Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,547
- 47,199
Sote tunakubali kwamba, baada ya nguli wa siasa za upinzani Dr. Slaa kujiondoa Chadema mijadala ya issue sensitive toka Chadema imekoma, zimebakia porojo tu.
Nakumbuka kipindi kile Dr. Akiwa Bungeni, alikua anatoa hoja mujarabu zenye changamoto kwa Serikali na Taifa kwa ujumla. Alikua akiibua mambo ambayo yanafaa kujadiliwa.
Alipokwenda kugombea Urais na baadae kuteuliwa kama katibu mkuu, baada ya kuukosa urais bado aliendeleza kuwa pioneer wa mijadala chanya. Kipindi kile ilikua siasa ya hoja.
Ghafla yakatokea yale tuliyoyaona, akaamua kukaa pembeni tokea kipindi kile Chadema kimeshindwa kua chama kile kilichokua kikivutia baadhi ya watu kwa kuibua hoja zinazojadilika.
Sasa hakuna ubunifu bali ni kudandia mambo tu, kila jambo linalotokea hufuatia na tamko la chama.
Hakuna mtu mwenye weledi wake anayetaka kwenda Chadema akapate doa la kufukuzwa, ila kila mpiga porojo anataka kwenda kule maana watu wengi hupenda mzaha, hivyo ukiongea mambo ya mizaha utapata wafuasi wengi tu. Basi wamepaki wadandia hoja na sio waleta hoja.
Chadema imepoteza mwelekeo limebakia jina tu lililojengwa na walioondoka.