Chadema: "Dk Slaa Kinara Utafiti wa Synovate!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: "Dk Slaa Kinara Utafiti wa Synovate!"

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Sep 20, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwa ana taarifa za matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Synovate zinazoeleza kuwa mgombea wa chama chake, Dk Willibrod Slaa aliongoza kwa kukubalika, lakini taarifa hizo hazikuwekwa bayana.

  Wiki iliyopita Synovate, ambayo imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ilitangaza matokeo ya utafiti wake juu ya jinsi ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti habari za uchaguzi mkuu, lakini taarifa hiyo haikuwa na kipengele ambacho kinazungumzia umaarufu wa wagombea na nani angeweza kushinda kama uchaguzi ungefanyika sasa.

  Lakini Mbowe amesema anazo taarifa kuwa Synovate wamefanya utafiti unaoonyesha kuwa Dk Slaa anaongoza kwa asilimia 45 na kufuatiwa na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye Mbowe alidai amepata asilimia 41.

  "CCM haitaki matokeo haya yatangazwe," alidai Mbowe wakati akihutubia umati mkubwa wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Isanja ulio Sanya Juu mkoani hapa.

  "Synovate haitakiwi iiogope CCM, itangaze matokeo ya utafiti wake bila ya kubadili ukweli.
  "Tuna hizo taarifa na niwaambieni tu, Synovate walifanya utafiti kujua ni mgombea gani na chama gani kinakubalika na utafiti wao unaonyesha kuwa Chadema inaongoza kwa asilimia 45 na CCM ina asilimia 41. Lakini, CCM inawatishia wasiitoe ripoti hiyo."


  Mbowe, ambaye aligombea urais mara moja kabla ya kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, aliongeza kusema: "Nawataka Synovate watoe matokeo ya utafiti huo kwa kuwa ni muhimu sana kwa wananchi kuyatambua na kujua nini kinaendelea."

  Juhudi za kuwapata Synovate kuelezea kama utafiti kama huo umefanyika, hazikufanikiwa.
  Mbowe alisema kuwa nchi kwa sasa iko kwenye msiba mkubwa wa umasikini na kwamba uchaguzi mkuu ujao Oktoba 31, ndiyo njia pekee ya kuondokana na msiba huo.

  "Njia pekee ya kuondokana na msiba huu ni kuiweka Chadema madarakani ili kuondokana na umasikini uliokithiri," alisema Mbowe.

  Naye Dk Slaa alieleza kushangazwa na ahadi za Kikwete za kupandisha hadhi hospitali wakati zahanati zilizopo sasa hazina dawa.

  Akiwahutubia wananchi wa Arumeru kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Usa River, Dk Slaa alisema kuwa ahadi hizo za Kikwete ni kiini macho kwa kuwa zinatoka wakati zahanati hazina dawa na wananchi wanaendelea kuteseka.

  Kikwete ameahidi kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN).

  Kutoka Kondoa, Fidelis Butahe anaripoti kuwa Kikwete aliwaahidi wananchi wa Kata ya Mrijo, Kijiji cha Mrijo atawapatia trekta la kulimia.

  Kikwete alitoa ahadi hiyo baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho, Rashid Mdundo kusimamishwa na mgombea huyo wa urais aeleza matatizo ya wananchi wa kijiji hicho.
  "Shule za kata zote hazifundishi masomo ya sayansi na hakuna umeme, idadi ya walimu haitoshi, maji pia ni tatizo," alisema Mdundo,

  "Hapa kuna kisima kirefu tangu enzi za mkoloni, lakini kutokana na watu kuongezeka kwa wingi maji hayatoshi kabisa, kuna migogoro kati ya wakulima na wafugaji."

  Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa matatizo mengine katika kijiji hicho ni ajira, kijiji kuwa mji mdogo pamoja na kutokuwa na barabara bora.

  Kikwete, ambaye aliwasili kijiji hapa saa 9:15 alasiri aliwaahidi wananchi hao kuwa atawadhamini ili wapate mkopo wa trekta kwa ajili ya kulimia.

  "Hili suala la kilimo nitawasaidia; cha kufanya nyinyi ni kuunda kikundi na mimi nitawasaidia ili mpate trekta kwa ajili ya kufanya shughuli zenu za kilimo bila kupata tatizo lolote, hii ni ahadi yangu na naahidi kuwa nitaitekeleza," alisema Kikwete.

  Kuhusu tatizo la umeme, Kikwete alisema: "Nimeona nguzo hapa sasa kama mnasubiri rais awavutie huo umeme jamani tutafika. Hii ni biashara; zungumzeni na watu wa Tanesco kwa kuwa wanafanya biashara."

  Aliwaahidi wananchi wa kijiji hicho kulifuatilia kwa ukaribu tatizo la maji katika kijiji hicho pamoja na kuiboresha barabara ya Handeni-Kondoa mpaka Singida kwa kuwa ipo katika ilani ya CCM.


  Source: MWANANCHI.
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mbona Synovate wenyewe wamekanusha? au tunalishwa propaganda ambazo hazijapikwa zikaiva sawasawa?
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unategemea JK atawaruhusu watangaze matokeo hayo?
   
 4. h

  hagonga Senior Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sidhani, nahisi bado ccm wamewakaba synovate kwelikweli,kwa jambo kama hili siamini kuwa Mbowe aweza kusema tu from no where.

  Mimi nasema si kitu, wananchi teendelee kucampain kila mahali maana hata Vyombo vya habari hasa Television wamewabana sana chadema ujumbe wao usiwafikie wnananchi kama walivyo ccm.
   
 5. M

  Masauni JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Just simple logic, synovate wamezuiwa kutoa kitu cha kweli kilicho katika utafiti wao(uwezi toa utafiti wako usiongelee swala la mgombea gani anakubalika) nao wamekubali kuficha. do you think watakuja kusema hadharani kwamba tulificha matokeo that is impossible.
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wakuu tusibweteke. kazi kubwa ipo mbele.
  Dola imejiALIGN nyuma ya CCM kukisaidia chama kwa hali na mali.
  Kama mnabisha angalia hizi clues.

  Mkuu wa majeshi mstaafu Mboma ni ccm mkongwe ilihali wanajeshi hawaruhusiwi kushiriki siasa
  Vivyo hivyo wa Mahita na Tibaigana ambao kiuhalisia bado wanatumikia viapo vyao kwani wamejiunga kwenye jeshi la akiba. Mwangalie Hansy Kitine yupo wapi leo? ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Mnadhani hawa na wengine waliostaafu wameondoka na mizizi yao huko walipotoka? Hasha bado wana-damu zao kwenye mfumo.

  IMEKULA KWETU KAMA TUTALALA
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pia mzee wa kulikoni ughaibuni alimuuliza kiongozi wa Synovate Aggrey Oriwo aksema yeyusha kimtindo KULIKONI UGHAIBUNI
   
 8. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa synovate mimi siwaamini hata kidogo kwani mimi nimeshawahi kuwafanyia kazi wakati ule inaitwa steadman group. Nayajua mimi mazingira ya hao wafanyakazi na wanavyo pikwa kulazimisha jawabu.

  Na mara nyingi wafanyakazi wao huwa wanajichimbia vyumbani na kuzijaza quationers zao bila hata kuwauliza walengwa.

  Lkn niwaulize tu ndugu zangu: kwa nini ule utafiti wa synovate uliompa kikwete 68% mbona tuliupinga sote kwa pamoja? Au mkuki kwa ngurue tu?

  Tukumbuke kua utafiti ule pia ulimpa maalim seif ushindi kule zanzibar lkn profesor lipumba aliukataa na dr slaa pia.

  Tukae tukijua kua hapa hatuna shirika huru la utafiti ispokua tuna wasemaji wa ccm tu. Mimi binafsi siamini kua synovate wanaweza kufanya utafiti na kumfanya dr slaa aongoze kwani tokea unapopewa quationer yako kwenda kuhoji unaambiwa mapema kua jawabu ni lazima iwe .........

  Kama tunataka alau utafiti ambao huenda tukaukubali kulingana na mazingira ya huo utafiti wenyewe basi labda alau tuwambie BBC waje wafanye lkn kwa synovate hamna kipya.
   
 9. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa synovate mimi siwaamini hata kidogo kwani mimi nimeshawahi kuwafanyia kazi wakati ule inaitwa steadman group. Nayajua mimi mazingira ya hao wafanyakazi na wanavyo pikwa kulazimisha jawabu.

  Na mara nyingi wafanyakazi wao huwa wanajichimbia vyumbani na kuzijaza quationers zao bila hata kuwauliza walengwa.

  Lkn niwaulize tu ndugu zangu: kwa nini ule utafiti wa synovate uliompa kikwete 68% mbona tuliupinga sote kwa pamoja? Au mkuki kwa ngurue tu?

  Tukumbuke kua utafiti ule pia ulimpa maalim seif ushindi kule zanzibar lkn profesor lipumba aliukataa na dr slaa pia.

  Tukae tukijua kua hapa hatuna shirika huru la utafiti ispokua tuna wasemaji wa ccm tu. Mimi binafsi siamini kua synovate wanaweza kufanya utafiti na kumfanya dr slaa aongoze kwani tokea unapopewa quationer yako kwenda kuhoji unaambiwa mapema kua jawabu ni lazima iwe .........

  Kama tunataka alau utafiti ambao huenda tukaukubali kulingana na mazingira ya huo utafiti wenyewe basi labda alau tuwambie BBC waje wafanye lkn kwa synovate hamna kipya.
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Synovate waganga njaa hao..........hawana lolote
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hawana lolote ndio maana wanaficha matokeo ya utafiti?
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Habari ndo hiyo.......Wasanii tu hao

  Fanya ufuatilie historia yao tangu wakiwa Steadman(japo kwa kidogo tu) utawajua ni watu wa aina gani

  Waganga njaa tu hao
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ngoja nitafuatilia historia yao! Yaani wanaganga njaa kama Richard Kiyabo aliyejiunga na vyama vitatu kwa mwaka!
   
 14. m

  mapambano JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  source:HabariLeo | Synovate:Mbowe muongo
  Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 21st September 2010 @ 08:30 Imesomwa na watu: 355; Jumla ya maoni: 9

  TAASISI ya utafiti ya Synovate imesema haijafanya utafiti wowote kuhusu wagombea wa nafasi za urais unaoonesha kuwa mgombea wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa anakubalika zaidi na wananchi.

  Baadhi ya vyombo vya habari (si gazeti hili) jana vilimnukuu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema kuwa Chadema ina matokeo ya kura za maoni za Synovate yanayoonesha kuwa Dk. Slaa anakubalika kwa asilimia 45 akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 41.
  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mbowe anadaiwa kusema kuwa takwimu hizo hazikutolewa Septemba 14 walipotoa taarifa za namna vyombo vya habari vinavyoripoti kampeni za uchaguzi mkuu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Meneja wa Synovate, Aggrey Oriwo alisema taarifa hizo ni za kughushi, hazina ukweli wowote na zinaupotosha umma kwa kuwa hawajawahi kufanya utafiti wowote unaohusu kukubalika kwa wagombea wa urais.

  “Kauli ya Mbowe imetukera sana na magazeti yalioandika pia yametukera, hakuna ukweli wowote na sisi ni kampuni huru, hatuwezi kubania taarifa yoyote, hatuegemei upande wowote, tayari tumewasiliana na vyombo husika vya habari na tumeandika barua kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kulalamikia suala hilo,” alisema Oriwo na kumtaka Mbowe kuweka bayana ushahidi kuhusu takwimu hizo.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya jana, Mbowe alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro.

  Alidai sababu za kutotolewa utafiti huo zinatokana na CCM kuikataza taasisi hiyo kufanya hivyo. Meneja huyo hakuwa tayari kuweka bayana kama watafanya utafiti kuhusu wagombea hao kwa madai kuwa wakati huu wa kampeni utafiti kama huo una hatari.

  Alisema kazi zao zina mipaka na utafiti kama huo ukifanyika, watautoa kwa jamii kupitia vyombo vya habari kama ambavyo wamekuwa wakifanya.

  HABARILEO jana ilimtafuta Mbowe kuzungumzia suala hilo bila mafanikio na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alipoulizwa alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa kipindi hiki cha uchaguzi, msemaji wa chama ni Mwenyekiti (Mbowe) au Kaimu Katibu Mkuu, John Mnyika ambaye naye hakupatikana jana.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba naye hakupatikana jana baada ya kutafutwa kwa simu kuzungumzia kuhusishwa kwa chama hicho katika suala hili.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mods -- unganisha post hii na ile nyingine iliyoanzishwa kuhusu issue hii.
   
 16. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Japokuwa kwa utafiti nilioufanya mimi Dr Slaa mpaka sasa anaongoza, bado Synovate wakikiri hivyo sitawaamini.

  Hawa jamaa nimewapinga sana hapa JF pamoja na huo 'u-international' wao. Yaani siwatofautishi na kina CCJ. Hao ni watu wanaocheza na hisia za watanzania ili kushibisha matumbo yao. Na mwaka huu Mwenyezi Mungu apasue vitambi vyao...vitoke mafuta ya uongo, utapeli na ufisadi.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kwa nn hawakufanya utafiti basi? Kwani last election si walifanya?...wamesoma upepo nn
   
 18. m

  mapambano JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  jamani hiki ndio chama kinachodai kina uwezo wa kuongoza TANZANIA YETU! Wameanza ufisadi mapema
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  My goodness kumbe SYNOVATE ndio the former STEADMAN.
  Nilifanya nao kazi for 3 years nawafahamu fika hao jamaa na washawai tugombanisha na mteja wetu ikafikia kwenda makao yao makuu kule Nairobi.
  Wamepinda na wanaogopa kufukuzwa
   
Loading...