Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema
hawatalipa kisasi hata baada ya mahakama kumfutia kesi ya ugaidi
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare, kwa
kigezo kuwa mashitaka hayo yalikuwa hayajitoshelezi kuitwa kuwa ni ya
ugaidi.
Akizungumza na gazeti hili baada ya hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kuvutia hisia za watu wengi Dk. Slaa
alisema: Tumesema toka mwanzo, tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu
na tutamaliza na Mungu, hujuma zozote dhidi ya CHADEMA kamwe
hazitashinda kwa uwezo wa Mungu.
CHADEMA tunapigania ukombozi wa pili wa taifa letu, tunawapigania
wanyonge, tunawapigania walalahoi. Hatukuwa, hatuna na hatutakuwa na
sababu ya ugaidi.
Source:Tanzania Daima