hivyo viwe vinakufa.

Chadema haipaswi kufa, ila isipoheshimu misingi ya demokrasia na uongozi wa kisheria ITAKUFA...
 
CUF Ngangari

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
273
0
Mtei - baba mwenye nyumba
mbowe - mtoto wa mwenye nyumba
Slaa - mpangaji
Lissu - Mchumia tumbo
Lema - Mini kabang
Nashukuru wana kigoma wameanza kuelewa maana walikuwa wanatumika Kama mshumaa
 
Mbanyitege

Senior Member
Jul 2, 2013
181
225
Wewe riz Ndio uliyejimaliza na maccm menzio chadema kamwe haitakufa na mtasubiri sana huo uutabiri feki wa baba yako wasira
 
BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
0
Nilitegemea thread hii ingekua na changamoto kubwa hasa wana cdm kama alivotamba mtoa uzi hapo mwanzoni, lkn kilichofuata baada ya hako ka intro nikaona kinaanza kuubiri wimbo na dhambi ambayo ccm wanaitenda kila cku za maisha yao, yaani udini ukanda ukabila. Hilo limenifanya nirud nisome nani katuma thread, nikapata picha ile inayofanana na thread yenyewe. Ritz, ni lini utakomaa uwe mtoto wa kiume na ufikiri kama mwanaume? (sina nia ya kuwadharau dada zetu) Yani ulete tpic hapa hata sisi tusoshabikia vyama vyenu tuweze kuzisoma?
 
tofyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,690
2,000
Sasa Kama CDM imeshajimaliza kuna haja gani ya kuianzishia thread? Vinginevyo bado ni tishio kwa mafisadi

dada naona umekuja kupambana. wewe unajitahidi kuzuia properganda za udini cdm
upo wewe asha mohammed
mohammed mtoi
some body zuberi.
lazima mtakuwa mnalipwa vizuri. maana mkiona uzi wa ritz lazima mtie maguu.
"endelea kutumika"
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
51,853
2,000
Chama kishakufa wewe unaleta thread gani. Wewe huoni mini kabang badala ya kujenga hoja bungeni yeye anazidi kumponda mwenzake eti apewe majina ayataje?
Maana yake chama kwishney
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom