Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 91
- Thread starter
-
- #21
Napenda sana kwa vyama hivi vife kipo cha natural death ili tupate watu makini na walio na uchungu wa Kweli na Taifa letu Tanzania. Na pia kuna kila Dalili kwa CHADEMA kupewa au kusurvival katika mabadiliko haya, na pia hata haya ya CUF ni mtikisiko ambao utavikumba vyama karibu vyote, Kizazi cha Dot.com kinakuja na wala hawawezi kuzugwa na mambo ya CCM. Sisi tunasema kuwa mwanga wa Kweli upo mlangoni ni vyama husika kuona vinajitayarisha kukubali matokea haya. Chadema Kina Kizazi ambacho wao wanaweza kujua na kutambua na pengine hata CCM watashindwa kujua alama hizi na kutojua miiko yao ya uongozi na ndio maana unaona more contradicts za ajabu kati yao kuhusu ufisadi.Nina imani kubwa kuwa pole pole mambo yanabadilika - miaka 40 na ushee ina madhara yake na inachukua muda kudadilisha mtazamo katika jamii. Ni kweli muumgano wa vyama vya upinzani hauwezi kuwa rahisi kwani viongozi wake wengi ni uzao wa ukiritimba wa chama kimoja. Hata hivyo naanza kuona dalili za kizazi kipya kinaanza kupenya kwenye hizi anga na wazee pole pole wanawekwa kando. Muda si mrefu kuna vyama itabidi vife "natural death".
Chadema imeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika hili wimbi hili la mabadiliko ya fikra. Tunaanza kuona viongozi wa vyama wakitofautiana wazi wazi na wanachama wao kwenye uchaguzi kama wa Tarime. Tulishuhudia kwa mfano wanachama wa NCCR wakitofautiana na viongozi wao na kushirikiana na Chadema licha ya maelekezo kutoka makao makuu kuwa wasitoe ushirikiano. Pia katika uchaguzi wa Busanda nina hakika wanachama wa CUF waliipigia kura Chadema.
Kuhusu Biharamulo pamoja na CUF kupoteza kada wake maarufu kwa Chadema, ni wazi waliokuwa wanachama wa CUF watakuwa nyuma ya mgombea wa Chadema na hivyo hivyo NCCR. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chadema hivi sasa inaanza kuwa tishio kwa vyama kamaa NCCR, CUF, UDP, na vyama vingine vya upinzani na viongozi wake wanaanza kuinyooshea vidole Chadema badala ya CCM. Hili ni thibisho kuwa Chadema ina kila sababu ya kujiita chama mbadala.
Wazo la kutaka vyama viungane hivi sasa vina lengo la kuidhoofisha Chadema na mimi ningewashauri wawe waangalifu sana kwenye hili. Kuna kila dalili kuwa hivi vyama tayari vinachungulia kaburi na vina hatari ya kutumiwa - ushauri wangu ni kuwa kama chombo kinazama, wakati wa kutoka ni sasa kama alivyofanya Lwakatare. Wale wasioipenda Chadema wanaweza kurejea CCM lakini wale walio na nia ya kweli ya kulikomboa taifa mikononi mwa mafisadi, wajiunge na Chadema.
Kama kawaida woga unawaingia CCM
Homa ya Chadema umelitikisa Bunge
Mwaka 2010 wengi wataachwa kwenye mataa.
Labda Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi
ziipakate CCM - kama kawaida yao.
CHADEMA WANaweza kufanikiwa kama wakijipanga vizuri. hivyo kama upinzania wa kweli upo mijini kwanini wabunge wengi wanatoka Mikoani na sio Mijini?? Watu wanasubiri CHama Mbadala na wana Hamu ya kuona haya. Tazama na sikia watu kwenye Vituo vya Mabasi, Kwenye Daladala watu wamechoka kabisa ,na hata maisha pia wamechoka, Serikali imechoka, vyama Vimechoka na watu wamechoka. Nani Mkombozi wa Kweli TanzaniaCHADEMA ingeongeza nguvu mikoani wilayani na vijijini, ikakamata majimbo mengi ili idadi ya wabunge waongezeke na wanachama waongezeke....wananchi wengi hawapati hizi habari kama tunavyozipata wa mijini.
Halafu hizo sera za CHADEMA kuzimwaga hadharani si ni kuwapa mwanya CCM kuiga na kuwamaliza?
Sasa wewe unataka waseme nini kama hawpo kwenye serikali. Hivyo tu kusema tutfanya hivi ama vile ni tosha kabisa kuongoza Serikali. Vyama vya Upinzani ni mbdala ya serikali navyo vinaongoza Serikali tarajiwaIla ni muda upinzani nao ukawaelimisha vizuri juu ya sera zao. Vyama vingi vya upinzani havisemi wao vitafanya nini bali wana kazania tu na CCM wameshindwa kufanya nini. Sasa kwa mwananchi wa kawaida atajuaje kuwa na wewe unaweza fanya kazi bora kuliko ya CCM? Je CCM isipo kosea na upinzani watakosa cha kusema? It is time upinzani ukakazania kujiimarisha badala ya kujaribu tu kuiua nguvu CCM. Ikija kwenye maneno ya jukwaani na kutumia pesa upinzani hawawezi kuishinda CCM. Ni muda muafaka sasa upinzani kujiwekea mikakati ya muda mfupi na mrefu. Ni muda sasa wa upinzani kusema sisi tutafanya hivi. Ni muda sasa upinzani ukatambua kuwa kila uchaguzi ukiisha basi kampeni zingine zimeanza na siyo kusinzia kwa miaka mitano uchaguzi mwingine ukifika wana lalamika hawana uwezo wa kutembelea majimbo yote. It is time they set realistic goals na kuacha ndoto za alinacha. Inabidi waone sasa kuwa mikakati yao mpaka muda huu imeshindwa na wanabidi wajipange upya.
Sasa wewe unataka waseme nini kama hawpo kwenye serikali. Hivyo tu kusema tutfanya hivi ama vile ni tosha kabisa kuongoza Serikali. Vyama vya Upinzani ni mbdala ya serikali navyo vinaongoza Serikali tarajiwa
Nafikiri waheshimiwa tunasahau kitu kimoja.Si jukumu la chadema pekeyake kuiondoa CCM ni jikumu la kila mtanzania ambaye amechoka na hasa vijana
kushiriki kikamilifu kwenye gurudumu la siasa
Mfano wakati wa mbio za kugombania uhuru vijana wakina mchonga walivyopambana
Watu wanajua nini vyama hivi vitafanya na pia kujua kama watafanya nini, labda kwa sababu wewe umemezwa na ukada na kuwapo muda mrefu katika chaka chako
Hapana Shaka kuwa lazima tufanye hivyo lakini inabidi tupate wapapandaji hodari sana na mahiri sana huku wakisaidiana na watu wengine makini sana katika kufanikisha haya malengoSi hilo tu mkuu, hili pia ni swala ambalo tumekuwa tukilipinga hapa, la serikali kuundwa na wabunge! Tunacho tegemea ni chama mbadala kama kitashinda uchaguzi, kinachukua vichwa safi kama Magufuri bila kujali itikadi ya mtu, na kuvipa post bila kuendekeza uswahiba na umwenzetu, vichwa vina badilisha utendaji kazi maramoja. Na kwa resources tulizo nazo ni myaka mitano tu, mambo yatakuwa yamebadilika sana!
Mfano ni kuchukua pesa ambazo serikali ina zitumia vibaya kama vile za chai, safari za wakubwa zisizo na tija, mashangingi, na kuzielekeza maramoja katika kitu kimoja, mfano kilimo, yaani within 2 yrs mabadiliko yataonekana. Na hiki ndicho tuna kikosa CCM ambao wamesahu jukumu lao badala yake wamebaki kutetea uozo wao kwa garama yoyote zile!
Watu wanajua nini vyama hivi vitafanya na pia kujua kama watafanya nini, labda kwa sababu wewe umemezwa na ukada na kuwapo muda mrefu katika chaka chako
Tunaweza kuifanya serikali ya pamoja na watu kuwa na wajibu wa kuwajibika na kuleta maendeleo ya watu wote