CHADEMA haitakufa kwa kuchoma ofisi


Tangu kale katabia ka wanasiasa kuhama chama kimoja na kujiunga na chama kingine ni jambo la kawaida sana katika siasa.

Duniani kote wanasiasa huyumba hufuata upepo wa kisiasa. ikiwa upepo utaonesha chama fulani kina mvuto, basi wengi watajiunga, lakini upepo huo wa kisiasa ukisimama au kubadili uelekeo nao pia hubadilika.

upepo wa kisiasa kuwakumba wanasiasa vibaraka, vigeugeu na wasaliti ambao ni rahisi kurubuniwa au kuhongwa na vyama nyenye ukwasi. Vibaraka huwa hawana msimamo, wao hufuata mkumbo au watu ila wenye msimamo hufuata sera za chama.

Ndiyo maana hatushangai hiki kinachoonekana katika chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa baadhi ya wanachama kujiondoa na kujiunga na CCM. Kati ya mwaka 2010 na 2012 tena baada ya CCM kupata ushindi mnono, tulishuhudia mamia kwa maelfu ya wanasiasa wakihama na kujiunga na CHADEMA.

Tulidhani, wakati ule walikuwa wanafuata sera za chama hicho, lakini baada ya kuzuka usaliti ndani ya chama na wasaliti kuondolewa tumeshuhudia watu wakihama CHADEMA na kujiunga na CCM.

Hiyo ni haki yao ya kidemokrasia lakini hali ilivyo inaelekea CHADEMA ilikuwa imebeba mamluki, wasaliti na vibaraka. Maana kama si vibaraka inakuwaje kusimamishwa (Sio kufukuzwa) viongozi watatu kuibue wimbi la wanachama kujitoa na kujiunga na CCM?

Je, viongozi hao wakikiri makosa wakasamehewa na kurejeshewa vyeo hao waliojiunga na CCM watarudi tena CHADEMA? Haiwezekani siyo?

Kama si vibaraka ni nani? kwa nini waliohama wanatoa matamko ya kuzuia ziara za mikoani zilizoandaliwa na viongozi na viongozi wa CHADEMA makao makuu wakati hawahusiki?

Kama si vibaraka ni nani? kwa nini waliohama wanatoa matamko ya kuzuia ziara zinazoandaliwa na viongozi wa CHADEMA makao makuu wakati hawahusiki?

Kama si vibaraka kwa nini waliohama wako mstari wa mbele kuandamana na kutishia kuwadhuru viongozi wa chama kisichowahusu?

Kama CHADEMA kimekwisha hakina sera kwa nini waliohama wanavamia na kuchoma ofisi za chama kilichokwisha?

Mwanachama anayejua anachosimamia hawezi kuwa mgomvi, kuanzisha vurugu kufanya hujuma kama kuchoma ofisi. hujuma hizi zinawafunua kuwa wao ni vibaraka.

CHANZO: Mawio Uk 6.

Mtoi
Nadhani huelewei kuwa siasa kwa Tanzania ni moja ya sehemu ya ulaji,hakuna mwanasiasa hata moja ktk taasisi hizi za siasa mwenye moyo wa dhati wa kufanya kazi kwa ajili ya wananchi,vyama vingi vipo kwa ajili ya maslahi na ndio maana maslahi yanapopotea ndipo mifarakano inapoanza,mambo huwa mazuri kama tu flow ya kile kinachotafutwa kinapatikana na kiwe kinapatikana kwa usawa la sivyo kunakuwa na mgongano na mwishowe taasisi hufa.
Yawezekana kabisa kuchomwa kwa ofisi kusisababishe chama kufa,lakini misingi ya kuongoza taasisi itakapoteteleka huo ndio mwanzo wa nyumba iliyoshikiriwa na msingi huo mbovu huanza kutoa nyufa na kama zisipozibwa basi wezi huchungulia.
Wanasiasa,tunaomba,fanyeni kazi kwa maslahi ya watu waliowafanya muwepo,na muepuke kuweka maslahi yasiyoweza kuifaidisha nchi hii yenye zaidi ya watu milioni 40.
Siasa imekuwa ni kichaka cha watu kujificha,watu wanatumia siasa kufanya wasiyoyaweza nje ya siasa.
 
Una uislamu gani wewe?
Au hilo jina?
We hujui kuwa kuna makafiri wengi tu wana majina kama lako?
Au nikupe mfano.
Haya angalia hawa ni ndugu yako pia!? Abdulhalim na huyu mwanao? Asha mohamed ??
Katika hoja za KIMASIKINI kabisa zilizoletwa kwenye jukwaa hili , hii yako iko nafasi za juu sana , kwani uislamu ni nini ? ama labda waislamu unaowajua wewe na akina nani na kwanini? NIMEKUDHARAU SANA !
 
sawa kamanda wa ukweli.

Ajira za watanzania zimekuwa kuokota makopo na vyuma chakavu hizo ndo ajira za ccm.
 
Sijaona mahali ulipoandika chochote kuhusu kifo cha Mzee Mandela, au ni kwa kuwa nae ni "mkatoliki"?

Kifo kifo, kifo hakina huruma. Niandike nini sasa zaidi ya anavyoandikwa na magwiji wa kuandika na wanaomjuwa zaidi yangu? awe mkatoliki au asiwe mkatoliki inahusu nini?

Alazwe anapostahiki.

Dead man don't count.
 
Kifo kifo, kifo hakina huruma. Niandike nini sasa zaidi ya anavyoandikwa na magwiji wa kuandika na wanaomjuwa zaidi yangu? awe mkatoliki au asiwe mkatoliki inahusu nini?

Alazwe anapostahiki.

Dead man don't count.

So is Nyerere alive? And if he is not, why bother with someone who doesn't count?
 
News Alert: POLISI: CHADEMA inahusika na moto Arusha.

Habibt FaizaFoxy
Kama unavyojua ugumu wa maisha umefanya Mohamedi Mtoi asijielewe; haelewi hata anachoakiandika mwenyewe; sisi tulitegemea yeye akiwa mwandishi wa habari atuletee habari sahihi bila kujali itikadi yake huyu mtu hana tofauti na kirusi kwenye jamii anatumia kila aina ya uandishi uliojaa uongo ili kujipendekeza kwa mabwana zake huyu ni mganga njaa kama alivyo Ben Saanane; Mwita Maranya; Mikael P Aweda; Yericko Nyerere Molemo; Matola hawa watu ukiwasoma unawatoa thamani kabisa yaani najiuliza huu utumwa wa akili wameutoa wapi karne ya 21 tulitegemea Tanzania tuwe na vijana wenye maono ya maendeleo lakini hawa wameguka hasara na mzigo mkubwa kwa taifa
 
Last edited by a moderator:
Habibt FaizaFoxy
Kama unavyojua ugumu wa maisha umefanya Mohamedi Mtoi asijielewe; haelewi hata anachoakiandika mwenyewe; sisi tulitegemea yeye akiwa mwandishi wa habari atuletee habari sahihi bila kujali itikadi yake huyu mtu hana tofauti na kirusi kwenye jamii anatumia kila aina ya uandishi uliojaa uongo ili kujipendekeza kwa mabwana zake huyu ni mganga njaa kama alivyo Ben Saanane; Mwita Maranya; Mikael P Aweda; Yericko Nyerere Molemo; Matola hawa watu ukiwasoma unawatoa thamani kabisa yaani najiuliza huu utumwa wa akili wameutoa wapi karne ya 21 tulitegemea Tanzania tuwe na vijana wenye maono ya maendeleo lakini hawa wamegeuka hasara na mzigo mkubwa kwa taifa

Nawasikitikia sana wazazi wao, kwani kama usemavyo hawana "thamani kabisa". Badili ya kujikomboa kwenye huo "utumwa wa akili" wao ndio wanaushadidia na kuuona kuwa ndio njia sahihi bila ya kujijuwa nafsi zao. Wanasikitisha sana, lakini aah, kama Waswahili wanenavyo "...halisikii dawa".
 
Katika hoja za KIMASIKINI kabisa zilizoletwa kwenye jukwaa hili , hii yako iko nafasi za juu sana , kwani uislamu ni nini ? ama labda waislamu unaowajua wewe na akina nani na kwanini? NIMEKUDHARAU SANA !

kwani wewe ukiniheshimu naongezeka nini?? jenga hoja na kejeli waachie walevi. hii ndio kazi na dhumuni la jukwaa
 
Back
Top Bottom