CHADEMA haitalipa kisasi-Dr Slaa

CHADEMA haitalipa kisasi-Dr Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema hawatalipa kisasi hata baada ya mahakama kumfutia kesi ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare, kwa kigezo kuwa mashitaka hayo yalikuwa hayajitoshelezi kuitwa kuwa ni ya ugaidi.

Akizungumza na gazeti hili baada ya hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kuvutia hisia za watu wengi Dk. Slaa alisema: “Tumesema toka mwanzo, tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tutamaliza na Mungu, hujuma zozote dhidi ya CHADEMA kamwe hazitashinda kwa uwezo wa Mungu.

CHADEMA tunapigania ukombozi wa pili wa taifa letu, tunawapigania wanyonge, tunawapigania walalahoi. Hatukuwa, hatuna na hatutakuwa na sababu ya ugaidi.

Source:Tanzania Daima
 
Na tuyasimamie haya tunayoyasema.
Bado kesi ya Wilfred lwakatare haijaisha!
Sasa najiuliza wale washabiki waliokuwa wanakiita CDM kuwa ni chama cha kigaidi, na wakaahidi kutoa ushahidi iwapo wataitwa mahakamani, wanajisikiaje kwa sasa?
 
Hata mahakamani una anza na kiapo kua uyasemayo sahihi, lkn unadanganya. Tusubiri mahakama mkuu punguza shangwe
 
  • Thanks
Reactions: mij
MaCCM yanatapatapa tu, wacha tuyasamehe...eti UGAIDI? wanapanga na kuongea kishetani bila hata kufikiria..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MaCCM yanatapatapa tu, wacha tuyasamehe...eti UGAIDI? wanapanga na kuongea kishetani bila hata kufikiria..
 
Nilitegemea kuwa waliotoboa Mv Bukoba, Waliozamisha meli kule znz, waliohamasisha maelfu kwenda samunge, waliosababisha wanafunzi kufeli, waliowafanya madaktari kutoa huduma kulingana na kiasi wanacholipwa na kupelekea vifo kuongezeka, wenye kusababisha Tembo kutoweka, Wenye kusababisha kupanda kwa gharama za maisha, Waliosababisha Lowassa kuutema u-PM ...wangeitwa MAGAIDI badala ya sasa wanajiita wazalendo chini ya serikali sikivu ya CCM isiyojali wananchi wake...
 
Watashindana lakini tutashinda kamwe nuru haizidiwi na giza!!
 
Watashindana lakini tutashinda kamwe nuru haizidiwi na giza!!
 
Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema
hawatalipa kisasi hata baada ya mahakama kumfutia kesi ya ugaidi
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare, kwa
kigezo kuwa mashitaka hayo yalikuwa hayajitoshelezi kuitwa kuwa ni ya
ugaidi.

Akizungumza na gazeti hili baada ya hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kuvutia hisia za watu wengi Dk. Slaa
alisema: “Tumesema toka mwanzo, tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu
na tutamaliza na Mungu, hujuma zozote dhidi ya CHADEMA kamwe
hazitashinda kwa uwezo wa Mungu.

CHADEMA tunapigania ukombozi wa pili wa taifa letu, tunawapigania
wanyonge, tunawapigania walalahoi. Hatukuwa, hatuna na hatutakuwa na
sababu ya ugaidi.

Source:Tanzania Daima
hawa lolote cdm nimagaidi tu.
 
Sijui waliokuwa wanaishambulia CHADEMA na kukiita chama cha kigaidi wanajisikiaje sasa,kuna mambo mengi ya kujifunza na kuendesha siasa zenye kuangalia hali ya baadae itakuaje,tunasubiri kesi ya Lwakatare iishe ili ukweli ujulikane.
 
Asante Dr. Slaa umenena vema.
 
Nadhani kuna mchezo umechezeka kati ya mahakama na cdm ili kuifuta kesi kwa 7bu wanazozijua wao mbona viongozi wajuu wa cdm walitanguliza kutoa kiapo cha kuiamini mahakama wakati wao wako against mahakama na vyombo vya usalama vya serikali? Hapa kuna alama ya kuuliza?
 
Hii ni aibu kwa Nchemba na kwa wafuasi wake wote! Tambueni ya kuwa Ubaya siku zote hauwezi kuushinda Wema'
 
Asante Dr. Slaa umenena vema.
 
Hii ni aibu kwa Nchemba na kwa wafuasi wake wote! Tambueni ya kuwa Ubaya siku zote hauwezi kuushinda Wema'
 
Ujumbe sahihi kwa muda muafaka

Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
CDM tuko na MUNGU CCM wao na Shetani.Ni dhahiri nguvu ya mungu ni KUU kabisa.
 
Back
Top Bottom